Kuuliza si ujinga

kachumbari

Senior Member
Nov 1, 2010
125
8
Mimi nina binti kaolewa na ana watoto 2 na wanakaa kwao kwenye nyumba ya yeye na mumewe,mama yuko mko mwingine na wao wako Mkoani lakini anamlalamika mama mkwe wake kila akienda kuwatembelea kwao,anajishughulisha sana,lakini kinachomkera huyu binti yangu ni kwamba imefikia mahali,binti akiwa amekwenda shule(chuoni) yeye anampeleka mtoto wake maji ya kuoga chumbani,anatandika kitanda na imefikia mpaka ana mfulia chupi huyu mume wa mwanangu(Mwanae),hata siku akiwa nyumbani wakipikwa kuku basi atahakikisha kwanza mwanae ndio anapata sehemu za kuku nzuri kuliko wajukuu zake na hizi taarifa anaambiwa na msaidizi wake hapo nyumbani hii inamaanisha nini?Nifanyeje kumsaidia Binti huyu?
 
Mimi nina binti kaolewa na ana watoto 2,lakini anamlalamika mama mkwe wake kila akienda kwao,anajishughulisha sana,lakini kinachomkera huyu binti yangu ni kwamba imefikia mahali,binti akiwa amekwenda shule(chuoni) yeye anampeleka mtoto wake maji ya kuoga chumbani,anatandika kitanda na imefikia mpaka ana mfulia chupi huyu mume wa mwanangu(Mwanae),hata siku akiwa nyumbani wakipikwa kuku basi atahakikisha kwanza mwanae ndio anapata sehemu za kuku nzuri kuliko wajukuu zake na hizi taarifa anaambiwa na msaidizi wake hapo nyumbani hii inamaanisha nini?Nifanyeje kumsaidia Binti huyu?


mawili either waache tabia ya kung'ang'ania kukaa nyumbani kwao(kwa mama mkwe)waende kupanga kama vip au mwambie yeye ajishughulishe na hizo kazi anazofanya huyo mama mkwe,..ila kwa upande wangu sijaona ubaya kwani mtoto hakui kwa mama yake
 
Tumebarikiwa watoto itafika mahali lazima tukubali majukumu mengine yatatoka mikononi mwetu ......... tuwape uhuru wale waliopenda kuongeza familia zetu kuyafurahia matunda tuliyotengeneza ....................huku ni kuingilia mipaka ya familia za watoto wetu
 
Pagumu! Japo mtoto hakui kwa mamake, ths is too much. Kama kuna msaidiz kwa nini asifanye hizo kaz yeye? Mapenzi gn haya? Yamepitiliza.
 
Ww unahisi hao wawili (mama na mwanae) wana-date? Suluhisho huo mama kwanini akae hapo? Fukuzia mbali.......
 
Dah!!! Kuna kusaidia ila hii too much hadi kufuliana nguo za ndani nah nah hii siyo kabisa hata kama ni upendo banaa not this way inavuka mipaka hii
 
inaelekea mwanao hatimizi wajibu wake kama, acha asaidiwe/afanyiwe.

N.B hakuna ambapo mwanao analalamika kuwa hata akifanya hizo shughuli mama mkwe anamkataza!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom