Kuuelewa Mgogoro wa CHADEMA - 6 - HITIMSHO NA MAPENDEKEZO

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
KUELEKEA SULUHISHO LA KUDUMU – 6

Nina uhakika utakuwa umefuatana nami toka mwanzo wa makala hii katika kuangalia kiini cha mgogoro ndani ya Chama Kikuu cha upinzani nchini ambacho kimebeba matumaini ya mamilioni ya watu. Toka mwanzo nimeweza kuonesha mambo kadha wa kadha lakini kubwa zaidi ni suala la nidhamu ya chama na jinsi gani muundo na mfumo wa chama umechangia katika kuanzisha migogoro. Jana tumeangalia kwa kudokeza jinsi wanasiasa watatu maarufu ndani ya chama hiki ambavyo kutokana na nafasi zao wanahusika katika kuhakikisha migogoro haitokei na inapotokea inashughulikiwa mara moja. Nimeonesha baadhi yale ambayo naamini ni matatizo kwa viongozi hawa.

Katika sehemu hii ya mwisho mpendwa msomaji tutaangalia yale ambayo nayaita mapendekezo ya jinsi ya kutatua na kumaliza mgogoro wa sasa na kujiandaa kuzuia na kushughulikia migogoro mingine iliyokwishatokea na ambayo inaweza kutokea baadaye. Hata hivyo kabla sijaangalia mapendekezo haya ambayo nina uhakika yanaweza kuwashangaza baadhi ya watu niseme mambo machache ya msingi nisije kuyasahau kabisa.

1. Migogoro na Migongano Itaendelea kutokea: Mahali popote ambapo pana watu wameamua kufanya jambo kwa pamoja ukiwapa muda, fedha, vyeo na mambo mengine lazima kutatokea kusuguana na kugongana. Hili ni jambo la kawaida na ni la afya kama inatokea kwenye taasisi kwani ni katika migogoro na migongano hiyo watu hujipambanua uwezo wao, udhaifu wao na waliokuwa butu watajikuta wananolewa na wenzao. Japo hili ni kweli mar azote tatizo linakuja ni jinsi gani kikundi au taasisi inaingilia kati migogoro, kuielewa na kuitafutia suluhisho la haki, usawa na la kudumu.

2. Kuna aina ya migogoro ambayo haivumiliki: Japo hilo la kwanza ni kweli lakini pia ni kweli kwamba baadhi ya migogoro na migongano haiwezi kuvumilika kwani inatishia moja kwa moja uwepo wa kikundi cha watu. Mwanzoni nimetumia mfano wa Jeshi kuonesha kuwa nidhamu ni kitu muhimu sana jeshini. Askari wakati wa vita hawezi kuanza kampeni ya kupatana na adui au kuwadhoofisha makamanda wake au kutoa siri za jeshi. Huu si mgogoro tu ni ugomvi ambao jeshi haliwezi kuvumiliwa. Ndio maana hata katika Katiba yetu ya Muungano tumeweka wazi kabisa kuwa hakuna mtu yeyote anayeweza kuisalimisha nchi kwa adui wakati wa vita au kutangaza kusalimu amri isipokuwa chombo halali kabisa kufanya hivyo.

3. Baadhi ya migogoro haiwezi kutatulika kirahisi au kwa kufanya maamuzi ya haraka. Migogoro mingine (kama siyo yote) inahitaji kuangaliwa kwa kina chake kabla ya maamuzi kuchukuliwa kuimaliza. Hili ni muhimu hasa pale panapohusisha migogoro ya viongozi. Viongozi wanapogongana kwa kawaida wanawagawa na wanachama au wafuasi wao na kama wakiachwa muda mrefu bila kuingiliwa basi madhara ya wao kufanya hivyo yanakuwa makubwa. Hivyo, wakati wowote ule mgogoro mkubwa unapotokea inapaswa kufuata utaratibu wa kina kuelewa na hatimaye kutafuta suluhisho sahihi na la kudumu.

4. Taasisi hazipaswi kuacha migogoro ianze kufukuta au viongozi waanze kuonesha utovu wa nidhamu kabla haijaingilia kati. Nimewahi kusema huku nyuma kuwa miongoni mwa vitu vibaya katika siasa zetu ni kile nilichokiita “siasa za kunyemeleana”. Ni sawasawa na wazazi wanapomuona mtoto anapotoka lakini wanamwachilia apotoke bila kumkemea hadi mtoto anapofika mahali pabaya sana ndio wazazi wanaingilia kati na kutoa laana! Wanasiasa ambao wanaonesha kwenda nje ya chama wanapaswa kushughulikiwa mara moja, kwa haraka na kwa uthabiti (promptly and swiftly). Kwenye taasisi kama ya chama cha siasa kuna mambo ambayo hayapaswi kuwekwa kiporo, mtu akianza kuyumba tu anatakiwa ashughulikiwe mara moja kujaribu kumrudisha kwenye mstari na kama inaonekana hawezi kurudi basi kumtimua au kumuondoa katika nafasi alizokuwa nazo.

Baada ya kusema hayo naomba niendelee na mapendekezo yangu ambayo msingi wake ni hoja zima toka tulipoanza. Mapendekezo yangu yako ya aina mbili hivi; upande mmoja kuna mapendekezo ya hatua za kuchukua kujenga muundo na mfumo wa kukabiliana na migogoro kabla haijawa mikubwa na sehemu ya pili nitatoa mapendekezo juu ya mgogoro ambao umekuwa kwenye fikra za watu wengi hivi karibuni – ule wa kuvuliwa uongozi kina Zitto, Dr. Kitila na Mwigamba ambao pia unatishia wao kuvuliwa uanachama. Sehemu ya pili kwangu ni rahisi zaidi kuitolea maoni kwani kama umenisoma toka mwanzo utakuwa umenielewa vizuri.
Mapendekezo ya Kimuundo na Mfumo (Katiba)

Huku nyuma nimeonesha baadhi ya yale ambayo nayaona kuwa ni matatizo ya kimuundo na mfumo wa CDM kama chama cha siasa; matatizo ambayo naamini yamechangia kuibuka, kukua na kuendelea kuibuka kwa migogoro ya hapa na pale. Baadhi ya mapendekezo yangu hapa ni haya yafuatayo:

1. Mabadiliko Makubwa ya Katiba: CDM inahitaji kufanya mabadiliko makubwa ya Katiba ambayo yataileta Katiba hiyo katika ulimwengu wa vyama vya siasa vilivyo katika mfumo wa vyama vingi ambao unakidhi haja na matakwa ya kidemokrasia. Nilionesha jinsi mfumo wa sasa ulivyonakili kutoka Katiba ya CCM kiasi kwamba madudu ambayo CCM inafanya tutajikuta tunahangaika nayo kwa CDM endapo itashika madaraka.

Baadhi ya mabadiliko hayo (mengine si ya mada hii) ni kuweka ndani ya Katiba majukumu ya viongozi wa kitaifa ili madaraka yao yawe yanatoka kwenye Katiba. Baadhi ya madaraka ambayo yanatakiwa yawe wazi kwenye Katiba ni suala la kusimamia maadili na nidhamu kwa viongozi wa chini na hili liwe muhimu pia kwa viongozi wa Kanda. Baadhi ya madaraka ambayo yamewekwa kwenye Kamati Kuu ya chama naamini yanapaswa kuhamishwa kwenda kwenye Kanda ili kuweza kushughulikia matatizo kwa haraka na kwa ufanisi badala ya kusubiri Makao Makuu kuingilia kati. Makao Makuu wabakie kushughulikia viongozi wa kitaifa, na wabunge tu pamoja na viongozi wa kanda. Viongozi wa Kanda washughulikia viongozi wa Mikoa na Wilaya wakati viongozi wa mikoa wawe wanashughulikia viongozi wa chini yao. Madiwani washughulikiwe na viongozi wa Kanda na maamuzi ya ngazi hiyo yawe ya mwisho.

2. Kuundwa kwa Chombo cha Nidhamu: Licha ya kutoa madaraka kwa viongozi wa kitaifa kushughulikia matatizo ya maadili na nidhamu ipo haja ya kuweka chombo huru ambacho kitawajibika kusimamia nidhamu katika chama. Kwa mfano, kuundwa kwa Kamati ya Nidhamu (Disciplinary Committee) ambayo itakuwa ni sehemu ya Sekretariati ya chama/ chini ya Sekretariati. Hii itaondoa ulazima wa vikao vya Kamati Kuu kushughulikia masuala ya nidhamu ambayo yangeweza kumalizwa na vyombo vingine. Madaraka ya chombo hiki kama yalivyo madaraka ya kamati nyingine yanapaswa kuwekwa wazi kwenye Katiba.

Chama cha Conservatives cha Uingereza (Tory) ambacho CDM kimejipanga nao nacho kina Kamati ya aina hii ambayo mara kadhaa imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kinidhamu dhidi ya viongozi mbalimbali. Kwa mfano, mwaka jana Kamati hiyo iliwasimamisha wadhamini wa tawi la chama hicho wa North Somerset kwa makosa mbalimbali mojapo ni lile la kiongozi wa Tawi hilo kutumia ofisi za chama kama ofisi zake za kufanyia biashara zake. Tawi hilo likajikuta linawekwa chini ya uangalizi wa moja kwa moja wa makao makuu.

3. Kuzipa nguvu Kanuni za Maadili na Miiko ya Uongozi (Code of Conduct and Leadership Ethics): Kuweka utaratibu ambapo viongozi wote wa kitaifa, wabunge, / watendaji wa makao makuu na viongozi wa mikoa na kanda wanaweka sahihi katika waraka wa kukubali kutenda kazi kwa mujibu wa maadili na nidhamu ya chama. Kwa watu ambao wamefanya kazi kwenye taasisi mbalimbali za ndani na za nje mojawapo ya nyaraka wanazoweka sahihi kabla ya kuanza kazi ni Kanuni za Maadili (Code of Conduct/Ethics). Kanuni hizi zipate nguvu kutoka kwenye Katiba. Katiba ilivyo sasa (Ibara 2.3) inasema kuwa “Maadili ya Chama ndiyo yatakayoainisha sifa, nidhamu, utii, uwajibikaji na dhamira ya wanaChama, watendaji na viongozi wa Chama katika ngazi zote. Maadili haya yanajumuisha uongozi wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee.” Katiba ya sasa tayari inatoa nafasi hiyo kwenye Ibara za 5.1.4 na 5.4.3. Hata hivyo, Katiba haijalazimisha kwa viongozi licha ya kula kiapo cha kuisimamia Katiba ya CDM wanapaswa pia kukubali kwa maandishi kufuata kanuni za maadili na utendaji wa chama.

Ibara ya 9.2 imetoa nguvu kwa Baraza Kuu kutunga kanuni hizi za maadili. Hata hivyo, kama nilivyosema hapo juu kanuni hizi hazijawekwa katika utaratibu wa kuhakikisha kiongozi anapoapishwa kushika nafasi fulani alazimike kuweka kwa maandishi kukubali kwake kuzitii kanuni hizi. Hii ni namna nyingine ya kuwafunga viongozi wajue kuwa wanapokiuka kanuni hizi hatua zitakapochukuliwa dhidi yao wasishangae au kuona wameonewa au wanaandamwa. Viongozi wanapaswa kuwa watu wa kwanza kuonesha utii wao kwa Katiba ya Chama na kufuata nidhamu ya chama. Kila kiongozi ni lazima awe na nakala iliyosainiwa ya kukubali maadili na miiko ya uongozi.

Sehemu hiyo ya maadili ni lazima ianishe mahusiano ya viongozi na viongozi, viongozi na wanachama, wabunge na viongozi wao (bungeni na nje ya Bunge). Viongozi wote wa CDM wanaotoka katika kuchaguliwa au kuteuliwa wanapaswa kukubali miiko na maadili ya chama.

4. Kufanya mabadiliko na Kuleta nidhamu Makao Makuu: Katika hili kwa kweli nazungumzia kwa kuangalia matokeo tu. Kama nilivyoonesha kuwa kumekuwa na uvujaji wa habari za Makao Makuu na wakati mwingine baadhi ya maafisa wa Makao Makuu wamekuwa wakitoa kauli mbalimbali (kwa majina yao au kwa majina ya kimtandao) kiasi cha kuonesha kurushiana vijembe kati yao na viongozi wao au viongozi wengine wa chama. Naamini hilo nalo ni ukosefu wa maadili. Ni lazima watendaji wa makao makuu wawe ni watu ambao wanaweledi na maadili ya kazi waliyopewa na chama na kuachana na malumbano yasiyo na sababu. Mambo ya wanasiasa waachiwe wanasiasa mambo ya utendaji wa chama yafanywe na watendaji wa chama.

Wiki iliyopita huko Marekani Mwenyekiti wa Kamati ya Mafunzo ya Chama cha Republican Steve Scalise alimfukuza kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Kamati hiyo Bw. Paul Teller kwa kukosa kuwa na imani naye. Kosa kubwa la Teller ni kumzungumza Mwenyekiti wake na kushirikiana na vikundi vingine katika kujaribu kutafuta kura za kupitisha sheria moja ambayo imekuwa mwiba kwa chama hicho.

Tunapozungumzia nidhamu hatuzungumzii ya wanasiasa tu bali hata watendaji wasio wanasiasa na wale wote ambao ni sura ya chama katika Makao Makuu. Sijui hili linaweza kufanywa vipi lakini naamini Mwenyekiti na Katibu Mkuu wataweza kufikiria namna ya kuhakikisha kuwa watendaji walio chini yao wanakiwakilisha chama kwa weledi wote unaotakikana. Binafsi sijapendezwa sana na propaganda zinazofanywa ki CCM kiasi kwamba tofauti kati ya vyama hivi viwili inaanza kufutika zaidi na zaidi.

Nimewahi kusema huko nyuma kuwa tunapotaka kubadilisha watawala hatutaki kubadilisha sura; hatuna tatizo la sura; tunataka kubadilisha watawala kwa sababu tunataka kubadili utawala. Tusije tukawapa watu utawala wakawa wamebadilisha sura za watawala lakini utawala ukawa ni ule ule wa kiCCM. Wananchi wa Zambia walijifunza kwa Frederick Chiluba kama vile Wamalawi walivyojifunza kutoka kwa Bakili Muluzi.

5. Kuweka Utaratibu wa Kutangaza Maslahi (Full Disclosure): Mojawapo ya mambo ambayo yanahitaji uamuzi wa haraka na kufanyiwa kazi mara moja ni suala la viongozi wakuu wa chama (wa makao makuu) na wabunge kuwa na utaratibu wa kutangaza na kutoa taarifa juu ya mahusiano yao ambayo yanaweza kuleta taswira mbaya. Chama ni lazima kiwe na utaratibu wa jinsi gani viongozi wake watahusiana na viongozi wa vyama vingine na ni katika utaratibu gani ili isije ikaleta mwonekano mbaya. Tayari tumeona mahusiano ya John Shibuda na Zitto Kabwe na viongozi wengine wa chama tawala yanavyokwaza baadhi ya wanachama na hata kusababisha waitwe majina.

Kwa watu waliofanya kazi kwenye taasisi za binafsi au zinazoshindana kuna fomu ambazo mtu wa cheo fulani anatakiwa kujaza na mojawapo ni hizi za kuwa na full disclosure au zile zenye kuzuia mgongano wa kimaslahi na washindani wake. Hii ni katika kuzuia mwonekano wowote au uwezekano wa kutokea mgongano wa aina fulani ya kimaslahi. Pamoja na hili ipo haja ya kuwa na Makubaliano ya Usiri (Confidentiality Agreement/Non Disclosure Agreement) ambayo yanamfunga kiongozi kutotoa siri za chama au siri ambazo zinapaswa kulindwa kwa mtu yeyote chini ya tishio la kufukuzwa uanachama.

Hapa hatuzungumzii kuficha madudu, ufisadi au vitendo vya uvunjaji wa sheria kwani hilo ni kinyume na kanuni hii kabisa. Tunazungumzia kile kinachoitwa (legitimate secrets) za chama; mikakati, mbinu, mipango, n.k ambayo endapo Chama kingine kikijua basi kinaweza kutumia nafasi hiyo kujinufaisha. Hili linapaswa kuzingatiwa na wafanyakazi wa makao makuu kama ilivyo kwa wanasiasa ambao wanaweza kuwa na nafasi (access) ya kujua siri hizo.

6. Mnadhimu wa Upinzani Apewe Nguvu Bungeni:
Sijui ni kwa kiasi gani Tundu Lissu ambaye ni Chief Whip wa upinzani ana nguvu za kuwaweka wabunge wake kwenye mstari. Hili ni muhimu wabunge wajue kuwa wanaenda kule siyo tu kuwakilisha na kuwasilisha matamanio yao na njozi zao au za watu wa majimbo yao lakini wako pale pia kwa ajili ya kukiwakilisha chama kilichowapa nafasi ya kugombea Ubunge huo. Hili ni muhimu liangaliwe kichama na upande mwingine KUB aangalie kwa kushirikiana na Spika na Kamati ya Bunge ya Uongozi ili kuona jinsi gani kazi na majukumu ya Mnadhimu Mkuu inaweza kuboreshwa zaidi.

7. Katika Masuala ya Fedha CDM Inahitaji Kuweka Utaratibu mzuri zaidi: Mojawapo ya mambo ambayo yanasumbua sehemu nyingi na taasisi nyingi ni masuala ya fedha. Mojawapo ya mambo ambayo binafsi naamini yanatakiwa kupewa uzito mkubwa ni kuondokana kabisa na utaratibu wa viongozi kukikopesha chama au kutoa misaada ambayo yaweza kuchukuliwa kama kukopesha chama au kujipa ujiko ambao wanachama wengine hawawezi kufanya.

Ukiangalia Katiba ya CDM – kama nilivyoonesha jana – chama hakiruhusiwi kikatiba kukopa. Iwe kutoka kwa wanachama au kwa taasisi za fedha. Katiba ya CDM inataja vyanzo vya mapato ya chama kuwa ni (Ibara 8:1): (a) Ada na viingilio vya wanaChama, (b) Michango ya hiari ya wanachama na wafuasi wa Chama, (c) Michango ya hiari ya watu wa ndani na nje wanaounga mkono Chama, (d) Misaada kutoka kwa vyama rafiki vya kisiasa vya ndani na nje ya nchi, (e) Misaada na ruzuku toka ndani na nje ya nchi, (f) Mapato yanayotokana na hisa na miradi halali ya Chama.

Utaona kuwa mikopo SIYO mojawapo ya vyanzo vya mapato ya chama. Sasa wanachama (wawe viongozi au vinginevyo) wanapokopesha chama uwezo huo unatoka wapi? Wanaweza kutoa misaada lakini hawawezi kukopesha chama. Na hatari ya hili ni kuwa hata kukopa Benki au kwenye taasisi za fedha inaweza kuwa inakatazwa.

Hili la mikopo linaweza kurekebishwa katika Katiba na kutoa nafasi kwa chama kutoa hata mikopo midogo midogo kwa wanachama wake wa muda mrefu ili kusaidia kuinua maisha yao. Hili linahitaji utafiti wa jinsi linavyoweza kufanyika siyo lengo la makala yangu hapa.

Upande mwingine CDM inahitaji kuweka wazi mapato yake na matumizi yake kwa wanachama wake ili kujitofautisha na vyama vingine na kujenga imani zaidi. Kwa mfano michango iliyoendeshwa chini ya M4C imegubikwa na maswali mengi na kukosekana kwa utaratibu mzuri ambao ungeeleweka. NI matumaini yangu kuwa mikutano hii itakapoanza tena kutakuwa na utaratibu mzuri zaidi na chini ya usimamizi mzuri zaidi. Binafsi ningeona kuwa kila mwezi CDM kupitia mtandao wake ingeweka wazi mapato na matumizi ya fedha kama ambavyo inafanywa kwenye fedha zinazoenda kwenye Halmashauri, Shule, Vijiji n.k ambapo wananchi wanaweza kuona fedha zinavyoingia na kutumika. Katika hili CDM wanahitaji kufikiria namna ambayo wanaweza kuweka masuala ya fedha wazi kwa wanachama wao.

Pamoja na hayo yote naamini CDM ni chama kinachokubalika na kupendwa na mamilioni ya Watanzania; wakati umefika kumobilize hawa wananchi katika kupata mitaji na fedha za kuweza kukiendesha chama na wakati huo huo kuwa na vitega uchumi ambavyo vitaipatia chama fedha zaidi na hatimaye kuondokana na kutegemea ruzuku. CDM ina wafanyabiashara wengi tu kwanini haijaanzisha mradi wa kuingiza mapato? Kwanini haijatafuta mahali pa kuwekeza hisa – wakati nafasi hizi zipo nyingi tu? CDM ikijijengea uwezo wa kifedha itaweza pia kufanya mambo mengi ya maendeleo – kuanzisha mashule, mahospitali, ujenzi wa nyumba za kupanga n.k bila kutegemea serikali au wahisani kutoka nje. Uwezo huu upo na ninaamini haujatumiwa ipasavyo.Tumeona jinsi CCM ilivyotumia nafasi hii vibaya na hata kujiingiza katika vitendo vya kifisadi (Deep Green Finance) CDM ijioneshe utofauti wake katika hili. Siyo katika ngazi ya taifa tu hata kwenye mikoa na ngazi za chini CDM iweke utaratibu ili matawi ya CDM yaweze kufanya uwekezaji wa kujipatia kipato badala ya wao pia kulalamikia kutegemea Makao Makuu au misaada ya wanachama wenye uwezo.

Yapo na mambo mengine ya jumla ambayo ningeweza kuyaweka kwenye haya mapendekezo lakini nitawaachia wengine nao watoe mawazo yao katika kukosoa ya kwangu au kuongezea katika haya.

Suala la Zitto na Wenzake
Suala la Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe na wenzake waliovuliwa nafasi za uongozi kwangu si suala gumu kivile kulipatia ufumbuzi wa kudumu. Hata hivyo naamini uamuzi wa KK unapaswa kutegemea mwitikio wa kina Zitto katika kutekeleza maagizo ya Kamati Kuu ya kujieleza kwanini wasivuliwe uanachama.

Chama Kina Uwezo na Haki ya Kusimamia Nidhamu
Kwa wale ambao tumefuatana toka mwanzo wa makala hii watakumbuka kuwa nimejenga hoja ya msingi kuwa nidhamu ni msingi wa mafanikio ya jambo lolote lile. Iwe nidhamu ya kujisomea au nidhamu ya kuandika au nidhamu ya kufanya utafiti. Bila nidhamu ni vigumu sana kufanikiwa katika jambo lolote. Katika taasisi au kikundi cha watu waliokubaliana kufanya jambo fulani nidhamu ndiyo gundi inayowaunganisha pamoja kwani kila mmoja kwa nafasi yake na kwa wajibu wake akitekeleza anachotarajiwa kufanya basi lengo lililokusudiwa litafikiwa.

Katika chama cha siasa suala hili ni la muhimu sana tena zaidi hasa kwa sababu linahusiana na uongozi wa mamilioni ya watu. Chama cha siasa siyo taasisi ndogo ambayo mtu anaweza kujifanyia lolote bila kuwa na matokeo makubwa mabaya. Kwenye kikundi kidogo mtu mmoja akiamua kujifanyia kivyake wakati mwingine haina madhara makubwa kwani ni rahisi kusahihisha. Lakini kwenye kikundi kikubwa ambacho kina malengo makubwa madhara.

Haki hii ya chama kusimamia maslahi yake na nidhamu ya viongozi wake ni suala lililoko kwenye mikono yake yaani ni prerogative ya chama. Hili ni jambo la msingi kulielewa. Chama hakipaswi kumuangalia mtu au kikundi cha watu na kuona aibu. Hivyo, uamuzi wa Kamati Kuu tukiamini kuwa umezingatia ushahidi wote mbele zake ni uamuzi ambao ulikuwa kwenye chombo halali na maagizo yake yalipaswa kutiiwa.


Mojawapo ya matatizo ambayo naamini yamechangia sana huu mgogoro ni wanachama kugawanyika na kufuata uongozi rasmi wa chama na uongozi wa Zitto. Zitto kama kiongozi wa chama alipaswa kusimama na kutii viongozi wake wa chama na kuwa chini yao siyo kuwa nao sambamba. Kama Mbunge na Kiongozi Zitto alipaswa kuhakikisha kuwa anakuwa karibu na chama chake na viongozi wenzake na kushughulikia hofu zao mara moja.

Kwa bahati mbaya sana imeonekana mara kadha wa kadha Zitto akitoa kauli mbalimbali nyingine zikionekana kukinanga chama chake yeye mwenyewe. Tuchukulie mfano suala la ukaguzi wa vyama vya siasa. Suala hili ni muhimu sana katika demokrasia lakini jinsi alivyolishughulikia amejikuta tena kwenye matatizo kwani ilionekana moja kwa moja anajaribu kushindana na chama chake na kusababisha malumbano mengine yasiyokuwa ya lazima. Kama kiongozi ndani ya chama alipaswa kuwa na mawasiliano na viongozi wenzake ili kwamba hata anapopeleka hoja yake Bungeni basi ajue kuwa wenzake wako nyuma yake.

Kinyume chake alijikuta kwenye matatizo mengine – japo ya nia nzuri ya kutaka uwajibikaji kwa vyama vya siasa- kwa kukosa mawasiliano ya karibu na wenzake. Ukiangalia utaona kuwa lipo kundi la wanachama (kama ni kubwa au la sijui) ambalo limejionesha kuwa linamfuata Zitto na limefikia hata kutoa changamoto kwa Kamati Kuu ya chama. Tumeshuhudia wenyewe baada ya Zitto nawenzake kuvuliwa uongozi baadhi ya watu walijitokeza waziwazi kupinga maamuzi hayo. Hili linaweza kuonekana ni jambo dogo lakini pia ni jambo kubwa; kwanini chama kimefika hapa? Kwanini kumekuwa na kama uongozi sambamba?

Baada ya KK kutoa agizo la kujitetea Zitto na Wenzake walipaswa kutii
Nimesema huko nyuma kwenye suala la insurbodination na kwanini ni muhimu kwa watu kujifunza kutii na kufuata maelekezo ya vyombo vilivyo juu yao. Kamati Kuu baada ya kuwavua uongozi iliwapa maagizo kina Zitto ya kujieleza kwanini wasivuliwe uanachama. Cha kushangaza sana Zitto na wenzake hawakutii hilo moja kwa moja na wakati mwingine hata hawakusubiri kupata barua zao za kutakiwa kujieleza na badala yake wakaenda tena mbele ya vyombo vya habari na kurusha maneno makali ambayo kwangu yalionesha kutokuelewa maana ya kuwa chini ya uongozi wa chombo cha juu. Hawakupaswa kufanya hivyo hata kama waliamini kuwa walikuwa na sababu ya kufanya hivyo. Badala yake waliendelea kujitetea hadharani na kutoa maneno ambayo upande mmoja yalionekana kuwapa shime watu wanaowaunga mkono.

Sijui ni juhudi gani huko nyuma zimewahi kuchukuliwa na viongozi wa juu kuhusu Zitto au kiongozi mwingine katika jitihada za kumrejesha kwenye mstari. Sijui ni ka kiasi gani Zitto au kiongozi mwingine alipata shida kutii maagizo hayo. Binafsi naamini ni muhimu sana kwa watu hasa viongozi kujifunza kukubali maagizo kutoka vyombo vya juu badala ya kuyapinga au kuyachallenge hata kama wanajua hawako sahihi.

Ni muhimu hapa kusema kuwa kuna watu wanafikiria nazungumzia kutii tu bila kuuliza maswali (blind obedience). La hasha, ninachozungumzia ni tunu ya kukubali kukosolewa na kuelekezwa na vyombo vya juu. Bahati nzuri nimeshafanya kazi kwenye makampuni ambapo maagizo yanatoka juu kwenda chini au maelekezo fulani. Wakati mwingine maelekezo hayo yanaweza yasionekane kuwa na maslahi au yasiyoeleweka; ni jukumu la anayelekezwa kutaka maelezo zaidi.

Wakati wowote kiongozi anaona hakubaliani na maelekezo ya watu waliojuu yake hapaswi kuyapuuza. Kama anaona maelekezo au maagizo yanapingana kabisa na misimamo yake au yanapingana na yeye angependa yawe basi kiongozi huyo anapaswa kujiuzulu. Huu ni utaratibu wa kidemokrasia. Demokrasia siyo tu kupinga au kubishanana viongozi wako lakini pia ni demokrasia kukubali matokeo ya kufanya hivyo – miongoni mwao ni kujiuzulu. Huwezi kuwa kiongozi ukapinga vyombo vya juu yako halafu ukataka kubakia kuwa kiongozi!

Je Zitto na Wenzake Wavuliwe Uanachama?
Binafsi sina tatizo kabisa na viongozi ambao chama kinaona hakiwezi kuendelea nao kuvuliwa uongozi na uanachama. Kama nilivyosema hapo juu hili ni suala la chama na maslahi yake. Baada ya uamuzi wa CDM kuwavua uongozi kina Zitto nilitoa mchango wangu na kusema ipasavyo kuwa kama habari hizo zitathibitishwa “inanikumbusha TANU 1958 na 1963. Hili limeachwa kwa muda mrefu mno hadi limefika hapa. Lilitakiwa lisipate nafasi ya kufika hapa kabisa.”
Ninaamini suala la kina Zitto halikupaswa kuachwa kufika hapa lilipofika. Uongozi wa CDM ulipaswa kuhakikisha kuwa unaingilia kati mapema zaidi kabla hali haijafikia ilipofikia ili kuhakikisha kuwa haifiki mahali watu wanatimuana uanachama. Wakati mwingine mtu anaweza kuanza kupotea taratibu na ni jukumu la viongozi kujaribu kumrudisha kwenye mstari. Kumwacha mtu apotee sana halafu mwisho kumfukuza naamini ni kukaribisha majanga. Ni sawasawa na suala la John Shibuda; baadhi yetu tunaamini alitakiwa avuliwe uanachama miezi mingi iliyopita lakini ameachwa kwa muda mrefu kiasi kwamba naamini wananchi waliomchagua wakidhani wamechagua mbunge wa CDM wanaweza kuwa wamenyimwa mwakilishi waliyemtaka!

Kwa upande wa kina Zitto suala hili lilipaswa kushughulikiwa mapema zaidi na si kwa njia ya kunyemeleana (kile nilichokiita siasa za kunyemeleana); viongozi wa juu na vyombo vya juu kama vilikuwa na mashaka na Zitto au kiongozi mwingine yeyote hawakupaswa kumuacha kwa muda mrefu hivyo, walitakiwa waingilie kati mapema zaidi. Sijui yawezekana juhudi hizi zimefanyika na ni matumaini yangu kama watavuliwa uanachama jitihada hizi inabidi ziwekwe wazi ili isije kuonekana kuwa uamuzi huu umechukuliwa bila kuchukua hatua za kina za kumrudisha au kuwarudisha kwenye mstari.

Mwaka 1958 Chama cha TANU kilijikuta kinawafukuza baadhi ya wanachama wake maarufu kufuatia uamuzi wa TANU kushiriki “Kura Tatu”. Kwa wanaokumbuka baadhi ya watu walioondoka kufuatia uamuzi huu ni pamoja na Zuberi Mtemvu na Sheikh Suleiman Takadir aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU (Makao Makuu). Kwa wasiojua historia vizuri Nyerere na Takadir walikuwa ni marafiki wa karibu sana lakini uamuzi wa kushiriki kura tatu uliwatenganisha sana na hawakuweza kupatana tena. Kulikuwa na suala la dini na ni masalia ya hawa waliotoka katika TANU na kuanzisha AMNUT (All Muslim National Union of Tanganyika) na ANC – cha Abbas Mtemvu ambacho nacho kilikuwa na mwelekeo wa kidini vile vile. TANU ilimvua vyeo vyake Takadir, Zuberi Mtemvu yeye aliachia nafasi yake ya Ukatibu Mkuu. Hawa wote walikuwa ni watu maarufu katika siasa za nchi wakati ule.

Hiyo haikuwa mara ya mwisho kwa viongozi wa chama kufukuzwa au kujiondoa wenyewe pale ambapo waliona kuwa hawakubaliani sana na sera au uongozi wa chama. Ilikuwa hivyo pia mwaka 1963 na mwaka 1968. Kwa hiyo siyo jambo geni kabisa na halitakuwa la kwanza katika Tanzania viongozi mashuhuri kuvuliwa uanachama au wao wenyewe kuondoka.

Uamuzi wa Kuwavua au Kuwabakisha Ufanywe kwa Umakini
Binafsi naamini kuwa kwa kuangalia hoja zote nilizotoa hapa uamuzi wa kuwaachia uanachama au kuwavua bado uko mikononi mwa Kamati Kuu. Wao ndio wameona ushahidi, wao ndio wamechunguza na wao bila ya shaka wanajua zaidi ya kilicho nyuma ya yaliyotokea labda kuliko mtu mwingine yeyote. Kwa vile wameshawavua uongozi ni wazi kuwa suala la kuwavua uanachama ni suala la muda tu. Ni uamuzi ambao haupaswi kufanywa kwa woga, upendeleo au husuda; waangalie ushahidi uliopo mbele yao na uzito wa ushahidi huo na kuona adhabu inayopaswa kutolewa baada ya ile iliyokwishatolewa (kuvuliwa uongozi).

Uamuzi Sahihi Juu ya Zitto na Wenzake ni Upi basi?
Hata hivyo naamini kuwa uamuzi huu unahitaji kupimwa vizuri na kuangaliwa vizuri. Unahitaji kupimwa siyo kwa kuangalia kiwango cha makosa tu lakini pia kwa kuangalia michango ya viongozi hawa kwa chama. Wakati mwingine ni rahisi sana kuwahukumu watu vikali kwa kuanglaia makosa yao tu na kusahau kabisa kuangalia michango yao.
Kwa maoni yangu uamuzi sahihi wa kufuata baada ya kusikiliza utetezi wao (kama wamejitetea) ni kuwapa masharti ya kukubali kwanini wasivuliwe uanachama na kama watakubali masharti hayo basi wataendelea kuwa wanachama. Baadhi ya Masharti ambayo yanapaswa kuwekwa wazi kwao:

1. Kutokufanya jambo lolote ambalo linaweza kuonekana au kutafsiriwa kukihujumu chama.
2. Kuwekwa chini ya uangalizi maalumu wa Kamati Kuu (wazee waandamizi wa chama wanaweza kuhusishwa) kuangalia mwenendo wao kwa kipindi ambacho kitawekwa.
3. Kuvunja makundi ikiwemo kutaka watu wanaowaunga mkono ama kuja chini ya uongozi wa chama au wao wajiondoe.
4. Kutokujihusisha na mkakati wowote wa kufanya mabadiliko katika chama na kusubiri taratibu za uchaguzi kuwekwa wazi ili wafuate taratibu hizo kugombea nafasi za uongozi.

Na masharti mengine muhimu ambayo watatakiwa kukubali.

Endapo masharti hayo yatakubaliwa na Zitto na wenzake basi wapewe Onyo Kali na nafasi moja ya kujirekebisha katika kipindi kilichowekwa. Kama hawatokubali masharti hayo – na ni lazima yawe masharti yanayoonesha hekima, haki na busara – basi Kamati Kuu ichukue uamuzi ambayo uko mikononi mwake huku wahusika wakibakiwa na haki ya kukata rufaa kwenye Baraza Kuu. Endapo wataamua kukata rufaa Baraza Kuu waambiwe mapema kuwa yale masharti hayatakuwa sehemu ya ofa tena bali swali litakuwa ni kuvuliwa kwao uanachama kuthibitishwe au kusithibitishwe.
Vyovyote vile ile ilivyo, KK ichukue uamuzi kwa kuangalia uwezo wake, hekima zake na bila kujali vitisho au maoni ya baadhi ya wanachama ambao wengine wamekuwa kama wanajaribu kuteka chama kuwa ni lazima watu wafukuzwe au wasikuzwe. Uamuzi uliojengewa hoja vizuri na ukichukuliwa kwa usahihi na hata ukizingatia maoni ya watu mbalimbali ni uamuzi ambao utapata kuungwa mkono na wanachama, mashabiki na wapenzi wa CDM.

Lakini uamuzi ni lazima uchukuliwe na uwe mwanzo wa kuchukua maamuzi kwa haraka ili hatimaye kuzuia migogoro mingine kuanza na kukua hadi kufikia mahali pa kutimuana. Ni bora kuzuia migogoro kuliko kufukuza wanachama. Binafsi sina tatizo lolote la kifikra la uamuzi wowote utakaochukuliwa alimradi uwe umejengewa hoja ipasavyo na unaoonesha kuwa kanuni za msingi za nidhamu, kupata haki na kuwajibishana zimezingatiwa.

MWISHO
 
Mkuu MMJ bado unajizungusha saana, kwa ufupi ni kuwa;

Kamati Kuu inapaswa kuwavua uwanachama, hao wasaliti, Zitto Zuberi Kabwe, Dkt. Kitila Mkumbo na Mwagamba hapo ndio tutajua kuwa Kamati Kuu ina busara na iko sahihi.

Kwa upande mwingine mkuu MMJ, hujatoa suluhisho/ushauri kwa hao wasaliti...

Ni kwmaba, waambie watoke CHADEMA wakaanzishe chama chao. pia nanyi muwaunge mkono huko...

Why wanangania CHADEMA, wakati vyama viko kibao na bado wana nafasi ya kuanzisha kipwa, kwa muundo na vyeo wanavyovitaka wao?
 
Chadema wakimfukuza ZZK 2015 slaa akipata kura nusu ya kura za majimarefu korogwe nahama nchi
 
Mzee mwenzangu, huwezi kutoa hitimisho halafu useme au utumie neno SIJUI. soma ulichokiandika hapo kwa Chief Whip
 
Hii ndio tabu ya kuandika makala ukiwa MacDonald unakunywa milk shake wakati kwenye field hujui hata kinachoendelea.
 
Mzee Mwanakijiji unadai chama kilinde nidhamu ya viongozi na katiba ya chama wakati huo huo unatetea wasaliti wa chama tuelewe na wewe ni sehemu ya mgogoro?

Tunaomba usikwepe kujibu maswali ya Yericko Nyerere.

Baada yakuzisoma makala zake tano zenye udhui la kulandana kwa jicho la tatu zaidi, imenilazimu kumuuliza maswali machache ili kujua zaidi msingi wa makala zake na yatarajiwayo KESHO.

1. Mkuu Mwanakijiji, maamuzi ya kamati kuu yalikuwa halali ama haramu kwamjibu wa katiba ya Chadema ya mwaka 2006?

2. Kutokana na maamuzi hayo, kuna haja ya chama kuacha katiba na kusaka kinachoitwa suluhu kwenye meza ya mduara?

3. Ipi nafasi ya Chadema katika uzingatiaji wa katiba yake na miiko ya chama katika mfumo huu wa vyama vingi nchini?

4. Wewe umekuwepo katika anga za siasa za Tanzania kwa mda mrefu sana, na umekuwa karibu kisiasa na wanasiasa wengi akiwemo Zitto Kabwe, je ipi nafasi ya Zitto Kabwe wa leo katika siasa za Chadema zinazotembea na kuishi katika katiba yake?

5. Vyama vya CUF, CCM na NCCR MAGEUZI vimeshaadhibu wanachama wake tena kwakuwavua uanachama kabisa huko nyuma, naomba uwathibitishie makutano wa jf ama popote pale kama uliwahi kutumia nguvu inayoshahabiana na hii unayotumia leo katika kubatilisha maamuzi ya cc ya Chadema,


Majadiliano ya hoja ni msingi wa ujenzi wa taifa lenye tija katika nyanja zote,

NB

Mods nawaomba msiunganishe uzi huu na zingine,
 
Kwa sumu ambayo ameimwaga na anaendelea kuimwaga Zitto nchini na hasa jimboni mwake (sijazungumzia ya kabla ya kuvuliwa uongozi); hafai na hapaswi kuendelea kuwa mwanachama kwa maslahi ya CDM. Ni bora kuyumba (kama kweli kupo, sijaona uyumbaji sana Kigoma) kuliko kuendelea kufuga mtu mbinafsi na msaliti kama Zitto (ushahidi wa ubinafsi na usaliti wake umetolewa mara kadhaa sina haja ya kutaja).
 
nimesoma mapendekezo yako yote ndugu Mzee Mwanakijiji lakini hakuna ulipogusia au kupendekeza suruhu ya hii kitu hapa chini. ambacho ndiyo chanzo kabisa cha mgogoro huu.iwapo na wewe hujui chanzo cha yote hayo nakupa pole.

attachment.php
 
Last edited by a moderator:
KUELEKEA SULUHISHO LA KUDUMU – 6

1. Kutokufanya jambo lolote ambalo linaweza kuonekana au kutafsiriwa kukihujumu chama.
2. Kuwekwa chini ya uangalizi maalumu wa Kamati Kuu (wazee waandamizi wa chama wanaweza kuhusishwa) kuangalia mwenendo wao kwa kipindi ambacho kitawekwa.
3. Kuvunja makundi ikiwemo kutaka watu wanaowaunga mkono ama kuja chini ya uongozi wa chama au wao wajiondoe.
4. Kutokujihusisha na mkakati wowote wa kufanya mabadiliko katika chama na kusubiri taratibu za uchaguzi kuwekwa wazi ili wafuate taratibu hizo kugombea nafasi za uongozi.

Mkuu haya masharti ni kitoto sana, ukirudia kusoma no. 1 3, na 4, ni kitu kimoja tu.

no.2 ndi kituko, napendekeza masharti yawe;

1. Kwamba, kutokufanya mkutano wowote wa kisiasa mahali popote kwa kutumia kofia ya CHADEMA,
2. Kwamba, kutovaa "magwanda" yetu ya "ukamanda" mahali popote
3.Kwamba, kutofanya wala kukunyaga mkuutano wowote wa CHADEMA mahali mpopote.
4.Kwamba, Kutotaja jina la CHADEMA kwa namna yoyote ile hadharani.
5.Kwamba, kutopatia Kadi yetu na tutamrudishia baada ya miaka 10 ikiwepo na mashart number 1-4
.

Asante MMJ, nadhani KK itafanya kama tajwa hapo juu (1-5) na wala si vinginevyo....
 
Mkuu MMJ bado unajizungusha saana, kwa ufupi ni kuwa;

Kamati Kuu inapaswa kuwavua uwanachama, hao wasaliti, Zitto Zuberi Kabwe, Dkt. Kitila Mkumbo na Mwagamba hapo ndio tutajua kuwa Kamati Kuu ina busara na iko sahihi.

Kwa upande mwingine mkuu MMJ, hujatoa suluhisho/ushauri kwa hao wasaliti...

