Kutupiana lawama na mustakabali wa ndoa za vijana………

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,354
Kuna kutupiana sana mipira na kulaumiana kati ya wanandoa vijana kuliko mtu anavyoweza kufikiria. Kila mmoja anataka mwenzake abebe majukumu makubwa na pengine zaidi kuliko mwingine.

Pengine baba kamwona mtoto akijisaidia na akashindwa kumchamba mtoto huyo akisubiri mama afanye kazi hiyo, wakati yuko jikoni akiandaa chakula, na baba anatazama TV. Hapa swala ni kuchagua moja, ama kushirikiana au kuvunja ndoa!

Nijuavyo mimi, kwenye ndoa imara na ya watu wakomavu, hakuna kazi ya mwanamke na ya mwanaume, labda kama kuna makubaliano kati ya wanandoa. Katika zama hizi, mke kuwa ndiye anayeilisha familia ni jambo la kawaida sana.

Baadhi ya vijana siku hizi, hasa mijini, wanalishwa na wake zao kutokana na ajira kuwa haba. Wanawake wanaweza ‘kubangaiza,' kutafuta riziki katika biashara ndogondogo, wakati waume zao ambao ndio kwanza wamemaliza masomo yao vyuoni au hata mashuleni wanasubiri ajira ambazo hazipo!

Kumbuka kwamba ushirikiano kwenye ndoa ni kujikana mwenyewe na kutafuta muafaka. Kama hamuwezi kushirikiana katika majukumu, basi mjue ndoa yenu haitadumu.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Top Bottom