Kutundika bunduki! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutundika bunduki!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Bikra, Aug 6, 2009.

 1. Bikra

  Bikra Senior Member

  #1
  Aug 6, 2009
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Niliondoka nyumbani, kwa hali ya kunyatia,
  Na bunduki mkononi, na risasi nimetia,
  Nikajitosa mwituni, nyama kujitafutia
  Askari wa mwituni, kuwinda kanizuia.

  Nilikua na yakini, minofu ntajipatia,
  Kwani bunduki jamani, najua kuitumia,
  digidigi vichakani, wote wananitambua,
  Askari wa mwituni, kuwinda kanizuiA.

  Nilipopita mbugani, nipate kuangalia,
  wanyama walibaini, swala na pundamilia,
  nikaiunda plani, nipate kuwafikia,
  Askari wa mwituni, kuwinda kanizuia.

  Mara yakatabayani, nisiyoyategemea,
  askari wa porini, ngumu akanitilia,
  kasema itue chini, bunduki nakuambia,
  Askari wa mwituni, kuwinda kanizuia.

  Japo nyama watamani, siwezi kukuachia,
  kumbuka kuna kanuni, ukweli tunaujua,
  budi ukate leseni, ya hao ulochagua,
  Askari wa mwituni, kuwinda kanizuia.

  Nikajiinamia chini, hali nikifikiria,
  sasa nirudi nyumbani, bunduki sijafayatua?
  Hii ni balaa gani, mwindaji yanifikia,
  Askari wa mwituni, kuwinda kanizuia.

  Kutundika ukutani, bunduki yaning'inia,
  Ninakua mashakani, kutu isijeingia,
  nisijekwenda windoni, ikashindwa kufyatua,
  Askari wa mwituni, kuwinda kanizuia.

  Swala namwona porini, kulenga wanizuia?
  sasa pesa za leseni, nani atanigawia,
  si mia wala miteni, ni nyingi yahitajia,
  Askari wa mwituni, kuwinda kanizuia.

  Askari mhisani, nakuomba fikiria,
  hizo siku za mbeleni, nashindwa kuzingojea,
  bunduki i hatarini, itajashindwa kulia,
  Askari wa mwituni, kuwinda kanizuia.

  Nami sipendi utani, kuwinda nikinuwia,
  Na hasa risasi ndani, ikiwa nimeshatia,
  Ningali najiamini, swala wengi ntatungua,
  Askari wa mwituni, kuwinda kanizuia.

  Kalamu natua chini, pasipo kujizuia,
  Na mikono mashavuni, ambayo naegamia,
  Nitumie hila gani, tatizo kulitatua?
  Askari wa mwituni, kuwinda kanizuia.
   
  Last edited: Aug 6, 2009
 2. GP

  GP JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  yako bunduki, ni aina gani niambie,
  acha taharuki, nikuazime yangu uwindie,
  imeshazoea mikiki, inanifanya nijivunie,
  yangu haisemezeki, mawindo shurti ujihesabie,
  askari wa mwituni, kuwinda atakukubalia.

  bikra angalia, gobore usitumie,
  smg najivunia, askari lazima augulie,
  risasi nikitumia, askari muhimu agugumie,
  mwilini ikiingia, maumivu lazima asikilizie,
  askari wa mwituni, kuwinda atakukubalia.
   
Loading...