Kuuliza upewe fursa, sio kufanikiwa ukipewa fursa!

Maisha001

Member
Nov 13, 2019
77
42
Salaam Wanajukwaa,

Nimekuwa nikiwasikia na wakati mwingine kuwaona baadhi ya watu wakiwa na mipango ya kuhamia maeneo fulani kiutafutaji na hivyo kuuliza wenyeji kuhusiana na fursa wanazoweza kuzipata huko!

Kwa upande wangu najaribu kujiuliza usahihi na msaada anaoweza kuupata mtu huyo kwa swali hilo.

Kwa bahati nzuri wanaJF niwaungwana kabisa na kila mtu atafunguka kulingana:

- Alichofanya/anachofanya yeye na kufanikiwa.

- Anachoona wengine wanafanya na kufanikiwa.

- Alichosikia/kuambiwa kuwa inalipa ukifanya.

Kwa uaminifu kabisa mtu atatiririka hapa na kufafanua akikutakia mema kabisa ili na wewe ukifanya ufanikiwe!

Lakini wasiwasi wangu unaibuka ninapojiuliza yafuatayo:

> Ni kweli uliyopewa ni fursa. Je, kwako yaweza kuwa fursa kweli?

> Je, nawe utafanikiwa kama aliyeona hiyo fursa alivyofanikiwa?

> Je, utakapoona mambo hayaendi kulingana na matazamio uliyokuwa nayo utakaza kama alivyokaza yeye aliyeona hiyo fursa?

> Je, ni kweli ni kuwa tayari fursa hiyo imeota mizizi moyoni mwako kiasi cha kuipenda kweli kweli?

Maswali haya na mengine yaweza kuleta wasiwasi juu ya jinsi gani unaweza kutumia majibu unayoweza kupokea kutoka kwa watu wenye moyo wa dhati kutaka ufanikiwe kwa kukuonyesha fursa.

Binafsi ninaamini:

- Mgunduzi wa kwanza wa FURSA ni wewe na sio mtu mwingine.

- Huwezi kupewa fursa na mtu mwingine na ukaitumia na kufanikiwa bila kuifanya kuwa ni fursa yako.

- Kila akupaye fursa ni kwa mtazamo wake na siyo wako.

- Kuna jambo laweza kuwa fursa kwa mtu mwingine ila kwako isiwe fursa kabisa

Na hivyo:

- Si mara zote ni rahisi kutumia fursa aloiona mtu mwingine na kufanikiwa ( japo inawezekana pindi utakapoifanya kuwa ni yako pia)

- Kuifanya fursa ya mwingine kuwa yako si lelemama yahitaji sacrifice (Japo si mara zote unaweza kusacrifice na kufanikiwa)

- Fursa makini ni pale uonapo tatizo/changamoto fulani na ukadhamiria kuifanya fursa. Ukweli ni kwamba fursa hii huwa haichuji hata kama utaspend miaka kuisimamisha ikisimama ni mwendo mdundo!

Kutamani fursa iliyomtoa mtu mwingine waweza fanikiwa(Japo ni nadra sana) ila mara nyingi na walio wengi humu wamesuffer sana na hata kupoteza mitaji Kwa kuwa walitamani na kuingia kisha wakalia baadaye.

Lakini, ikitokea ukaitamani fursa fulani basi tia nia kweli kweli, jizuie kutoona fursa nyingine (maana ukiangalia kwingine tu umefeli), hangaika usiku na mchana unaweza kupata mafanikio kiasi fulani japo si kama aloiona ama aliyefanikiwa kupitia fursa hiyo!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom