Kutunza vitu usivyotumia Ni ugonjwa

meghan markle

JF-Expert Member
May 22, 2018
481
1,166
Unakuta mtu kamaliza perfume anatunza chupa, kamaliza lotion hatupi kopo dressing table imejaa kama dampo. Maviatu na nguo ya miaka nenda rudi havai, hagawi yanajaza tu space.

Jikoni sasa ndio hakufai.... Vikopo kama sita vya blueband iloisha, makontena ya ice cream, thermos imepasuka, hotpots zimechokaaaa... Yani vimejaa vinakua kama takataka jiko linakosa mvuto.

Huu Ni ugonjwa unaitwa Obsessive Compulsive Disorder ama Hoarding disorder.
Mara nyingine mtu ananunua kitu halafu hana matumizi nacho kinajaza tu nafasi.
FB_IMG_1556815505549.jpg
 
Unakua na nguo za ndani zimechakaa unashindwa hata kuzichoma moto kuna ex wangu flan wa kichaga anapesa kweli na mzuri kweli siku hiyo kaja home kumbe ndio siku aliyovaa chupi imetoboka kwa kweli nilimdharau na kumshusha
Thamani
 
Hii tabia wanayo hasa wazee wetu wa zamani. Yaani ana makorokoro kibao hata kazi nayo hana.

Wengine hawa dada zetu. Mtu ana manguo kibao mengine anamaliza hata miaka hajayavaa yapo tu.

Nashukuru huu ugonjwa umenipitia kushoto. Yaani kila mwaka mwingine naangalia kitu gani sikitumii kabisa.
 
Kabatini nina nguo nyingi ila nina kaugonjwa mwingine nikishikilia nguo moja hiyo hadi niikinai.
Una nyota ya ufundi garage.

Niuzie kabati nguo zangu mie nimezijaza kwenye mfuko wa rumbesa.
 

Similar Discussions

9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom