Kuulinda Mhimili wa Bunge: Na sisi tunaweza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuulinda Mhimili wa Bunge: Na sisi tunaweza!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 25, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 25, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Na. M. M. Mwanakijiji

  KATIKA makala yangu ya wiki mbili zilizopita nilielezea jinsi wabunge wetu wanavyolindwa au kuhakikishiwa usalama wao kwa namna inavyowezekana kibinadamu.

  Nilitoa mifano kadhaa inayoonyesha kwamba hatuna utaratibu mzuri wa ulinzi wa wabunge wetu na bunge letu; hivyo kulazimika kupata gharama kubwa zisizo za lazima kama taifa. Tumenusurika na mara nyingine kulazimika kulipia gharama kubwa zaidi.

  Niliahidi wiki iliyopita kuwa ningelikuja na mapendekezo yangu ya jinsi ya kupunguza na hatimaye kuondoa vitu ambavyo huko nyuma vilitusababishia kupoteza maisha ya wabunge na hata kutishia usalama wa bunge lenyewe.

  Msingi wa mapendekezo yangu unatokana na kanuni zifuatazo: kwanza kabisa, ni gharama kubwa ya kufanya chaguzi ndogo za marudio kuliko kuja na mfumo mzuri wa ulinzi wa wabunge. Tuko tayari kurudia uchaguzi mdogo kwa gharama kubwa kuliko kuajiri madereva wa kudumu wa wabunge na kuwaweka katika malipo ya serikali. Nitalieleza hili zaidi baadaye.

  Kanuni ya pili ni kuwa katika ulimwengu tunaoishi sasa Bunge letu limeanza kupata uhai linaostahili na kuanza kuuma; itakuwa ni kutokuwajibika kuendelea kuishi kama zamani Bunge letu lilipokuwa ‘bendera fuata upepo'.

  Kwa kadiri Bunge letu linavyozidi kutunisha misuli yake mbele ya taasisi nyingine na kwa kadiri wabunge wetu wanavyozidi kuthubutu kuwa wawakilishi wetu wa kweli ndivyo ambavyo maisha yao na mali zao zinavyozidi kuwa hatarini!

  Hivyo, kuwalinda wabunge na Bunge lenyewe ni kwa maslahi yetu sisi wenyewe wananchi kwa ujumla wake. Tunacholinda siyo wao kama watu tu bali wao kama raslimali yetu ambayo tumewekeza kwa kupiga kura. Tunalinda kura zetu kwa miaka mitano!

  Kanuni ya tatu na kubwa ni kuwa tayari tunawalinda watumishi wa juu wa mihimili mingine ya dola: Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu, Majaji wa Mahakama ya Rufaa, Majaji wa Mahakama Kuu n.k. Zaidi ya yote viongozi wa juu wa vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama nao wanalindwa: CDF, Mkuu wa Usalama wa Taifa, IGP, DCI, Makamanda wa Polisi Mikoa na Magereza. Na karibu wote hawa licha ya kuwalinda tumewapatia pia madereva wa kudumu na vikolombwezo vingine.

  Kanuni ya mwisho na kubwa pia inatokana hiyo ya tatu. Wabunge ndiyo watunga sheria wa nchi hii na ni wao ambao wamepewa jukumu la kuisimamia serikali. Ni wao kimsingi kabisa wanaosimama kati ya utawala wa kidikteta na utawala wa demokrasia; ni wao ambao ni ngao ya uhuru wetu na ni pekee wanaosimama kama watetezi wa mwisho dhidi ya udhalimu. Kutowalinda hawa ni sawa na kuchezea shilingi ******; na ni sawa na kuweka rehani hatima ya taifa letu. Kuwalinda wabunge na kulilinda bunge ni jambo la msingi, la lazima na kwa hakika ni la kizalendo. Kutofanya hivyo ni kuwa wepesi wa fikra, dhaifu wa maamuzi, na waoga wa kutenda. Kutofanya hivyo ni kuacha nasibu iwe hakimu wetu kila wakati.

  Tuwalindeje basi?

  Ninapozungumzia kuwalinda, sizungumzii kumpatia kila mbunge mlinzi, kulinda nyumba zao, ofisi zao au kuwalinda wakienda kwenye mashamba yao! Nazungumzia kutengeneza mfumo ambao utatusaidia kuleta ulinzi wa Bunge; mfumo utakaoondoa kutishiwa kwa maisha ya wabunge na bunge lenyewe. Hivyo, mapendekezo yangu yafuatayo yamegawanyika katika sehemu mbili: kulilinda Bunge kama mhimili wa dola na pili kuwalinda wabunge kama wawakilishi wa wananchi.

  Kulilinda Bunge na Spika

  Ipo haja ya kulinda Bunge na Spika kutoka kuingiliwa na chombo kingine chochote na kuhakikisha usalama wake. Ili demokrasia yetu ifanikiwe na ikomae ni lazima Bunge lisiwe katika hali ya kuhofu chombo kingine cha serikali kuhusu usalama wake au usalama wa wajumbe wake wa kwanza kati yao akiwa ni Spika na Naibu wake.

  Katika hili napendekeza kuanzishwa kwa kikosi maalum cha Ulinzi na Usalama wa Bunge (Parliamentary Security and Protection Unit). Kikosi hiki kitakula kiapo maalum cha kulinda Bunge na Spika na kutoa usalama kwa wabunge kama nitakavyofafanua hapa chini.

  Kikosi hiki kinaweza kuwa na maafisa wasiozidi 200 ambao watatoka katika jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa na JWTZ au kwa namna yoyote ambayo itapendekezwa. Bila kujali wanakotoka pindi wakishakula kiapo cha kulilinda Bunge watumishi hao watakoma kuwa watumishi wa majeshi au taasisi zao na hivyo mishahara, mafao, n.k vyote vitakuwa chini ya Spika.

  * Kiapo cha kikosi hiki kitahusu kuhakikisha usalama na Uhuru wa Bunge.

  * Jukumu la kikosi hicho kwanza ni kutoa ulinzi binafsi wa Spika na Naibu wake kuanzia kazini na nyumbani na mahali popote ambapo Spika au Naibu wake anakuwepo.

  * Kuweka ulinzi wa eneo zima la Bunge na kuhakikisha usalama wa jengo hilo na kila mgeni anayefika hapo. Polisi na maafisa wengine wote wanapofika Jengo la Bunge wanasalimisha silaha zao na nguvu zao zinaishia kwenye mipaka ya Bunge. Usalama wote wa Bunge uko chini ya kikosi hicho maalum.

  * Kuhakikisha wanatoa ushauri wa kiusalama kwa mbunge yeyote na kutoa ulinzi wakati wowote wanapoelekezwa na Spika. Kwa maneno mengine, mbunge akikosa dereva wake wa kawaida ni jukumu la kikosi hiki kuhakikisha linampatia mbunge huyo dereva anayejulikana kwa taratibu watakazokuwa wamejiwekea. Lengo hapa ni kuondoa kabisa uwezekano wa mbunge yeyote kuwa chini ya udereva wa mtu yeyote yule.

  * Watasimamia uchunguzi wa jambo lolote lenye kutishia usalama wa Bunge, au mbunge yeyote yule.

  Madereva wote wa wabunge wawe katika ajira ya serikali


  kati ya vitu vinavyoshangaza sana ni kuwa hadi hivi sasa wabunge wanapewa fedha za kuwalipa madereva wao lakini madereva hawa hawajaajiriwa na serikali. Jambo hili kwa kweli ni upungufu mkubwa sana wa maono. Ukifikiria gharama ya uchaguzi mdogo mmoja tu kama ule wa Tarime na gharama ya kuajiri madereva kwa wabunge wote utaona kuwa ni rahisi zaidi kuajiri madereva kwa miaka mitano kuliko kurudia chaguzi angalau moja kila mwaka kufuatia kifo au ajali inayomfanya mtu ashindwe kuendelea na ubunge wake.

  Kwa ajili ya mjadala wetu hapa tufikirie kuwa uchaguzi mdogo unagharimu karibu shilingi 2,000,000,000 (hii ni gharama tu ya maandalizi, kampeni na uchaguzi wenyewe), ukizichukua hizo na kugawa kwa wabunge 325 kila mbunge anapata shilingi milioni 6,153,846 kama kila mbunge anamuajiri dereva mmoja kwa mwezi anaweza kumlipa ni laki 512, 820 kiasi ambacho ni kikubwa ukilinganisha na kima cha chini.

  Sasa kama tunaweza kuwa na kiasi hicho kwa nini tusiingize fedha hizo kwenye bajeti y a kawaida ya Bunge ambapo madereva wa wabunge watakuwa chini yake na hivyo kuwa waajiriwa wa Bunge? Kwa kufanya hivyo tutaongeza ajira, tutakuwa na utaratibu mzuri na madereva hawa watakuwa wanafanya kazi katika maadili yanayosimamiwa vizuri kuliko jinsi ilivyo sasa. Zaidi ya yote kutakuwa na rekodi nzuri ya madereva na kwa kadiri muda unavyoenda tutakuwa na madereva wazoefu katika shughuli za wabunge kuliko ilivyo sasa. Uchaguzi mpya unapokuja, na wabunge wapya wanapoingia hakutakuwa na haja ya mbunge kuanza kutafuta madereva kwani tayari wapo.

  Hii itakuwa ni sawasawa na ilivyo kwenye taasisi au mashirika mengine ya serikali ambapo kuna madereva ambao hawajali ni nani bosi wao bali wako tayari wakati wote kufanya kazi yao chini ya yeyote atakayekuwa bosi wao kwani wao si waajiriwa wa mtu bali wa taasisi. Unapokuwa na madereva rasmi na wenye mkataba wa serikali utaona kuwa linapotokea janga au jambo ambalo likawasababishia ulemavu au au hata kifo basi madereva hao na familia zao watakuwa kwenye utaratibu wa kupata matibabu au mafao ya aina fulani kuliko ilivyo sasa ambapo dereva wa mbunge akifia kazini sijui zaidi ya rambirambi ana haki gani nyingine.

  Hili hata hivyo ni jambo ambalo ni wabunge wenyewe wanaweza kuamua kulitungia sheria badala ya kusubiri kuipigia magoti serikali. Mambo yote niliyoyapendekeza hapa na mengine ambayo yapo mbeleni utaona kuwa yanawezekana kufanywa na kuletwa Bungeni na wabunge wenyewe.

  Jambo moja ambalo hatuna budi kulikataa ni kuambiwa kuwa "serikali haina fedha". Mbunge atakayekubali kusikia kuwa ati serikali "haina fedha kwa wakati huu" kuhusu mabadiliko haya mbunge huyo itabidi tumtimue Bungeni. Tuna kiasi cha kutosha cha fedha na wakati umefika kuanza kuweka vipaumbele vyetu sawasawa.

  Mwisho
  Mapendekezo haya kwa watu wengine yanaweza kuonekana ni mageni. Hata hivyo nchi kadhaa duniani zina utaratibu kama nilioupendekeza hapo. Miongoni mwao ni Marekani ambayo ina kikosi kama nilichofafanua hapa. Tunaweza kama tukitaka na sisi kuulinda mhimili huu wa serikali jinsi ambavyo tunalinda mihimili mingine. Na hilo litawezekana kwa kuunda kikosi maalum cha Ulinzi wa Bunge na Wabunge.

  Ni mpaka pale tutakapoweza kuhakikisha kuwa bunge letu liko salama na ulinzi wake umeahidiwa ndipo hapo kweli Bunge letu litakuwa huru kweli na wabunge wetu kutokuwa katika huruma ya serikali au taasisi nyingine. Bunge letu haliwezi kuwa salama na huru kwa kadiri ya kwamba linategemea taasisi nyingine za mhimili wa dola kupata ulinzi wake. Bunge lijilinde lenyewe, kwani siku moja litapitia majaribio ya kuona uhuru wake unakoma wapi.

  mwanakijiji-at jamiiforums.com
   
  Last edited: Feb 25, 2009
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Umesema kweli Mwanakijiji, nitazungumzia machache

  MADEREVA
  Serikali nadhani inakwepa hili sababu ya kukwepa pia stahili zao wanapoajiriwa, manake ukimuajiri mtu kuna vitu anastahili kupata ambavyo kama hujamuajiri hapati. Lakini kama hili ndio wanaogopa, wangeajiriwa kwa mikataba kama wafanyavyo kwa madereva wa miradi (projects) mbalimbali.
  Wabunge nao kwa hili wanachemka mno, ila tatizo lililokuwepo ni kwamba hawawezi kulipigania hili wakati wengi wao huajiri ndugu zao. Hii hali ya kupewa wao uwezo wa kuajiri imepelekea hizi nafasi wawape ndugu, jamaa ama rafiki zao. Ingekuwa hili linafanyika katika mashirika ungesikia kelele zao, ila kwa kuwa linawahusu, na wao ndio watunga sheria wako kimya kabisa.

  ULINZI
  Hili la ulinzi ni zuri, lakini sidhani kwa bunge kuwa huru linahitaji sana hiki kikosi. Tuna vikosi vingi tu vya ulinzi, vinatakiwa vyote viwajibike katika kulinda raia, na si wabunge tu. Mfano chukulia mahakimu wanaohukumu watuhumiwa, hawa wako katika hatari kubwa ya kudhuriwa na wanaowahukumu, ndugu zao, walio na maslahi nao nk. Pia hata watu kama wale walio katika ile kamisheni ya ushindani (sijui kama napatia jina kwa kiswahili, Fair Competition Commission-FCC), hawa huenda kwa waagiza bidhaa na madukani, na wakikuta ni za kubumba (counterfeit) huziharibu, hivyo nao wana maadui kibao tu sababu ya kazi zao. Hivyo kila unapokuwa unatekeleza jukumu fulani, unaweza kuwa unajijengea maadui. Kwa mawazo yangu, vikosi vyetu vyote vya ulinzi vinatakiwa kulinda raia wote kuanzia wabunge, mahakimu, madaktari, waalimu, wakulima, wafanyabiashara nk.

  Ulinzi madhubuti utatokana na KATIBA, kama tutaweza kuiandika katiba yetu upya, haina haja kwa Dr. Slaa, Dr. Taarabu nk kuogopa kuchangia. Vile vile wale wa CCM ambao wanaogopa kuchangia kwa kulinda maslahi ya Chama na yao wenyewe kwamba wakiikosoa CCM wanaweza kutopitishwa kugombea miaka inayokuja. Katiba ikiweka kuwa wagombea huru wanaruhusiwa, wabunge hata wa CCM watakuwa huru zaidi kuchangia, wakijua kama watatemwa kugombea na chama, basi watagomea kama wagombea huru. Hivo muhimu kwa Bunge letu kuwa huru ni kuwa na KATIBA ambayo ni ya kidemokrasia zaidi kuliko hii tuliyorithi iliyo na viraka kibao.
   
Loading...