Kutumia shilingi bilioni moja kukagua miradi ya shilingi milioni mia nne | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutumia shilingi bilioni moja kukagua miradi ya shilingi milioni mia nne

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mbwago2007, Mar 6, 2011.

 1. m

  mbwago2007 Member

  #1
  Mar 6, 2011
  Joined: Oct 19, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumekuwa na kawaida ya viongozi wakuu wa kitaifa hususan rais na waziri mkuu wake kufanya ziara za mikoani na wilayani kwa lengo la kukagua miradi na wakati mwingine kuwawashukuru wapiga kura. Ziara hizo zinaligharimu taifa (walipa kodi mabilioni ya fedha) Kwa mfano rais anatumia kwenye ziara yake zaidi ya shilingi milioni mia sita kwenda kukagua au kuzindua mradi wa jengo la shule uluogharimu shilingi milioni mia mbili na unakabbliwa na uhaba wa fedha za kukamilisha mradi huo. Bila shaka katika muundo wa serikali yetu, rais anawakilishwa hadi kijijini, sasa sijui ni kitu gani kinachomfanya asafiri masafayote hayo na kwa gharama kubwa hivi kwenda kukagua miradi ambayo angeweza kupata taarifa kutoka kwa watendaji waliopo maeneo husika.
   
 2. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #2
  Mar 6, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Ni kushindwa kupanga vipaumbele
   
 3. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ngd yangu hiyo ndo inaitwa Tz, ni mchezo wa kekundu kwa kwenda mbele. Hakuna vipa umbele wala uwajibikaji. Kazi kweli kweli
   
 4. Mwanaitelejensi

  Mwanaitelejensi Senior Member

  #4
  Mar 6, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndio serikali ya ufisadi ndio maana hakatai safari yoyote yupo kazini kula kodi za walalahoi, hata kama ukiwa na shughuli ya kuchinja mbuzi ukimualika atakuja. Huyo ndio Kikwete mpenda safari a.k.a Vasco da Gama
   
 5. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Huo ndo unaitwa ulevi wa Madaraka. Watu hawaangalii kile wanachofanya kina matokeo gani kwa wale wanaodai kuwaongoza, wanajiangalia wenyewe. Mamisafara yale ya rais na waziri mkuu na makamu wa rais kuna watu wananufaika nayo sana! Ndo maana unaona rais hakai ofisini akichapa kazi bali kila wakati yuko barabarani au angani.

  Angalia ni nchi gani makini ambayo viongozi wake hawakai ofisini. Hiyo mikakati ya kuliendeleza taifa unaifikiria saa ngapi wakati kila siku uko safarini? Ni mfumo mbovu! Ni ulevi tu wa madaraka. Hakuna wanaofanya value for money kwenye masafari hayo ya rais na wakubwa wenzie. Watu wanataka tu rais aonekane kila wakati, eti ndo kumweka machoni mwa wapiga kura.

  Ni ulevi tu, ulevi wa madaraka!
   
 6. czar

  czar JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 340
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yap, akili ni nywele kila mtu ana zake. KUna jamaa alituma 5000 kwao, baada ya wiki akaenda kuhakikisha kama ilifika alitumia 10000 kwa nauli tu.
   
 7. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #7
  Mar 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Safari ndiyo njia halali ya kula hela mzee!! Wewe kwani hujui?
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  Mar 6, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Sijui kama ulichokiongea ni kweli au lah ila kama ni kweli inabidi budget iwabane.
  Reports zikiwafikia zinatosha hasa kwa miradi midogo midogo.
   
 9. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #9
  Mar 6, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Usishangae sana ndugu! Ndiyo staili ya pa diem hapa kwetu. Uzinduzi wa kisima cha maji ya ku-pump kwa mkono huku mkuu wa wilaya/mkoa akitumia vx!
   
 10. G

  Giddy Mangi JF-Expert Member

  #10
  Mar 6, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 833
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Pinda pesa anayotumia breakfast,lunch nd dinner+drinks akiwa nje ya Dar es Salaam ni 20 M.Source Intelligency
   
 11. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #11
  Mar 6, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Umeshajiuliza Mbowe na Silaa wanatumia fedha ngapi kuandaa maandamano ya uchochezi? na wanazitowa wapi hizo fedha?

  Muarubaini upo jikoni, itabidi wajieleze.
   
 12. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #12
  Mar 6, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  Hakika aina hii ya usanii imekua ikiniumiza sana kichwa. Ukiangalia magari yanayotumika katika misafara ya viongozi, hali yao ya kiafya(SIHA) na mavazi yao na ukalinganisha na sehemu inayotembelewa na hali ya watu wa sehemu husika hakika unabaki ukijiuliza hivi ni kweli ama unaota? na ni wewe tu unayeona hayo? Nahisi tunahitaji Muongozo wa kikatiba wa kazi za Raisi na safari ziwe zinapangwa miezi kabla....Hii zimamoto inanyoendelea ikomeshwe maana ndio iletayo maajabu ya kutumia.......kukagua mradi wa ......
   
 13. c

  carefree JF-Expert Member

  #13
  Mar 6, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Watz tupige kelele kwa sauti kubwa hii tunayoitoa hawasikii wanazidi kutukandami
   
 14. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #14
  Mar 6, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Humu Kwenye JF hawakusikii, ni wachache sana wenye hata kujuwa kuitumia internet. Tafuta mbinu mpya za kupayuka.
   
 15. M

  Mboja Senior Member

  #15
  Mar 6, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 158
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mr Safari, nafikiri mtu kama huyo alikuakua akipenda kula miguu ya kuku utotoni. Ila tu niseme kiongozi kama huyo ana ufinyu wa kufikiri!
   
 16. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #16
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  sIO BATHOLOMEO DIAZ??????????
   
 17. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #17
  Mar 6, 2011
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 499
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Duh! Kwani Chadema wanatumia pesa za walipa kodi? Mleta mada anazungumzia waliopo madarakani ambayo wanatumia pesa za serikali kwenye safari ambazo hazina tija.
   
Loading...