Ni kwmaba, waambie watoke CHADEMA wakaanzishe chama chao. pia nanyi muwaunge mkono huko...

Why wanangania CHADEMA, wakati vyama viko kibao na bado wana nafasi ya kuanzisha kipwa, kwa muundo na vyeo wanavyovitaka wao?

tatizo upo bias mno kamanda, wengine wenye mawazo huru tunaamini mwenyekt pia ni tatizo mbona hujagusia mwanakjj kutokugusa?!
 
Kinachonishangaza hapa Mkuu Mwanakijiji ni kwamba hizi kamati kuu ndo walewale waliowahukumu mwanzoni na ndio watawasikiliza tena(nikimaanisha watu wale wale),sasa apo haki itatoka wapi?

Kwanini isiundwe hiyo kamati huru uliyosema kwa muda ili isikilize ilo shauri na kulitolea maaumuzi,kuliko meza hiyo hiyo akae mpuuzi Godbless J Lema !
 
Last edited by a moderator:
Nina uhakika utakuwa umefuatana nami toka mwanzo wa makala hii katika kuangalia kiini cha mgogoro ndani ya Chama Kikuu cha upinzani nchini ambacho kimebeba matumaini ya mamilioni ya watu. Toka mwanzo nimeweza kuonesha mambo kadha wa kadha lakini kubwa zaidi ni suala la nidhamu ya chama na jinsi gani muundo na mfumo wa chama umechangia katika kuanzisha migogoro. Jana tumeangalia kwa kudokeza jinsi wanasiasa watatu maarufu ndani ya chama hiki ambavyo kutokana na nafasi zao wanahusika katika kuhakikisha migogoro haitokei na inapotokea inashughulikiwa mara moja. Nimeonesha baadhi yale ambayo naamini ni matatizo kwa viongozi hawa.

KUELEKEA SULUHISHO LA KUDUMU – 6

Je Zitto na Wenzake Wavuliwe Uanachama?
Binafsi sina tatizo kabisa na viongozi ambao chama kinaona hakiwezi kuendelea nao kuvuliwa uongozi na uanachama. Kama nilivyosema hapo juu hili ni suala la chama na maslahi yake. Baada ya uamuzi wa CDM kuwavua uongozi kina Zitto nilitoa mchango wangu na kusema ipasavyo kuwa kama habari hizo zitathibitishwa “inanikumbusha TANU 1958 na 1963. Hili limeachwa kwa muda mrefu mno hadi limefika hapa. Lilitakiwa lisipate nafasi ya kufika hapa kabisa.”

Ninaamini suala la kina Zitto halikupaswa kuachwa kufika hapa lilipofika. Uongozi wa CDM ulipaswa kuhakikisha kuwa unaingilia kati mapema zaidi kabla hali haijafikia ilipofikia ili kuhakikisha kuwa haifiki mahali watu wanatimuana uanachama. Wakati mwingine mtu anaweza kuanza kupotea taratibu na ni jukumu la viongozi kujaribu kumrudisha kwenye mstari. Kumwacha mtu apotee sana halafu mwisho kumfukuza naamini ni kukaribisha majanga. Ni sawasawa na suala la John Shibuda; baadhi yetu tunaamini alitakiwa avuliwe uanachama miezi mingi iliyopita lakini ameachwa kwa muda mrefu kiasi kwamba naamini wananchi waliomchagua wakidhani wamechagua mbunge wa CDM wanaweza kuwa wamenyimwa mwakilishi waliyemtaka!

Kwa upande wa kina Zitto suala hili lilipaswa kushughulikiwa mapema zaidi na si kwa njia ya kunyemeleana (kile nilichokiita siasa za kunyemeleana); viongozi wa juu na vyombo vya juu kama vilikuwa na mashaka na Zitto au kiongozi mwingine yeyote hawakupaswa kumuacha kwa muda mrefu hivyo, walitakiwa waingilie kati mapema zaidi. Sijui yawezekana juhudi hizi zimefanyika na ni matumaini yangu kama watavuliwa uanachama jitihada hizi inabidi ziwekwe wazi ili isije kuonekana kuwa uamuzi huu umechukuliwa bila kuchukua hatua za kina za kumrudisha au kuwarudisha kwenye mstari.

Mwaka 1958 Chama cha TANU kilijikuta kinawafukuza baadhi ya wanachama wake maarufu kufuatia uamuzi wa TANU kushiriki “Kura Tatu”. Kwa wanaokumbuka baadhi ya watu walioondoka kufuatia uamuzi huu ni pamoja na Zuberi Mtemvu na Sheikh Suleiman Takadir aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU (Makao Makuu). Kwa wasiojua historia vizuri Nyerere na Takadir walikuwa ni marafiki wa karibu sana lakini uamuzi wa kushiriki kura tatu uliwatenganisha sana na hawakuweza kupatana tena. Kulikuwa na suala la dini na ni masalia ya hawa waliotoka katika TANU na kuanzisha AMNUT (All Muslim National Union of Tanganyika) na ANC – cha Abbas Mtemvu ambacho nacho kilikuwa na mwelekeo wa kidini vile vile. TANU ilimvua vyeo vyake Takadir, Zuberi Mtemvu yeye aliachia nafasi yake ya Ukatibu Mkuu. Hawa wote walikuwa ni watu maarufu katika siasa za nchi wakati ule.

Hiyo haikuwa mara ya mwisho kwa viongozi wa chama kufukuzwa au kujiondoa wenyewe pale ambapo waliona kuwa hawakubaliani sana na sera au uongozi wa chama. Ilikuwa hivyo pia mwaka 1963 na mwaka 1968. Kwa hiyo siyo jambo geni kabisa na halitakuwa la kwanza katika Tanzania viongozi mashuhuri kuvuliwa uanachama au wao wenyewe kuondoka.

Uamuzi wa Kuwavua au Kuwabakisha Ufanywe kwa Umakini
Binafsi naamini kuwa kwa kuangalia hoja zote nilizotoa hapa uamuzi wa kuwaachia uanachama au kuwavua bado uko mikononi mwa Kamati Kuu. Wao ndio wameona ushahidi, wao ndio wamechunguza na wao bila ya shaka wanajua zaidi ya kilicho nyuma ya yaliyotokea labda kuliko mtu mwingine yeyote. Kwa vile wameshawavua uongozi ni wazi kuwa suala la kuwavua uanachama ni suala la muda tu. Ni uamuzi ambao haupaswi kufanywa kwa woga, upendeleo au husuda; waangalie ushahidi uliopo mbele yao na uzito wa ushahidi huo na kuona adhabu inayopaswa kutolewa baada ya ile iliyokwishatolewa (kuvuliwa uongozi).

