Kuuliza napo ambapo hujaelewa sio Ujinga?

Mkogoti

TAPELI Mkubwa
May 3, 2020
2,416
3,911
Bwana John Okello ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara mpya baada ya teuzi teuzi akachaguliwa na yeye kuwa mkuu wa mkoa, baada ya kama siku tatu akawa amesharipoti na kukabidhiwa ofisi na wa zamani aliekuwepo kuondoka

Bwana John akaomba siku inayofata aweze kwenda kutembelea baadhi ya wilaya, basi kesho yake Asubuhi akapewa ratiba kama ifuatavyo, kuanzia saa 8:30 Asubuhi mpaka saa 13:00 mchana atafanya Ziara yake na kapanya baada ya hapo ataenda kula chakula cha mchana Nanguruwe

Kutakuwa na mapumziko kidogo mpaka saa 16:00 alasiri atamalizia Kizimbani. Bwana John Okello kusikia ratiba hiyo alihamaki na kuuliza yani ratiba yangu nifanye na kapanya pia haitoshi nikale pia Nanguruwe. Alipanick sana lakini baada ya kumtuliza Alielezwa hiyo ni baadhi ya wilaya za Mkoa wa Mtwara.

Kuuliza si Ujinga ukiona kuna kitu hakipo sawa uliza tu ata ukionekana mjinga lakini umeshakielewa tu Mimi niwatakie Usiku mwema wote 🙏🙏
 
Back
Top Bottom