Kuua bila kukusudia! (?)

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,753
7,844
Afungwa kwa kukiri kumuua mumewe

2007-11-11 10:11:45
Na Jumbe Ismailly, Singida

Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma imemhukumu mjane Asha Ramadhani (43), kufungwa jela miaka mitano baada ya kukiri kosa la kumuua mumewe bila kukusudia.

Mfungwa huyo mkazi wa kijiji cha Irisya katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida alikiri kumuua mumewe Selemani Ntandu(70)kwa kumchoma na kijanga cha moto mwili mzima.

Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Mwanaisha Gwariko wa Mahakama Kuu,wakati wa vikao vya mahakama hiyo vinavyoendelea mjini Singida.

Mwendesha Mashtaka na Mwanasheria wa serikali Bi.Neema Mwanda alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Novemba 2002.

Mwanasheria huyo alidai siku hiyo saa 2:00 usiku katika kijiji cha Irisya Asha alimuua Ntandu baada ya kumchoma sehemu mbalimbali mwilini kwa kijinga cha moto.

Alidai kuwa mshtakiwa ambaye sasa ni mfungwa siku hiyo alirudi nyumbani akitokea kwenye pombe ya kienyeji akiwa amelewa chakari.

...sawa, madhali amekiri, 'naweza' kubali hakukusudia, lakini,...

Kwa mujibu wa Mwanasheria huyo wakati wanandoa hao wakiwa chumbani, mumewe alimhoji mkewe Asha sababu za kuendelea kulewa pombe wakati alimkataza tabia hiyo.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa huyo hakupendezwa na kukaripiwa badala yake aliamua kuchukua kijinga cha moto na kumchoma sehemu mbalimbali za mwili mumewe.

Mwanasheria huyo alidai muda mfupi baadaye Ntandu alifariki dunia na mshtakiwa huyo alimburuza hadi sebuleni na kumlaza chini.

Alichukua kamba ya kufungia ng`ombe na kuifunga kwenye paa la nyumba kisha kuiviringisha kwenye shingo ya marehemu mumewe.

Alidai kuwa baada ya kumtundika kwa lengo la kuharibu ushahidi alikwenda kwa majirani kuwapa taarifa kwamba mumewe alijinyonga hadi kufa.

Hata hivyo, ilisemekana kwamba majirani zake hawakukubaliana na maelezo hayo na walipofanya uchunguzi, waligundua kuwepo kwa damu kwenye kitanda cha wanandoa hao.

...hapo ndipo ninapoingiwa na mashaka iwapo ni kweli hakukusudia!

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, wakili wa kujitegemea Bwana Nyangarika, aliiomba mahakama hiyo impe adhabu nafuu mteja wake kwa kuzingatia kwamba amekaa mahabusu miaka mitano na kwamba alitenda kosa hilo akiwa amelewa pombe.

Alimtetea kuwa, kwa kuwa alikuwa amelewa ni dhahiri amejuta na pia ni mara ya kwanza kukosa.

Akitoa adhabu hiyo, Jaji Gwariko alisema Mahakama yake imetafakari maombi ya mshtakiwa yaliyotolewa kwa niaba yake na wakili wake Nyangarika.

Pia imebaini kuwa mshtakiwa pamoja na kuwepo kwa pengo kubwa la umri kati yao lakini alikuwa anampenda mumewe kwa sababu ameonyesha dhahiri kujutia kosa hilo.

``Kwa hivyo Mahakama hii imefikia uamuzi wa kumpa mshtakiwa adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka mitano jela ``, alisema jaji Gwariko.

...mnh, hainiingii akilini wajameni, hii inaweza kutokea tena katika jamii, kisingizio ikawa 'alilewa pombe, aliua bila kukusudia, ingawa pia alichukua kamba ya kufungia ng`ombe na kuifunga kwenye paa la nyumba kisha kuiviringisha kwenye shingo ya marehemu mumewe na kumtundika kwa lengo la kuharibu ushahidi.

swali;

...Inaingia akilini hii kweli?
 
Kwa hakika huu uhuru wa kutoa hukumu kwa jina la kaua bila kukusudia sasda linawaingia sana binadamu kiasi kwamba hata maana ya kuua bila kukusudia imepotea kabisa. Hebu tafakari, umemchoma mumeo kwa kijinga cha moto mwili mzima, kisha unaona tayari kisha kufa unapata akili nyingine ya kujaribu kufuta ushahidi ya kumning'iniza kama vile kajinyonga mwenyewe. Ikiwa huyu mama baada ya kuona uchomaji ule umetoa uhai wa mumewe aliyempenda sana basi ikiwa angeanguka chini na kuanza kupiga yowe kwamba hakutegemea ingekuwa vile na wananchi wakasikia yowe lile na kukuta mama yule akilia kisha akasimulia kilichojiri, hakika ningeunga mkono kwamba hakukusudia. Lakini hii hata haijakaa sawa. Nawashauri ndugu wa marehemu wakate rufaa.
 
Unaweza kushangaa Dito naye anafungwa kifungo cha nje kwa miaka miwili

...Naam, si unaona huyo 'mjane' kaombewa na defence lawyer wake apunguziwe adhabu kwakuwa keshakaa 'rumande' miaka mitano, ndio maana kahukumiwa mitano 'tu' mingine...

Kwa hakika huu uhuru wa kutoa hukumu kwa jina la kaua bila kukusudia sasda linawaingia sana binadamu kiasi kwamba hata maana ya kuua bila kukusudia imepotea kabisa...

...Nawashauri ndugu wa marehemu wakate rufaa.


...Labda watasema 'under influence' of alcohol, maana weshasema eti alikuwa kalewa 'chakari', vipi kama 'alimnywea'?

ndio maana naogopea hili, isijetokea tena na tena 'muuaji' akawa anaponea kunyongwa/kifungo cha maisha kwa kisingizio alikuwa amevuta sana bangi/ amelewa sana 'gongo', wakati 'ukweli' unajionyesha kitendo hicho kilikuwa pre-planned!

...ndio kusema DPP hawapo makini katika kuwakilisha/kusimamia kesi, ama ndio 'takrima' ishatembea?
 
hapo sheria sijui imetafsiriwa vipi,kuchukua kiji(a)nga cha moto inaelekea alikusudia maana alimchoma sehemu mbali mbali kama hakukusudia iweje amchome sehemu mbali mbali za mwili wake?
Sijui sheria labda nimetafsiri tofauti
 
Soulmate umeamua kuwa mwanasheria au? Nijuze ili nijue kuwa hii biashara ya machungwa naifanya peke yangu kuanzia sasa.

Nimewaza bila kukusudia ujue.

Kwa kweli wanasheria na wajuzi wa mambo haya mtujuze.
 
Back
Top Bottom