Kuuliza si ujinga, ile tuzo aliyopewa Waziri Mkuu ilitokana na nini?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,599
217,991
Waziri Mkuu wa Tanzania Mh Kasimu Majaliwa ni miongoni mwa wadau walioambulia Tuzo kutokana na mchango wao kwenye maendeleo ya soka la Tanzania , tunashukuru sana kwa waliompa tuzo hiyo kwa kutambua mchango wake ambao sisi wengine hatujawahi kuuona.

Bali sisi watu wa soka tunataka kujua ni kipi alichokifanya kwenye soka Mh Majaliwa ambacho kimesababisha apewe tuzo hiyo?

Naomba kuwasilisha
 
Tuzo ya Karia ile ya kujikomba komba kwa ccm wenzake ili wasimsahau kwenye uteuzi baada tu ya kutuachia TFF yetu, miaka michache ijayo.
 
Waziri mkuu ndiye alimsaidia kitumbo mwenyekiti fake wa tff kushindana uchaguzi uliopita

Hayo ndio maajabu ya mpira wa bongo
 
Mtoa uzi kwanza upimwe akili!
Yote haya alioyafanya Majaliwa kwenye Michezo unapata wapi Nguvu ya Kuhoji Tuzo aliyopewa?
Achana na hizo harambee alizokuwa akizifanya kwenye timu yetu ya Taifa au Kama hiyo haitoshi waulize Yanga amewasaidia Nini?
 
Shida hapo ni hiko cheo cha Uwaziri Mkuu...watu wanashindwa kufanyakazi za Maendeleo wanatengeneza majungu kila kukicha
 
Na hili naliona watu wanaChuki binafsi na Wala sio Utendaji kazi wa Majaliwa wanaumia Sana na cheo Cha Uwaziri Mkuu ..
Tukisema tulete na Kuyachambua aliyoyafanya Majaliwa atutamaliza Leo Ila Mimi binafsi sitomsahau Majaliwa kwenye lile la kukaa siku nzima na Wamachinga kujadili nao kwa kweli Mimi Bado lipo kichwani kwangu
Huyu Ni kiongozi wa mfano kwangu
 
Back
Top Bottom