Kuuelewa Mgogoro wa CHADEMA- Nyongeza ya Hitimisho

IsangulaKG

Verified Member
Oct 14, 2010
707
250
Ndugu yangu Mzee Mwanakijiji,

Kwanza nikupongeze kwa makala zako murua na napata faraja kuona watanzania ambao wanaweza kuandika mambo yaliyofanyiwa analysis ya kutosha badala ya kuwa washabiki wa ‘fulani kasema’. Mchango wangu fuatao nautoa kwa kuwa mimi ki-profeshenali ni Mtaalamu wa tafiti japo nimejikita sana katika masuala ya jamii na sera zenye mlengwa huo bali mbinu za tafiti za aina hii hushabihiana kwa kiasi fulani na ‘investigative journalism’ unayoifanya ambayo end point ni kujenga uelewa wa kutosha kwa jamii na kutoa mapendekezo yenye lengo la kuelimisha au kuchachusha mabadiliko ya kisera au mikakati.

Nimefuatilia makala zako zote kuhusu mgogoro wa Chadema na mahitimisho(conclusion) na mapendekezo (recommendations) zako ambazo ni za msingi sana. Labda kitu ambacho kimefanya recommedations zako ziwe na ‘linkage’ iliyopwaya kidogo (si sana) ukilinganisha na hoja zako za msingi katika makala zilizopita, ni kwamba mependekezo yote haya yatatatua ‘majani’ au ‘shina’ la tatizo na si mzizi wa tatizo iwapo Chadema wataamua kuya-implement kama yalivyo yaani wayachukue kama msaafu.

Nina sababu kadhaa;
Mosi, mapendekezo haya yanalenga kuimarisha mifumo ya kiutawala na nidhamu katika kazi. Labda nikukumbushe kwamba hata Mwalimu Nyerere katika misingi yake ya nchi kuendelea, WATU ni msingi muhimu wa kwanza huku uongozi bora na siasa safi ikiwa misingi inayofuata. Msingi mkuu hapa ni WATU. Watu hawa, mimi ninapofikiria hili, ni watu ambao wametoka katika misingi (Siyo mifumo) ya kimalezi iliyo bora, misingi iliyowajegea hulka ya kupenda kufanya mambo kiuadilifu na kusimamia mifumo (systems and structures) zilizowekwa na watu wenyewe.

Nidhamu kwa mtu yeyote ni matokeo ya fikra ambazo ni matokeo ya misingi ya kimalezi, makuzi na fursa (opportunities) za kukuza au kubadili fikra za mtu husika. Iwapo utazaliwa katika misingi mizuri ya kimalezi lakini ukakulia katika mazingira yenye misingi miovu utakuwa mwovu vile vile. Iwapo utazaliwa katika misingi myema na ukakulia katika misingi mizuri lakini ukawa exposed katika misingi miovu (opportunities za kuwa mwovu) kuna uwezekano mkubwa sana ukawa mwovu vile vile. Tatizo ni kwamba hapa nchini watu wengi hasa waluiozaliwa miaka ya nyuma walizaliwa katika misingi myema inayothamini utu na maadili. Lakini makuzi, fursa/ mazingira ambayo wamekulia na ambayo hata sisi tunakulia na wanetu wanakulia yanatu-exposed katika mambo mabaya na maovu , vivyo hivyo wengi wetu ambao mifumo ya kuhimili mshindo huu wa mabadiliko ya kifikra(resilience systems and structures) inashindwa kutusaidia kukabili mabadiliko haya huishia kuwa wabinafsi na wapenda maovu.

Nimeeleza hayo hapo juu kwa sababu mambo mengi uliyoeleza hasa yanayohusu ‘nidhamu’ na siasa za ‘kuviziana’ umeyaangalia kwa juu kiasi bila kuangalia mzizi wake (iceberg view). Siasa za kuviziana hazikuanza juzi, zilianza toka enzi za Adamu na hawa pale shetani alipo 'mvizia' hawa, hata Pontio Pilato 'alivyomvizia' Yesu (sina uhakika sana wa Kuran kwani sina uelewa nayo sana) na hata enzi za wakoloni, enzi za vita ya maji maji n.k na hata Mzee Mandela ni mfano tu kati ya mifano mingi. Wakoloni tena kwa kuwatumia waafrika wenzetu kama vibaraka wao ‘kuwavizia’ wapigania uhuru, Vivyo hivyo, hata baada ya ukoloni na kupata uhuru, bado viongozi wengi waliviziana…wajua visa vya akina Bibi Titi , Mzee Sokoine na wengine uliowatolea mfano ambao najua wewe una uelewa nao mkubwa zaidi yangu.
Siasa hizi haziko Chadema tu, zipo CCM toka katika michakato ya Urais na nafasi mbali mbali ndani ya Chama. Siasa hizi ziko NCCR toka enzi za akina Mabere Marando , Augustine Mrema hadi hii ya sasa ya Kafulila na Mheshimiwa mbunge. Siasa hizi ziko pia Ulaya kama unakumbuka issue ya Monica Lewinsick na Rais mstaafu. Zimeonekana pia miaka ya karibuni kama unakumbuka Obama alivyokuwa akizushiwa mambo mengi ya nyuma wakati wa kampeni za uchaguzi.

Wakati siasa hizi tunaziona za majitaka, kuna wakati ni ‘positive checks’ za maadili ya viongozi. Kiongozi mwenye busara akijua kuwa mambo ndiyo yako hivi na pana ‘watchful eye’ kwake ni lazima atakuwa muadilifu na kurudia yale makuzi ya wema aliyozaliwa nayo. Siasa hizi za majitaka zaweza kuwa ni msisimo wa mabadiliko ya kimaadili kwa viongozi ili wawe mfano wa kuigwa katika jamii na kuepuka kujenga taswira mbovu kwa jamii. Mtu awezaje kusema ni kiongozi mzuri iwapo hawezi kuiongoza tabia yake mwenyewe? Hawezi kuiongoza tamaa ya mwili na roho yake? Hawezi kuyaongoza maamuzi yake? Kwa upande wangu, bado naona siasa hizi za akina Mwigulu Nchemba zina nafasi pia katika kuweka sawa maadili ya viongozi.

Hata hivyo hakuna kizuri kisichokuwa na madhara au kibaya kisichokuwa na faida, siasa hizi pia zaweza kuharibu sifa na jina la mtu hasa kama ana nafasi katika jamii. Mimi Mlosi nikishikwa na mke wa mtu kisha nikamwomba mke wangu msamaha hutaona gazeti lolote likiandika maana sina nafasi kubwa katika jamii. Lakini Rais akifanya lolote ataandikwa na mbunge vivyo hivyo, hali hii yaleta fedheha kwa viongozi na familia zao, swali je ni vema tukaendelea kulea upuuzi huu na kukanywa kuusema ati kwa kuwa walioutenda watadhalilika kwa familia zao tukisema? Kama wao wakati wanafanya mambo hayo walidharau uwezekano wa fedheha kwa familia zao sisi ni nani hata tuione hiyo fedheha? Utamthamini vipi mtu ambaye yeye hajithamini na amekuonyesha wazi wazi kuwa hajithamini? Huku si kudhihirisha kuwa na sisi ni wale wale?

Mbili, nikirudi kwenye hoja ya msingi, hata kama tutaweka mifumo ya udhibiti wa fedha na nidhamu, ni vigumu kuwabadilisha watu wazima nidhamu yao, ama tutawafanya waishi kwa maigizo ya kinidhamu. Si vema mifumo ndiyo ikatumika kutengeneza nidhamu bali fikra za mtu ndizo zingetengeneze nidhamu yake. Fikra hizi hazijengwi kwa mifumo bali kwa misingi ya kimalezi na makuzi. Hujaona mtu mkarimu sana nyumbani kwake kwa maana ya customer care mtu huyo huyo ni mtu mwingine kabisa mahala pa kazi? Ni mkali na mkorofi? Je makazini hakuna mifumo ya kuelekeza jinsi ya kuhudumia wateja? Tena panapo hizo code of conducts kibao lakini huduma ni mbovu na nyumbani pasipo na hayo maandiko ya code of conduct mtu huyo huyo ni mkarimu sana. Hapa ndiyo tunaona tofauti ya misingi na mifumo. Nyumbani mtu huwa mkarimu kwa kuwa misingi ya ukarimu wa kifamilia, ndoa na mahusiano kwa ngazi ya nyumbani imejengwa na kuambukizwa kwa vizazi na vizavi kwa utaratibu maalumu wa malezi na makuzi ya kijamii na huchukua muda mrefu sana. Na mifumo ya kazini imeundwa kumfanya mtu aifuate ili kudhibiti mwenendo wake. Njia nzuri ingekuwa kujenga misingi na fikra za kifamilia makazini na hapo ndiyo tuna changamoto. Bado tuna nafasi ya kuanzisha misingi ya kimalezi katika vyama vyetu ili kuwalea viongozi wetu na situ kuweka mifumo ya kudhibiti nidhamu yao. Ni lazima tuwe na misingi ya kuwafundisha baya na jema katika uongozi ili wakikengeuka sasa tutumie mifumo ya kinidhamu kuwadhibiti.

Tatu, tunahitaji viongozi wasiokuwa na fikra za tamaa. Mwaka fulani nikiwa chuoni niliweza kuanzisha kaasasi kangu kwa hustle nyingi mno huku nikiwekeza Boom langu lote kuhakikisha kanafanikiwa na baada ya miezi kadhaa mambo yakawa mazuri. Asasi ikawa na akaunti ya benki na fedha ikaanza kuflow. Hali hii haikushindwa kuwavuta watu wenye tamaa ya fedha kwa mgongo wa uongozi. Na baada ya mwaka mmoja nikaenguliwa na katiba niliyoitunga mwenyewe lakini ilinilazimu kusimamia misingi ya utawala bora japo nilizijua nia za vijana hao lakini wanachama ambao ndiyo waamuzi hawakuwa katika mood ya kuliona hilo au kusikia tofauti na kile walichoamini ni sahihi kwa wakati huo. Kiasi fulani nilijalaumu kwa kushindwa ku-wamentor wanachama wangu ili watambue kiongozi mzuri ni yupi lakini ilinibidi niheshimu katiba. Baada ya muda vijana wale wakatafuna fedha yote na asasi ikafa na bahati mbaya muda wangu wa kutoka chuoni ulikuwa umewadia na sikupata nafasi ya kuifufua.

Katika mgogoro wa Chadema tumesikia watu wakisema ‘Chama hiki tumekitoa mbali’ mara ohh ‘Chama hiki watu wamekifia’ . Maneno ya aina hii yanamaanisha kuwa Chama kile ni mali ya watu walio’kisotea’ hadi kikafika kilipo. Mimi nikijiunga leo hata kama nina maono mazuri lakini kwa kuwa ‘sijakisotea’ itakuwa nadra sana mimi kukua ndani ya Chadema kwa kuwa tayari kina wenyewe. Hili laweza kuwa jambo jema lakini iwapo hatutakuwa na mifumo ya kuruhusu mawazo yaliyo nje ya kile tunachokiamini hatutaendana na mabadiliko halisi ya upepo wa kisiasa. Kiongozi mwenye busara ni yule anayeweza kuwa-mentor waliochini yake wawe viongozi bora kwa muda wake wa kikatiba na pindi muda huo ukiisha awaache wengine sasa waendelee. Hapo ‘umma na jamii utamtukuza’ kama inavyosomeka sehemu ya kiapo cha madaktari. Migogoro mingi hutokea pale chama kinapowagawanya wanachama wake kwa makundi ya ‘wakongwe’ na ‘wa juzi’ na majina mengine kadhaa. Wanaweza kuwemo wakongwe ambao huhitaji nguvu mpya ili kukabili changamoto mpya za kisiasa.

Kwa kumalizia kwa leo kwa kuwa muda umenitupa mkono, kwa kuzingatia maelezo na mifano yangu hapo juu, hata tuwe na mifumo mizuri kiasi gani, si rahisi kudhibiti nidhamu ya mtu mzima. Njia rahisi ingalikuwa ni kujenga misingi ya kujenga fikra za kinidhamu toka awali kabisa kwa misingi ya kimalezi na makuzi ndani ya chama. Labda sasa ni nafasi ya kuwa-mentor vijana ili wajenge fikra za kinidhamu kabla hata hawajafikiria kuwa viongozi. Ni hapo tu tutakuwa tumetatua tatizo katika ngazi ya mzizi wake.

Pili, tunahitaji viongozi ambao ni role models wasiokuwa na hulka ya tamaa ya madaraka. Katika mgogoro huu wa Chadema, wakati nilitegemea Mbowe atumie busara kwa kujiengua, ili abaki kuwa mentor wa yule atakayekuja, nilitegemea pia Zitto awakanye wanachama waliofanya kila aina ya uchafu kwa niaba yake, I mean kwa kushinikiza kuwa arudishwe. Nilitegemea Zitto atumie busara zaidi ya kuwaacha ‘wawakomoe’ wabaya wake na ‘waonyeshe kuwa ananguvu za kisiasa'. Viongozi wa aina hii hawafai kabisa kuwa viongozi maana si role models kwa sisi vijana wenye aspiration ya kufanya siasa.Ni kwa kuwa na viongozi wasio na fikra za visasi na kukomoana na wenye maadili mema hasa kutokana na misingi ya makuzi na malezi ndani na je ya chama ndipo tutakuwa na siasa tunayoiita siasa safi. Tunahitaji kuwa na misingi ya kimalezi ya chama ambalo itajenga fikra za kimaadili ili sasa vijana hawa watakapoenenda kinyume na malezi waliyopatiwa kichama ndipo mifumo ya kinidhamu itumike kuwadhibiti.

Wasalaamu,
Mlosi K. Mtulutumbi
 

celincolyn

JF-Expert Member
Dec 17, 2013
243
0
Mlosi K. Mtulutumbi Duh! Kweli mkuu umeongea kitu cha maana sn. Unajua mazingira yana mchango mkubwa wa kuwafanya watu aidha kuwa wema maeneo yao ya kazi au nyumbani na familia zao. Mf. Mimi binafsi nayafurahia maisha pindi niwapo nyumbaini na familia yangu kuliko kuwa kazini nikishirikiana na watu ambao binafsi naona ni wabinafsi, wapenda makundi na wanaofurahia kuona wananyenyekewa kuliko kitu chochote. Mpaka ss nafikiria kuacha kazi ili nikajifanyie biashara zangu kuliko kufanya kazi na watu tusio aminiana na mbaya zaidi ni pale wanapokuwa si wawazi kwenye mambo ya kazi na unapokuwa mkweli inakuwa nongwa zaidi. Tubadilike jamani kama ni vyeo makazini basi tuangalie uwezo na si nani na rafiki wa nani.

Anyway good analysis.
Napita tu mm mwenyewe mgeni.
 
Last edited by a moderator:

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,013
2,000
Tatizo lililopo kwenye mgogoro huu wa Chadema na migogoro mingi ya kisiasa sio kwamba watu hawajui nini cha kufanya, ila watu hawako tayari kufanya jambo sahihi iwapo jambo hilo halibebi maslahi yao ya kisiasa.
 

jnuswe

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,270
1,195
Mwandishi title na ulicho andika ni tofauti kabisa , unawezaje kukosoa wanaosema chama hiki nimekitoa mbali au wanaosema chama hiki kina damu yangu wakati na wewe ulisha wapa uhalali huo. Kwa nini useme Mbowe alitakiwa ajiweke pembeni amwachie Zitto nafasi na yeye awe Mentor wake, "I doubt about this analysis". Chadema ni taasis Kubwa wala sio Mbowe na Zitto

Ni kikwambia wewe na Mwanakijiji mnatumika utapinga ?
 

gastone

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
329
0
Mwandishi title na ulicho andika ni tofauti kabisa , unawezaje kukosoa wanaosema chama hiki nimekitoa mbali au wanaosema chama hiki kina damu yangu wakati na wewe ulisha wapa uhalali huo. Kwa nini useme Mbowe alitakiwa ajiweke pembeni amwachie Zitto nafasi na yeye awe Mentor wake, "I doubt about this analysis". Chadema ni taasis Kubwa wala sio Mbowe na Zitto

Ni kikwambia wewe na Mwanakijiji mnatumika utapinga ?

