Kuundwa kwa baraza la wapambanaji wana chama wa chadema

Expedito Mduda

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
522
240
Ndugu zangu wa JF, kuna mwenzetu mmoja ametoa wazo nzuri sana mi nimelipenda sana. Amependekeza kuwa tuunde baraza la wanachadema kwa ajili ya mapambano ya 2015. nafikiri utaratibu huu ukifanyika unawenza kutusaidia tusijisahau. Kumbukeni kuwa mwisho wa uchaguzi uliopita ulikuwa mwanzo wa maandalizi kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2015.
Nawaomba kama kuna mawazo zaidi basi tuwasiliane kwa 0753903809.
Ndugu zanguni nchi yetu hii inahitaji kukombolewa!
VIJANA TUSILALE TUIKOMBOE NCHI YETU KWA AJILI YA KIZAZI HIKI NA VIZAZI VIJAVYO!
 
Wazo zuri. Ni aibu watu kupita bila kupingwa!

Vile vile ni vema tukawasaidia wabunge wa upinzani walioingia bungeni, kwa hali na mali, ili wafanye vizuri katika majimbo yao. Itakuwa ni aibu, kwa mfano, jiji la mwanza lisipo kuwa mfano wa majiji bora tanzania. Forum hii iwasaidie mawazo wabunge.
 
Wazo ni zuri lakini ukumbuke chadema kama chama cha siasa kina katiba yake ambayo pamoja na mambo mengine inatoa muundo wa chama hicho. Sina uhakika kama muundo uliotolewa chini ya katiba hiyo unatoa nafasi kwa hilo Baraza. Hata hivyo kwa maoni yangu hilo alikatazi wapenzi na wakereketwa wa chadema kubuni mfumo utakaosaidia kuunganisha nguvu zao katika kuisadia chadema kufanikisha ukombozi wa pili wa nchi yetu.
 
Yaani hilo baraza sijui tuite Urafiki wa wana CHADEMA! Si maanishi organ ambayo itahitaji usimamizi wa chama! Labda nisema tuunde mtandao wa marafiki wa CHADEMA kwa ajili ya kupeana mawazo na kujua kinachoendelea majimboni. Tuungane ili tupate nguvu!
 
tuko pamoja, nataka nianze mchakato wa jimbo la kinondoni
 
Ni wazo jema. Utekelezaji au evaluation yake iwe kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2014. Nitafurahi sana kama wazo hili litaungwa mkono ili by January 2015 kwa mfano mambo yafuatayo yafanyike (lakini kwa baraka za Chama hasa kupitia Bavicha)
1. Wagombea walau watatu wa nafasi za ubunge wawe wamejulikana kwa majimbo yote Bara na visiwani
2. Nguvu ya Chama iwe imeongezeka hasa maeneo ya mikoa kama vile Mtwara, Dodoma, Moro, Tanga, Lindi pamoja na Visiwani
3. Uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2014 tushinde kwa kiwango kisicho pungua asilimia 50.
4. Kila jimbo walau liwe limeanda volunteers wasiopungua 30 wasio na njaa na wenye uelewa wa mambo yanayohusu uchaguzi na serikali au siasa kiujumla.
5. Ianzishwe fundraising programme ikiwezekana ili kuepuka hujuma kama ilivyotokea kwa ile programme ya simu
6. Tuwape mapendekezo kwa viongozi wa chama ili kuanzisha vyombo vya habari vya chama mfano magazeti badala ya kutegemea vyombo vya habari vya watu binafsi mapema kabla ya 2012.
7. Kuimarisha kurugenzi ya vijana (Baraza la vijana-Bavicha) ili kukabiliana na propaganda chafu (Simaanishi Green Guard). Hawa wawe spesho kwa ajili ya kukabiliana uhuni wa UVCCM hasa kuwapaka matope viongozi wa chadema.
8.Sisi wenye wana JF tuanze sasa kutangaza nia kwa ajili ya majimbo na kata zote hapa nchini huku tukiandaa fungu (capital) kwa ajili hiyo. Mimi natangaza nia katika jimbo mojawapo katika mkoa mpya wa Njombe baada ya vumbi la uchaguzi uliopita kuanza kutulia.

Naomba kuwasilisha
 
bonge la wazo i ever heard.tuungane kwa kuanza tujulishane tuko pande za wapi.uhakika katika kila chuo wapo wanaharakati wengi tu kama sisi.halafu organisation ikiwa kubwa tufanye kuonana tunapanga sikumoja tunakutana TANGAZO LITAWEKWA HUMUHUMU.kisha tunaendeleza mchakato au sio jamani?
 
Ni wazo jema. Utekelezaji au evaluation yake iwe kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2014. Nitafurahi sana kama wazo hili litaungwa mkono ili by January 2015 kwa mfano mambo yafuatayo yafanyike (lakini kwa baraka za Chama hasa kupitia Bavicha)
1. Wagombea walau watatu wa nafasi za ubunge wawe wamejulikana kwa majimbo yote Bara na visiwani
2. Nguvu ya Chama iwe imeongezeka hasa maeneo ya mikoa kama vile Mtwara, Dodoma, Moro, Tanga, Lindi pamoja na Visiwani
3. Uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2014 tushinde kwa kiwango kisicho pungua asilimia 50.
4. Kila jimbo walau liwe limeanda volunteers wasiopungua 30 wasio na njaa na wenye uelewa wa mambo yanayohusu uchaguzi na serikali au siasa kiujumla.
5. Ianzishwe fundraising programme ikiwezekana ili kuepuka hujuma kama ilivyotokea kwa ile programme ya simu
6. Tuwape mapendekezo kwa viongozi wa chama ili kuanzisha vyombo vya habari vya chama mfano magazeti badala ya kutegemea vyombo vya habari vya watu binafsi mapema kabla ya 2012.
7. Kuimarisha kurugenzi ya vijana (Baraza la vijana-Bavicha) ili kukabiliana na propaganda chafu (Simaanishi Green Guard). Hawa wawe spesho kwa ajili ya kukabiliana uhuni wa UVCCM hasa kuwapaka matope viongozi wa chadema.
8.Sisi wenye wana JF tuanze sasa kutangaza nia kwa ajili ya majimbo na kata zote hapa nchini huku tukiandaa fungu (capital) kwa ajili hiyo. Mimi natangaza nia katika jimbo mojawapo katika mkoa mpya wa Njombe baada ya vumbi la uchaguzi uliopita kuanza kutulia.

Naomba kuwasilisha

Walio na njaa hawawezi kuwa volunteers Chadema?

If that is the case, you are going no where with this proposal!
 
Aisee Hilo wazo ni kali mno, yaani wewe Mduda unakipaji kizuri, Mimi nawaunga mkono wote mlio changia, tuwe tunautaratibu wa kukutana ili tubadilishane mawazo, na tupeane mbinu na uzoefu wa kusimama majukwaaani, kwani 2015 vijana wengi watasimama jukwaa mbalimbali kupitia CHADEMA, hata mimi nitasima kuwania ubunge kupitia CHADEMA huko Mbarali, mbeya. Nimepata uzoefu kidogo kupitia kampeni za Sugu. Si kazi ndogo kuwaangusha mafisadi, Siasa ni kazi nzito, kunafitina na mambo mengi. Hili wazo ni zuri sana tusilipuuze hata kidogo
 
Ni wazo jema. Utekelezaji au evaluation yake iwe kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2014. Nitafurahi sana kama wazo hili litaungwa mkono ili by January 2015 kwa mfano mambo yafuatayo yafanyike (lakini kwa baraka za Chama hasa kupitia Bavicha)
1. Wagombea walau watatu wa nafasi za ubunge wawe wamejulikana kwa majimbo yote Bara na visiwani
2. Nguvu ya Chama iwe imeongezeka hasa maeneo ya mikoa kama vile Mtwara, Dodoma, Moro, Tanga, Lindi pamoja na Visiwani
3. Uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2014 tushinde kwa kiwango kisicho pungua asilimia 50.
4. Kila jimbo walau liwe limeanda volunteers wasiopungua 30 wasio na njaa na wenye uelewa wa mambo yanayohusu uchaguzi na serikali au siasa kiujumla.
5. Ianzishwe fundraising programme ikiwezekana ili kuepuka hujuma kama ilivyotokea kwa ile programme ya simu
6. Tuwape mapendekezo kwa viongozi wa chama ili kuanzisha vyombo vya habari vya chama mfano magazeti badala ya kutegemea vyombo vya habari vya watu binafsi mapema kabla ya 2012.
7. Kuimarisha kurugenzi ya vijana (Baraza la vijana-Bavicha) ili kukabiliana na propaganda chafu (Simaanishi Green Guard). Hawa wawe spesho kwa ajili ya kukabiliana uhuni wa UVCCM hasa kuwapaka matope viongozi wa chadema.
8.Sisi wenye wana JF tuanze sasa kutangaza nia kwa ajili ya majimbo na kata zote hapa nchini huku tukiandaa fungu (capital) kwa ajili hiyo. Mimi natangaza nia katika jimbo mojawapo katika mkoa mpya wa Njombe baada ya vumbi la uchaguzi uliopita kuanza kutulia.

Naomba kuwasilisha

Tuko pamoja mkuu,

Kwa msisitizo wa kipekee, chadema ianze mipango ya kuwa na vyombo vya habari hasa redio na television.

kuendelea kumtegemea tido au mzee mengi agundue dili ya cocaine dhidi ya mwanae ndipo awapatie airtime si mujalabu kabisa.
 
Naunga mkono! Ni wazo zuri sana WanaJF hasa litaimalisha nguvu na morali hasa kwa sisi vijana ambao tuna -emerge kwenye siasa na kutangaza nia. Binafsi natarajia kutangaza nia 2015 jimboni Buchosa, ninauhakika kama nikipata support kupitia baraza hili kazi itakuwa nyepesi na nitapata muda wa kutosha kujitangaza na kuanza propaganda ili wanajimbo wafahamu wasfu wangu na kuitangaza vizuri ilani ya chama chetu na pia kufahamu changamoto zinazowakabili wanajimbo. Hivyo mimi naunga mkono 100/100 wazo hili.
 
Walio na njaa hawawezi kuwa volunteers Chadema?

If that is the case, you are going no where with this proposal!

Hili nalo linataka uelewa kiasi gani kujua kwamba walengwa hapa ni wale wanaojiunga na vyama kwa ajili ya kupata kitu fulani cha haraka. kama huja experience unaweza ukadhani mzaha lakin sisi wengine huko vijiji ukitaja chama unaambiwa ugawe walau 500/=. Kumbuka nazungumzia volunteers sio wanachama. Kama sijaeleweka sidhani kama naweza kufafanua zaidi hapa. Hata hivyo nakushukuru kwa kuwa umenielewa hayo maeneo mengine. Tupo pamoja
 
Back
Top Bottom