Uamuzi Sahihi Juu ya Zitto na Wenzake ni Upi basi?
Hata hivyo naamini kuwa uamuzi huu unahitaji kupimwa vizuri na kuangaliwa vizuri. Unahitaji kupimwa siyo kwa kuangalia kiwango cha makosa tu lakini pia kwa kuangalia michango ya viongozi hawa kwa chama. Wakati mwingine ni rahisi sana kuwahukumu watu vikali kwa kuanglaia makosa yao tu na kusahau kabisa kuangalia michango yao.
Kwa maoni yangu uamuzi sahihi wa kufuata baada ya kusikiliza utetezi wao (kama wamejitetea) ni kuwapa masharti ya kukubali kwanini wasivuliwe uanachama na kama watakubali masharti hayo basi wataendelea kuwa wanachama. Baadhi ya Masharti ambayo yanapaswa kuwekwa wazi kwao:

1. Kutokufanya jambo lolote ambalo linaweza kuonekana au kutafsiriwa kukihujumu chama.
2. Kuwekwa chini ya uangalizi maalumu wa Kamati Kuu (wazee waandamizi wa chama wanaweza kuhusishwa) kuangalia mwenendo wao kwa kipindi ambacho kitawekwa.
3. Kuvunja makundi ikiwemo kutaka watu wanaowaunga mkono ama kuja chini ya uongozi wa chama au wao wajiondoe.
4. Kutokujihusisha na mkakati wowote wa kufanya mabadiliko katika chama na kusubiri taratibu za uchaguzi kuwekwa wazi ili wafuate taratibu hizo kugombea nafasi za uongozi.
Kwamba Zitto ana hatia au hana hatia; bila shaka ni jambo la wana-CHADEMA wenyewe na katiba yao huku nikiamini kwamba uamuzi wowote hautatokana na personal issues bali kwa kuzingatia maslahi ya chama. Hali kadhalika, hata suala la kama Zitto na wenzake wanastahili kufukuzwa au hapana; hili nalo ni la wana-CHADEMA wenyewe bila kusahahu angalizo lililotangulia.

Pamoja na yote hayo, nahisi kama CHADEMA wako very sensitive na watu ambao ni source ya ruzuku kwa chama. Napata taabu sana kufahamu ilikuwa kuwa vipi mtu kama Shibuda ameendelea ku-exist ndani ya CHADEMA kwa muda wote huu ambao hakuna siri tena kwamba he's not there for CHADEMA, at least kwa kuangalia kauli na matendo yake. Zitto ni mtu ambae amekuwa akipata tuhuma nzito nzito kutoka kwa wana-CHADEMA, tena wa ndani kabisa. Binafsi, sina hakika ikiwa tuhuma ni za kweli au ni majungu lakini bado sijaacha kujiuliza inakuwaje mtu mwenye tuhuma mzito mzito kama anazopata Zitto bado ameendelea kuwa kwenye chama. Akili ya kawaida inanituma kwamba, ikiwa wana-CHADEMA wana uhakika na yale ambayo yamekuwa yakisemwa dhidi ya Zitto basi Mheshimiwa huyo alipaswa kuwa amefukuzwa zamani sana unless kama tuhuma dhidi yake zilikuwa ni majungu. Tuhuma ambazo Zitto amekuwa akipewa kwa miaka sasa ni tuhuma mzito mzito pengine kuliko hili la sasa la Waraka wa Mabadiliko lakini sijaacha kushangaa ilikuwa kuwa vipi Zitto aliachwa muda wote huo na kuja kupata "stahiki" yake sasa....mbona CHADEMA hawapo hivi?! Mbona wale Madiwani hawakucheleweshwa muda wote huo? Mbona Samson Mwigamba hakucheleweshwa muda wote huo? Huku nikiamini kwamba hasira za wana-CHADEMA wengi dhidi ya Zitto si huu waraka wa sasa bali matendo yake ya huko nyuma. Kwanini basi CHADEMA wamekuwa na kigugumizi dhidi ya Zitto na Shibuda kwa muda wote huu? Ni kwa ajili ya RUZUKU?

Frankly speaking, nashawishika kuamini kwamba ni hofu ya kukosa Ruzuku ya Wabunge wawili ndio inayowafanya CHADEMA washindwe kuchukua hatua dhidi ya Zitto(na Shibuda). Na kama hivyo ndivyo, basi hakuna kosa kubwa ambalo CHADEMA watafanya kama wataamua kumuacha Zitto kwa sasa ( kwa ajili ya hofu ya kupoteza Ruzuku) na kisha wakaamua kutafuta sababu na kumchukulia hatua hapo baadae. Wapo wana-CHADEMA ambao wana-undermine influence ya Zitto ndani ya CHADEMA; huku ni kujipa imani. Mwacheni Zitto aitwe; the guy ana influence ndani ya CHADEMA na jamii kwa ujumla. Ni kujidanganya kuamini kwamba hata leo hii Zitto akifukuzwa CHADEMA, chama hakitatetereka. BInafsi naamini kwamba, siku CHADEMA wakimtimua Zitto, CCM watafanya sherehe tofauti na watu wanavyoamini kwamba CCM watasikitika! Watafanya sherere si kwa sababu wanachuki na Zitto bali watafanya hivyo kwavile wanaamini CHADEMA sasa ndo inatetereka kama si kugawanyika! Hivyo basi, ikiwa CHADEMA waanaamini pasipo na shaka yoyote kwamba Zitto hafai tena kuwamo kwenye chama basi wakati muafaka wa kumuondoa ni sasa ili chama kipate muda wa kutosha kujikusanya upya coz', mtake msitake; Zitto akifukuzwa lazima CHADEMA itayumba! Ikiwa Zitto ataendelea kulelewa kwa hofu ya kupoteza ruzuku na kisha CHADEMA wakaja kuchukua hatua towards 2015; hapo lazima itokee disaster upande wa chama coz' u'll no enough time to reorganize.
 
Last edited by a moderator:
Kimsingi nitaunga mkono pendekezo la kufukuza kabisa Wasaliti na Waasi.

tungeanza kumtimua kwanza mwenyekt kwa sababu mbali ya tuhuma za ufisadi ndani ya chama - amejiongezea tuhuma nyingine mpya ya uzinzi dhidi ya viti maalumu..............
 
tatizo upo bias mno kamanda, wengine wenye mawazo huru tunaamini mwenyekt pia ni tatizo mbona hujagusia mwanakjj kutokugusa?!

Hata kama kamnda Mbowe ana Tazizo, mimi na wewe ndio wa kumjenga siyo kutaka kuanzisha makundi na mtandao wa kumpindua...

Je, hilo ndilo suluhu?
 
Hapana shaka kuwa kipengere cha kufanyia mabadiliko makubwa katiba yao, kinaweza kukata mzizi wa fitina chamani humo. Mapendekezo mengine na shauri zingine ulizoandika zitakuwa na msukumo imara mara baada ya kurekebisha katiba hiyo.
 
1. Mwanakijiji katiba ya chadema ipo ili kujenga chama au kubomoa chama??
kama ipo kujenga chama basi iheshimike na aitumike vilivyo.
kama ipo kubomoa chama basi hakuna haja ya chadema kuwepo .
 
Umeandika makala nzuri sana yenye lengo la kukijenga chama. Sina tatizo na mapendekezo yako kuhusu cdm kufanya mabadiliko makubwa ya kikatiba. Lkn umeonesha udhaifu mkubwa sana ktk kushauri namna nzuri ya kushughulikia mgogoro wa zitto na wenzake. Umeonyesha woga wa wazi mno! Toka mwanzo umeonesha mapungufu mengi mno ya zitto,umekiri juu ya urafiki wake na ccm nk. Lkn pia jinsi alivyoamua kushindana na KK kwa uamzi wake na wenzake wa kupinga uamzi wa KK kwa kutumia vyombo habari. Kwa hali ya kawaida,kosa hilo peke yake,linatosha kumuondoa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom