Kuugua Mwakyembe wazee wa Kyela waja juu

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,835
2,792
Kuugua Dk. Mwakyembe: Wazee waja juu...!

2008-06-17 14:57:25
Na Thobias Mwanakatwe, PST - Kyela

Siku chache tu baada ya Mbunge wa Jimbo la Kyela, Mhe. Dk. Harrison Mwakyembe kuugua ghafla wakati akiwa bungeni na kukimbiziwa kwenye zahanati ya ukumbi huo mjini Dodoma, limeibuka jopo la wazee mbalimbali maarufu mjini Kyela lililokuja juu na kudai kuwa kuumwa kwa mbunge wao huyo si bure na kwamba sasa wanajipanga katika kuhakikisha kuwa hadhuriwi na mambo ya kiuchawi.

Na kwa kuanzia, wazee hao wamesema tayari wameshaunda kamati ya wenzao kumi, ambao wamepiga kambi katika Kijiji cha Nduka kilichopo wilayani Kyela kwa ajili ya kupeana mbinu kali za kiulinzi kabla ya kufunga safari ya kuelekea Dodoma, ili hatimaye wakaonanane na mbunge wao huyo kipenzi na kumueleza kusudio lao la kumpa ulinzi kijadi.

Wakizungumza na PST mjini Kyela, wazee hao waliokataa kuandikwa majina yao gazetini kwa sababu walizodai kuwa ni za \'kiufundi\', wamesema kamati yao hiyo ya wazee kumi mahiri wa mambo ya kijadi, itaanza kwa kufuatilia kiundani ili kujihakikishia kile wanachoamini kuwa kweli, kuugua ghafla kwa mbunge wao huyo ndani ya Ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumetokana na kulogwa.

``Baada ya hapo, kama itabainika kuwa ugonjwa uliompata (Dk. Mwakyembe) umetokana na mikono ya watu wanaokwazika na kazi yake ya kututetea sisi na Watanzania wengine, kitakachofuata ni kumganga na kisha kumtengenezea ulinzi imara ili asidhuriwe tena,`` akasema mmoja wa wazee hao.

Wakasema wamepata wasiwasi mkubwa juu ya kuugua ghafla kwa mbunge wao huyo, hasa baada ya kusikia habari za kuwepo kwa hofu ya vitendo vya kishirikina kufanyika ndani ya Jengo la Bunge.

``Tunajua kuwa siku zote Serikali haiamini mambo haya... na hata mheshimiwa si mfuasi wa mambo haya. Lakini yeye ni mtu wetu muhimu sana. Tukigundua kuwa alichezewa, sisi tutamlinda kwa namna tunayoijua hata kama mwenyewe akikataa,`` mzee mwingine akaongeza.

Alasiri ilipojaribu kuwasiliana na Dk. Mwakyembe ili kupata maoni yake kuhusiana na kikosi cha wazee hao kinachodai kutaka kumpa ulinzi maalum, hakuweza kupatikana kwenye simu yake ya mkononi.

Hata hivyo, kuna taarifa kuwa sasa Dk. Mwakyembe yuko buheri wa afya na jana alirejea tena Bungeni kwa ajili ya kuungana na wenzie katika kuijadili bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha wa 2008/09.

Dk. Mwakyembe amejijengea heshima kubwa baada ya Kamati yake iliyotumwa na Bunge kufuatilia mkataba tata baina ya Serikali na Kampuni ya Kuzalisha Umeme ya Richmond kuibua udhaifu mwingi, ambao mwishowe ulimfanya Waziri Mkuu Edward Lowassa na mawaziri wengine watatu kujiuzulu.

Aidha, umahiri wake ulimfanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bwana Jakaya Kikwete amteue kuwa mmoja wa wajumbe waliounda Tume ya Jaji Bomani iliyopitia mikataba ya Madini na kuwasilisha mapendekezo yake (kwa Rais) hivi karibuni.

http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2008/06/17/116675.html

SOURCE: Alasiri
 
Wababaishaji tu na hawana kitu. Kama wana uwezo huo si wangezuia yasitokee kabisa?

Nchi imejaa wasanii wengi sana.
 
Hao matapeli wanataka kuingiza mtu mkenge ,sasa kuna hatari ya nchi kuingia katika dimbwi jengine ,lakini bora wazee wajadi wawaekee kinga vijana wao wanaoingia katika mambu ya serikali na kwenye ubunge ,kama wale wa wazee wa pemba ambao wamemjenga Maalim Seif na kumfunga vibaya sana kiasi wanaomsogelea kwa kumzuru huanza kuzungumza luga isiyoeleweka kabla hawajamfika huku wakitetemeka miguu na mikono.
 
Wababaishaji tu na hawana kitu. Kama wana uwezo huo si wangezuia yasitokee kabisa?

Nchi imejaa wasanii wengi sana.

Ulaji mwingine. Kwanza nauli, posho na vijisenti vitachangwa na wakulima wa mpunga wa Kyela kuwapa hao wazee ambao naamini ndio wajanja wa huko wanaokula kiulaini bila kulima kama wenzao. Pili Mwakyembe hata kama haamini hana ubavu wa kuwakataza ama kuwazuia maana yamewahi kuwatokea wabunge wengi, ambao wanaogopa sana wapiga kura ama wapambe wao kiasi kwamba hata kama wanafanya mambo ya ovyo wanalazimika kuwavumilia na hivyo wakimtembelea Dar ama Dodoma, naye atatoa vijisenti. Nakwambia kufa kufaana
 
Hao matapeli wanataka kuingiza mtu mkenge ,sasa kuna hatari ya nchi kuingia katika dimbwi jengine ,lakini bora wazee wajadi wawaekee kinga vijana wao wanaoingia katika mambu ya serikali na kwenye ubunge ,kama wale wa wazee wa pemba ambao wamemjenga Maalim Seif na kumfunga vibaya sana kiasi wanaomsogelea kwa kumzuru huanza kuzungumza luga isiyoeleweka kabla hawajamfika huku wakitetemeka miguu na mikono.
__________________

Sielewi.... matapeli wa Kyela lakini wa Pemba ndio .......!!!!!!!!!!
 
si wamloge Sinclair na Andrew Young kwanza.... halafu wakimaliza wawaloge wote waliokwapua fedha zetu Benki Kuu ili wachanganyikiwe na kuamua kujitaja wenyewe pale MAELEZO?
 
si wamloge Sinclair na Andrew Young kwanza.... halafu wakimaliza wawaloge wote waliokwapua fedha zetu Benki Kuu ili wachanganyikiwe na kuamua kujitaja wenyewe pale MAELEZO?

Watamlogaje Young na Sinclair wakati wako upande wa pili wa bahari?
 
Watamlogaje Young na Sinclair wakati wako upande wa pili wa bahari?
Ha ha...mkuu hii kali...lakini Sinclair mara kwa mara si yuko Tanzania na Andrew Young alikuwa Arusha siku chache zilizopita.
 
Quote:
Originally Posted by Mzee Mwanakijiji View Post
si wamloge Sinclair na Andrew Young kwanza.... halafu wakimaliza wawaloge wote waliokwapua fedha zetu Benki Kuu ili wachanganyikiwe na kuamua kujitaja wenyewe pale MAELEZO?
Watamlogaje Young na Sinclair wakati wako upande wa pili wa bahari?
Reply With Quote

Imekaa vizuri lakini dalili za kukata tamaa. Yaani wao bora katika kila kitu. Bora kuiba, bora propaganda, bora kuloga, bora kutawala, bora..... ohoooo sasa tutawapisha na majumbani kwetu. HAIWEZEKANI hawana lolote wajinga wajinga hao.... SIKU ZAO ZINAHESABIKA
 
Jamani mambo ya jadi hayo msiyabeze!
Ulimwengu huu kila mwanasiasa anakazia.Si unaona barabara ya Bagamoyo imepigwa rami ili kuwarahisishia kwenda na kurudi faster kwa masangomaa.
Ndo maana siasa za Tz SIZIWEZI kabisa kama ni lazima ukazie.
Si mnakumbuka mtu mzima Jk alianguka wataalamu wakasema Tambiko lilikuwa hafifu!
Haya mabo yapo jamani!
 
Bonge la spin ya CCM......sijui wamempata wapi huyu spin doctor wao.......watu wako busy na uchawi....kama kawaida ya Tanzania watu wana nidhamu ya uoga=create fear...watu kimyaaaaaaaaa
 
Jamani mambo ya jadi hayo msiyabeze!
Ulimwengu huu kila mwanasiasa anakazia.Si unaona barabara ya Bagamoyo imepigwa rami ili kuwarahisishia kwenda na kurudi faster kwa masangomaa.
Ndo maana siasa za Tz SIZIWEZI kabisa kama ni lazima ukazie.
Si mnakumbuka mtu mzima Jk alianguka wataalamu wakasema Tambiko lilikuwa hafifu!
Haya mabo yapo jamani!

Ofcourse haya mambo binafsi siyaamini ila huwa nabaki kushangaa, watu wakubwa wenye heshima zao, shule kali sana unakuta sangoma hata shule hajaenda huwapelekesha wakamjengea nyumba nzuri, na lishe ya mji wa sangoma swaaafi! mpaka hapo huwa naona kihindi hindi tu, je ni kweli huwa anawafanikisha? ama ni basi tu coincidences?

Ila kwa Mwakyembe why this time?
 
kama anawaona pale bariadi VS kyela,baada ya hapo sijui itakuwaje maana kunatimu nyingine ya igunga nao bado wanapasha misuli yao moto tayari kwa pambano.
Sasa kila watu wakileta timu zao hapo bungeni sijui itakuwaje,mwenyezi mungu yapishie mbali,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom