Kutumia Picha ya RAIS kwenye video yoyote ni kosa?

dadeez

Senior Member
Nov 30, 2010
112
139
Masaa machache leo ilianza kusambaa video ikimuonesha msanii maarufu wa vichekesho Tanzania Joti akiwa anamuwish Heri ya kuzaliwa Rais wa jamuhuri wa muungno wa Tanzania Mh Magufuli... Video hiyo fupi ya sekunde 59 ilipostiwa na joti mwenyewe bila shaka kupitia channel yake ya Youtube inayojulikana kama JotiTv ikimuonesha msanii huyo akimuwish Rais siku yake ya kuzaliwa na vituko vingine kadhaa mbele ya picha hiyo tukufu huku ikiwa imesimamishwa chini na joti akiwa amelala.. naakiongezea na vituko vingine kadhaa. Lakini masaa kadhaa baadae video hiyo iliondolewa ghafla na kutoka katika account hiyo ya Jotitv. Katika kufatilia hakuna tamko lolote lililotewa mpaka dakika hii... SWALI la Msingi JE NI MAKOSA KUTUMIA PICHA YA RAIS KAMA ALIVYOFANYA JOTI?
 
Back
Top Bottom