tatizo ndani ya cdm kuna kundi 'flani' linaamini linamamlaka kuliko wanachadema wengine wote - ukitoa mawazo tofauti tu na wanachotaka kukisikia mara moja utaitwa msaliti/mhaini/Lumumba buku 7 nk
kundi hilo lisiloamini ktk haki na usawa kwangu mie ndo kikwazo kikubwa ktk kufikia mabadiliko tunayoyataka 2015...........lenyewe linaangalia zaidi 'nani kasema' au 'nani kafanya' - mfano rahisi na wakaribuni ni uvunjifu wa maadili wa mwenyekt wetu wa chama ukiachilia mbali tuhuma nyingine za huko nyuma.
wafuasi wamevaa miwani ya mbao hawataki kuona, sasa tafakari ingekuwa ni zito hali ingekuwaje?!
 

jnuswe

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,270
1,195
tatizo ndani ya cdm kuna kundi 'flani' linaamini linamamlaka kuliko wanachadema wengine wote - ukitoa mawazo tofauti tu na wanachotaka kukisikia mara moja utaitwa msaliti/mhaini/Lumumba buku 7 nk
kundi hilo lisiloamini ktk haki na usawa kwangu mie ndo kikwazo kikubwa ktk kufikia mabadiliko tunayoyataka 2015...........lenyewe linaangalia zaidi 'nani kasema' au 'nani kafanya' - mfano rahisi na wakaribuni ni uvunjifu wa maadili wa mwenyekt wetu wa chama ukiachilia mbali tuhuma nyingine za huko nyuma.
wafuasi wamevaa miwani ya mbao hawataki kuona, sasa tafakari ingekuwa ni zito hali ingekuwaje?!
Acha siasa za maji taka your a poor judge how can you judge someone kwa kusikiliza upande mmoja ? je umesikiliza upande wa pili achilia mbali hilo there is the third part ambaye ni katibu wa bunge naye ujamsikia alafu umefikia hitimisho kwa maneno ya Mwigulu
 

IsangulaKG

Verified Member
Oct 14, 2010
707
250
Mlosi K. Mtulutumbi Duh! Kweli mkuu umeongea kitu cha maana sn. Unajua mazingira yana mchango mkubwa wa kuwafanya watu aidha kuwa wema maeneo yao ya kazi au nyumbani na familia zao. Mf. Mimi binafsi nayafurahia maisha pindi niwapo nyumbaini na familia yangu kuliko kuwa kazini nikishirikiana na watu ambao binafsi naona ni wabinafsi, wapenda makundi na wanaofurahia kuona wananyenyekewa kuliko kitu chochote. Mpaka ss nafikiria kuacha kazi ili nikajifanyie biashara zangu kuliko kufanya kazi na watu tusio aminiana na mbaya zaidi ni pale wanapokuwa si wawazi kwenye mambo ya kazi na unapokuwa mkweli inakuwa nongwa zaidi. Tubadilike jamani kama ni vyeo makazini basi tuangalie uwezo na si nani na rafiki wa nani.

Anyway good analysis.
Napita tu mm mwenyewe mgeni.

Celincolyn,
Pengine si busara kuyakimbia matatizo kwani hata kutoaminina kupo katika biashara. Ni vema ukaruhusu kujipambanua uwezo wako kwa kuhimili mikikimikiki ya kutokuaminiana
 

IsangulaKG

Verified Member
Oct 14, 2010
707
250
Mtanzania mwenzangu pengine hujasisoma hoja vizuri. Haya ni madhara ya kusoma kichwa cha habari na mistali miwili ya mwisho!

Mwandishi title na ulicho andika ni tofauti kabisa , unawezaje kukosoa wanaosema chama hiki nimekitoa mbali au wanaosema chama hiki kina damu yangu wakati na wewe ulisha wapa uhalali huo. Kwa nini useme Mbowe alitakiwa ajiweke pembeni amwachie Zitto nafasi na yeye awe Mentor wake, "I doubt about this analysis". Chadema ni taasis Kubwa wala sio Mbowe na Zitto

Ni kikwambia wewe na Mwanakijiji mnatumika utapinga ?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom