Kuumwa tumbo

Lady

JF-Expert Member
Apr 12, 2010
282
61
Habari wadau.

Naomba mnisaidie nina tatizo la kuumwa tumbo kila wakati ninapoanza tu kula chochote linauma baada ya muda linatulia, tumbo linanifanya nakosa hata hamu ya kula, sababu iwe ni mchana nikimeza tu mara ya kwanza tumbo linaanza kuuma, usiku pia hivyo hivyo.
 
Pole sana ingawa hujatueleza wewe una umri gani? Umeshaolewa? Umeshazaa? inaonyesha una chango la uzazi wewe jaribu kwenda Hospitali kumuona Daktari ataweza kukupa dawa ili matatizo yako yaweze kumalizika. Au jaribu kutumia Dawa hii kama utaweza kupata Asali mbichi safi

ambayo inayotoka Mtini haijapikwa au kuchanganywa na kitu kila tumbo linavyo kuuma uwe unakunywa hiyo Asali kijiko kimoja kikubwa cha kulia wali jaribu kutumia hiyo Asali itakusaidia kuondosha hayo matatizo yako. au uwe unakunywa hiyo Asali kila siku Asubuhi kabla ya kula kitu

Asali kijiko kimoja na wakati wa usiku ukimaliza kula au wakati wa kwenda kulala unywe Asali kijiko kimoja kila siku kwa muda wa siku 40. Kazi yake hiyo Asali inasaidia kusafisha ini na figo kwenye Mwili wako jaribu utaniambia nini kinachoendelea katika mwili wako asante.
 
Vidonda vya tumbo au una shinda au kukaa na njaa muda mrefu bila kula, jifunze kula ontime na maji mengi au juice fresh, sio za kijoti
 
Thanks kwa ushauri, ntajitahidi kutafuta asali na pia kula on time,
By the way kwa hapa dar ni wapi naweza kupata asali mbichi original?
 
Pole sana ingawa hujatueleza wewe una umri gani? Umeshaolewa? Umeshazaa? inaonyesha una chango la uzazi wewe jaribu kwenda Hospitali kumuona Daktari ataweza kukupa dawa ili matatizo yako yaweze kumalizika. Au jaribu kutumia Dawa hii kama utaweza kupata Asali mbichi safi

ambayo inayotoka Mtini haijapikwa au kuchanganywa na kitu kila tumbo linavyo kuuma uwe unakunywa hiyo Asali kijiko kimoja kikubwa cha kulia wali jaribu kutumia hiyo Asali itakusaidia kuondosha hayo matatizo yako. au uwe unakunywa hiyo Asali kila siku Asubuhi kabla ya kula kitu

Asali kijiko kimoja na wakati wa usiku ukimaliza kula au wakati wa kwenda kulala unywe Asali kijiko kimoja kila siku kwa muda wa siku 40. Kazi yake hiyo Asali inasaidia kusafisha ini na figo kwenye Mwili wako jaribu utaniambia nini kinachoendelea katika mwili wako asante.

tehe tehe hapo kwenye redi mzizi umenifurahisha siku nyingine tutasema kijiko kimoja cha kulia kande.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom