Elections 2010 Kutumia nguvu (violence) kwenye siasa kunaruhusiwa

3D.

JF-Expert Member
Sep 7, 2010
1,018
282
Nimesikitishwa sana na kauli ya Mzee Mwanakijiji ya tarehe 5 November, 2010 saa 3:05 asubuhi: "Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi" ambayo katumia muda mwingi kujaribu kujenga hoja kuwa katika ulimwengu wa waliostaarabu lugha "zinazochochea matumizi ya nguvu" hazina nafasi.

Nakubaliana na hoja kuwa nchi yetu kama nchi nyingine yoyote inahitaji kuwa na amani. Lakini natofautiana naye pamoja na watu wenye msimamo kama wake wa "Uchaguzi umeshapita, tuangalie mengine." Huu ni msimamo wa CCM (ambao ni wa hadaa). Nitaeleza.

CCM imekuwa mstari wa mbele kutumia vyombo vya habari hasa magazeti kumchafua Dr. Slaa na kumtusi. Magazeti kama Al-Huda yalifikia hatua ya kuchapisha picha za mafuvu ya binadamu yakidai Dr. Slaa kuchochea mauaji ya Mwembechai dhidi ya Waislamu. Magazeti kama Tazama, Taifa Letu etc yamekuwa yakimtukana Dr. Slaa na baadhi yao kugawiwa bure hasa yakiandika taarifa hasi juu ya Dr. Slaa. Gazeti la Serikali Habari Leo limemchafua sana Dr. Slaa. Gazeti la Serikali la Daily News lilitoa msimamo kuwa Dr. Slaa hatakuwa Rais wa tano wa Tanzania (Serikali kuu haikujitenga na kauli hii).

Mwishowe Magazeti ya Mwananchi na MwanaHalisi ndiyo yaliyotishwa kufungiwa badala ya Al-Huda na mengine. Baada ya Uchafuzi huu Magazeti haya sasa yanaombwa na Kikwete "Kusaidia kutibu vidonda vya Uchaguzi." Ni kweli yatafanya hivyo kwa kuwa Kikwete anajua kabisa kuwa ukihitaji magazeti yabomoe wakati wa uchaguzi yatumie halafu uchaguzi ukiisha yatumie tena kujenga kwa kuwa Watanzania ni mazezeta na wanaamini sana magazeti.

Kikwete anajua kuwa ukitaka kushinda iba kura, tumia majeshi kutisha na kupiga watu, tume ikishakuweka madarakani kwa ghilba wapo akina Mwanakijiji, Pengo, Mokiwa na Getrude Lwakatare ambao wakiongea tu "Kubalini matokeo, tunataka amani" basi Watanzania watakubali. Na akina Mzee Mwanakijiji wanatumia technique ya lugha "Katika ulimwengu wa wasomi" ili ukitofautiana nao uonekane siyo msomi na mpenda machafuko.

CCM wana akili timamu na wanaona kila hatua inavyokwenda. Uchaguzi utakuja, ataibuka Mrema au Slaa au Lipumba, atapigwa zengwe, ataitwa mdini. Kama ni Lipumba akigombea basi magazeti ya Kikristo ya kihafidhina yatamtukana Lipumba na kumwita mdini na mtu asiye na ndoa (Ilitokea year 2000). Kisha kura zitaibwa. Watu wote (including viongozi wa dini na akina Mzee Mwanakijiji) wataona kuwa kura zimeibwa. CCM itashinda. Polisi watapiga watu wanaodaiwa kuwa wapenda fujo na wanaotumiwa na viongozi waroho wa madaraka (Akina Dr. Slaa). Kikwete ataapishwa akiwa amejeruhi nchi.

Watu watabaki na alama za wino wa kura (indelible ink) huku wakizomewa na kutajwa kama wapenda fujo, wasokubali kushindwa, wanaotumiwa na wanasiasa na akina Mzee Mwanakijiji wataenda mbali zaidi na kuwaita "wasioelimika" na "waliojiunga JF juzi tu." Kuna memba wa JF ameshauri wana JF wachanga wapewe muda wa mwezi mmoja wa "Kutazama kwanza hoja zinavyotolewa na wakongwe kabla hawajapewa nafasi ya kuchangia."! Sawa bwana.

Ikumbukwe kauli za kuzuia Watanzania kudai haki yao na kutaka wawe makondoo (siyo kondoo) ni kuzuia mabadiliko. Haisaidii kutumia miaka milioni moja kujadili "nguvu za hoja" wakati inamchukua mgombea siku mbili kuchakachua kura na uongozi.

Pole Dr. Slaa. Pole sana. Najua hukutaka kugombea Urais. Ulichukua fomu ya Ubunge. Kamati Kuu ya CHADEMA ikakubana sana ugombee Urais. Ukakubali. Umejenga hoja sana katika kampeni (kama akina Mzee Mwanakijiji wanavyodai wanapenda). Kura zako zimeibwa. Sasa akina Mzee Mwanakijiji waliokushangilia wanakwambia "Uchaguzi umeshapita, tugange yajayo." Kwa maana fupi tu Dr. Slaa "usituharibie nchi yetu."

Watanzania wanapenda vitu vizuri lakini hawapendi gharama. Kwaheri Mkoloni Mzungu, karibu Mkoloni Mwafrika. Historia itatuhukumu. Nakubaliana na mawazo tofauti na yangu (kwa hoja lakini).

Mungu Ibariki Afrika,
Mungu Ibariki Tanzania,
Nawasilisha.
 
Mkuu well said!! hii post yako imenigusa kuliko post zote nilizozisoma baada ya uchaguzi.ndio wametuibia na yale magazeti ya sijui al nani huko walikuwa hawayaoni..nina uhakika lipumba kaenda pale kwenye kusikiliza matokeo ili asimharibie mwenzake kule zanzibar tu basi, ila kila kitu kipo wazi jinsi kura zilivyoibiwa na hiki sio kilio cha chadema au slaa, Slaa sio maskini halali kwenye nyumba za mabati kama maaskari wetu na halali kwenye nyumba za tembe na wala hahitaji kujenga nyumba ya bati au ya sementi, SLaa hana njaa wala shida yoyote ,yeye anachofanya ni kutuwezesha sisi watanzania tusio watoto wa wakubwa na tusio ndani ya mtandao.

Ila tumezipiga kura na kina kiravu wameziiba .ok poa hamna shida lenye mwanzo lina mwisho..kina CHENGE WANAMAKASHFA KIBAO WANATAKA KUWA SPIKA WA BUNGE,,,??? HII NI NINI? AU TUPO SAYARI NYINGINE?

WANATUN'GON'GA WAZI WAZI na sisi tunacheka. si ndio tushapewa matshirt! cha moto tutakiona
 
Hoja yangu ni kuwa lazima tupambane na mbinu chafu za Kikwete na wenzake na kuhakikisha kuwa njama zao zote chafu walizozitumia zinaanikwa wazi na ziwaandame maisha yao yote. Ni hoja yangu Chadema wasiache wizi huu wa kura kupita bila kupingwa.

Nimeshauri kesi ifunguliwe ili ushahidi wote uanikwe hadharani. Hii itatusaidia kupambana na njama kama hizo uko mbeleni. Tukiacha mambo haya yaendelee, tutakuja kuzungumza hoja kama hizi mwaka 2015 na kwa bahati mbaya kila uchao tunazeeka.
 
Heshima yako mkuu 3D shukrani kwa maoni lakini mkuu twende taratibu mkuu Mzee Mwanakijiji hakuna na maana tofauti kwamba tukae kimya hapana alikuwa na maana kuwa bado tunaweza kuipigania haki yetu kwa uungwana na si kwa vitisho ambavyo vinaveweza kuikosesha amani Tanzania.

Maana tunaweza kuingia kwenye machafuko na tusipate tunachokitaka kwa hivi tuendelee na maisha siku ya siku itafika basi tutaipata haki yetu. Wanaoandika kwenye magazeti au mitandao kumchafua Dr.SLAA hivyo ni namna wao wanavyofurahisha roho zao lakini mimi na wewe na wengine wote waliompigia kura SLAA tunamjua ni mtu wa namna gani kwa hivi lisikuumize sana kichwa wataaongea kwa muda halafu utafika wakati wataacha.

Tuwe wavumilivu tutumie zaidi busara zipo njia mbadala za kulia kilio chetu kikasikika na si kwa kutegemea tuanze kukimbizana tushindwe kwa kuelekea. Wanasema usibishane na mpumbavu na wewe utakuwa mpumbavu sasa wanaotukana wacha watukane ni mojawapo ya starehe yao. Tunaamini sote Dr.SLAA hakushindwa bali alishinda na ataendelea kushinda.

Amefanya kazi kubwa ya kuwaamsha watanzania.Kikubwa tuombeane sote uzima na maisha yaendelee wajameni. Tumeshalia sasa hatuwezi kuendelea kulia milele yote.
 
Ni kweli Mkuu. Katiba inaruhusu kufungua kesi kupinga matokeo ya Ubunge na chini ya hapo. Hairuhusu kufungua kesi dhidi ya tume ya uchaguzi kwa matokeo ya Urais, hii ndiyo changamoto. Utatuzi wake una mlolongo unaoweza kulazimisha kwenda mahakama ya katiba kwanza ili kifungu hicho kiondolewe, then ikiwa hukumu itapita hivyo ndipo kesi ifunguliwe mahakama kuu kupinga matokeo ya Urais.

In short ndo imetoka hiyo. Kama ulikuwa na kazi ya kusukuma mkokoteni basi rudi kazini na bandeji uliyofungwa mkononi (nani alikwambia ufanye fujo?)
 
Nakubali lakini lazima tuwe na mikakati ya kupinga udhalimu huu. Kunyamaza na kuogopa kubishana na mjinga wakati mjinga huyo anasababisha watu kuendelea kutopea katika umaskini, wakati anagawa raslimali za nchi si kitendo cha kizalendo. Hapa ni lazima tuwe na mikakati ya kupambana na utawala huu kwa mbinu zote halali za kisheria. Hii ni pamoja na kutoa ushahidi jinsi kura za Watanzania zilvyoibwa, jinsi Tume ya Uchaguzi ilivyoendesha uchaguzi kizembe na kwa kupokea amri za CCM.

Ni lazima tudai kuwajibishwa kwa viongozi wa Tume hii. Kwa bahati mbaya sana nimekuwa nibandika katika nyuzi mbalimbali katika mtandao huu uamuzi wa Mahakama ya Rufaa katika kesi ya Attorney General & 2 others v. Dr. Amani Walid Kaborou (1996) TLR 156 kwamba maamuzi ya Tume ya Uchaguzi yanaweza kupingwa mahakamani licha ya maelezo ya Ibara ya 74(5) inayokataza hivyo. Niletegemea watu wangezinduka hapa na kujadili hilo lakini hakuna hata mmoja aliyeliona au kulizungumza hilo.

Nimekuwa kama ninapoteza muda wangu kuwaeleza hayo.
 
Nimependa umeenda tofauti na mtazamo wa MM, ni hatari sana wote kuwa na mtazamo wa aina moja. Hili si bunge la CCM.
 
Mkuu 3D

umechambua vizuri lakini, Mie naomba niweke mawazo yangu kwa somo nililolipata MUAFAKA WA CCM NA CAF ZANZIBAR,,kuna wanachama waliojitolea maisha yao, waliuwawa, kuna wengine walienda ukimbizini mpaka SOMALIA kwa kusimamia HAKI je sasa hivi CCM na CAF wanakula BATA je HAWA watu waliwakumbuka, kabla ya huo muafaka wao ni kwanini wasingewafikiria waliokimbia nji na walio uwawa

MWANAKIJIJI anachojaribu kutafadhalisha kama nimemuelewa vizuri zitumike njia mbadala; Haihitaji akili ya kushe kuelewa kwamba UCHAGUZI HAUKUWA WA HAKI NA HURU lakini unataka wananchi wahamasishwe waende barabarani??Hilo halitakuwa na tija sio kwa CHADEMA Wala TAnzania kwa ujumla
 
Heshima yako mkuu 3D shukrani kwa maoni lakini mkuu twende taratibu mkuu Mzee Mwanakijiji hakuwa na maana tofauti ........ ......................Tumeshalia sasa hatuwezi kuendelea kulia milele yote.

Asante kwa mchango wako Mkuu Pakawa. Naamini 2015 CCM watarudisha sehemu kubwa sana ya majimbo yao yaliyokwenda upinzani, tena hata kwa ghilba. Tutaongea haya haya tena. Tuombeane uzima.

Nimnukuu Nyerere, "Tunataka Wakoloni watupe Uhuru wetu. Wasipotupa tutawashtaki Umoja wa Mataifa. Umoja wa Mataifa wasipotusikiliza tutawashtaki kwa Mungu. Mungu asipotusikiliza tutawashtaki kwa shetani."
 
Well said, wameweza Tarime watashindwa huko kwingine? Na ukondoo huu lazima yote yarudi kwa kishindo
 
Mkuu 3D

umechambua vizuri lakini, Mie naomba niweke mawazo yangu kwa somo nililolipata MUAFAKA WA CCM NA CAF ZANZIBAR,,kuna wanachama waliojitolea maisha yao, waliuwawa, kuna wengine walienda ukimbizini mpaka SOMALIA kwa kusimamia HAKI je sasa hivi CCM na CAF wanakula BATA je HAWA watu waliwakumbuka, kabla ya huo muafaka wao ni kwanini wasingewafikiria waliokimbia nji na walio uwawa

MWANAKIJIJI anachojaribu kutafadhalisha kama nimemuelewa vizuri zitumike njia mbadala; Haihitaji akili ya kushe kuelewa kwamba UCHAGUZI HAUKUWA WA HAKI NA HURU lakini unataka wananchi wahamasishwe waende barabarani??Hilo halitakuwa na tija sio kwa CHADEMA Wala TAnzania kwa ujumla

Heshima kwako Mkuu Prodigal Son. Ni dhahiri panapowezekana njia mbadala ni vizuri zitumike. Tatizo linabaki njia mbadala ni zipi (ambazo ni tofauti na zile mbadala za awali zilizoshindwa za kushtaki kwa Jumuia ya kimataifa na kujaribu kwenda mahakamani)?
 
Ni kweli Mkuu. Katiba inaruhusu kufungua kesi kupinga matokeo ya Ubunge na chini ya hapo. Hairuhusu kufungua kesi dhidi ya tume ya uchaguzi kwa matokeo ya Urais, hii ndiyo changamoto. Utatuzi wake una mlolongo unaoweza kulazimisha kwenda mahakama ya katiba kwanza ili kifungu hicho kiondolewe, then ikiwa hukumu itapita hivyo ndipo kesi ifunguliwe mahakama kuu kupinga matokeo ya Urais.

In short ndo imetoka hiyo. Kama ulikuwa na kazi ya kusukuma mkokoteni basi rudi kazini na bandeji uliyofungwa mkononi (nani alikwambia ufanye fujo?)
Naomba nikujibu kwa maelezo ya Jaji Mkuu Nyalali ndipo utaona kuwa bado kuna mwanya wa kupinga udhalimu huu Mahakamani.

Ndugu zangu hii ni sehemu ya kesi ya Attorney General & Others v. Dr. Amani Walid Kaborou (1996} TLR 156 ambapo Mahakama ya Rufaa chini ya Jaji Mkuu Nyalali, Robert Kisanga na Lameck Mfalila ilitoa uamuzi juu ya umuhimu wa kuendesha uchaguzi huru na haki. Na vilevile ilisema wazi kuwa hakuna kinga yoyote ile ya kikatiba dhidi ya maamuzi ya Tume ya Uchaguzi ambayo ni kinyume cha sheria. Nitajitahdi kuiweka hukumu nzima ili watu wajisomee. Naomba radhi kwa makosa yanayoonekana kwani katika kuitoa katika pdf mfumo umeshindwa kufanya kazi inavyotakiwa.

We now come to our reasons in support of our findings on ground number one in both memoranda of appeal concerning the validity of the Tamko Rasmi. We begin naturally by considering whether courts of law have jurisdiction to inquire into the validity of the Tamko Rasmi in view of the provisions of sub-article (12) of article 74 of the Constitution. That sub-article as amended by Act 4 of 1992 states:

'No Court shall have jurisdiction to inquire into anything done by the Electoral Commission in the exercise of its functions according to the provisions of this Constitution.'

On the face of it, it appears that the Constitution expressly prohibits the courts from inquiring into the validity of such things like the Tamko Rasmi, but on a deeper consideration of the principles that underlie the Constitution, it is obvious that such an interpretation of the Constitution is wrong. One of the fundamental principles of any democratic constitution, including ours, is the Rule of Law. The Principle is so obvious and elementary in a democracy, that it does not have to be expressly stated in a democratic constitution. However, perhaps for purposes of clarity, there is an express provision to that effect under the Constitution of the United Republic of Tanzania. It is Sub-Article (1) of Article 26 which states:

'Every person is obliged to comply with this Constitution and the laws of the United Republic.'

In the light of this principle, we respectfully agree with the sub- mission of Mr Werema Learned Senior State Attorney to the effect that Sub-Article (12) of Article 73 of the Constitution cannot be interpreted so as to protect unconstitutional or illegal acts or deeds, see the recent famous case of Anismic Ltd v. Foreign Compensation Commission (1).

Since Tanzania has reverted to dejure multi- party democracy, it is time the same was similarly articulated here. We are satisfied and we find that the High Court in this country, like the High Court in England, has a supervisory jurisdiction to inquire into the legality of anything done or made by public authorities such as the Tamko Rasmi. As a collorary, this Court has similar jurisdiction to do so in a matter properly before it, as in the present case.

We now come to our reasons in support of our finding to the effect that the Electoral Commission is empowered to make and issue the Tamko Rasmi but under the circumstances of this case, the Tamko Rasmi is invalid. It is patently clear that the Electoral Commission derives its powers under the Constitution and the Elections Act, 1985 as amended from time to time. Under para (b) of sub-article (6) of article 74 as amended by Act 4 of 1992, read together with ss (2) of s 4 of the Elections Act, 1985 as amended by Act 6 of 1992.

In our considered opinion, we are satisfied that on a true and proper interpretation of the above cited provisions of the Elections Act, the Electoral Commission is empowered to make regulations not only in furtherance of specific provisions of the Act, but also in furtherance of the purposes of the whole Act. From the scheme of the Act as manifested in the various provisions of the Act, including the provisions for secrecy of the ballot and for polling agents, counting agents, one person one vote, one candidate one seat, as well as those provisions concerning election campaigns and election offences, it is evident that the overriding purpose of the Elections Act is to secure the election of the President of the United Republic and the members of the parliament of the United Republic in a free and fair election. It is also implicit from the provisions of the Constitution.

Majaji wakaendelea kusema

As we have already stated, we concur with the reasons given by Mchome J, and we have additional reasons for upholding his finding. First, weare satisfied that the established rule of interpretation embodied in the Latin Maxim 'Expressio Unius EST Exclusio Alterius' that is, where matters are expressly stated, then any other matters of the same class not so expressly slated are excluded, does not apply to s.108 because that section provides defences to matters which are not expressly stated therein. Second, taking into account the principle which underlies the Constitution and the Elections Act, 1985 that elections shall be free and fair, we are of the considered opinion that an election which is generally unfree and unfair is not an election at all as envisaged by the Constitution and the Elections Act, and consequently anything which renders the elections unfree or, and unfair is in law valid ground for nullification of such purported D election. We are further of the considered opinion that any law which seeks to protect unfree and unfair elections from nullification would be unconstitutional.
 
mkuu imekaa sawa hii 2fanyie kazi.
 
Isipite kimya kimya. Idadavuliwe mpaka UN ikiwezekana!!
 
Naomba nikujibu kwa maelezo ya Jaji Mkuu Nyalali .................................... We are further of the considered opinion that any law which seeks to protect unfree and unfair elections from nullification would be unconstitutional.

Mkuu Ruge nakubaliana na maoni yako na ya majaji pia kwamba katiba haitakiwi kutumika kuwa kichaka cha kuficha wahalifu. Nomba kwanza ninukuu kifungu cha Katiba Ibara 74 (12)

"Hakuna mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza jambo lolote lililotendwa na Tume ya Uchaguzi katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii."

Tatizo bado linabaki, katika mazingira ya kawaida (ya uchakachuaji) tume iko makini kuonesha kuwa inajali haki na uhuru. Ikumbukwe uchakachuaji vituoni na majimboni si kosa la tume as long as forms za mawakala zinaonesha kusainiwa (Makongoro Mahanga kashindaje?). Kitendo cha matokeo kucheleweshwa kwa visingizio vya kuscan forms hakutoi mazingira ya kuonesha "kukiuka katiba" au uhuru bali ni suala la "teknolojia" na "idadi kubwa ya watu waliopiga kura." Mazingira yanatengenezwa kiasi kwamba hutawakamata tume kwa kwenda kinyume na katiba kwa maana ya utawala wa sheria. Kubwa linalofanyika "Chakachueni vituoni, leteni forms zenye matokeo myatakayo, sisi tutaweka vituo vingi na hatutalipa mawakala. Kwa kuwa wapinzani hawana uwezo wa kulipa mawakala wengi, mtapata nafasi ya kuchakachua."

Ukitazama vizuri utagundua arguments za Majaji uliowataja zina mantiki kwa maana ya kuwa katiba haiwezi kulinda uovu, lakini arguments hizi hazitekelezeki kwa kuwa wezi wa kura hawaji wakitangaza "tunakuja kuiba." Janja ni nyingi sana. Suala ni kifungu hicho kuondoka kwa kuwa ndicho kinacholinda wezi kwa kisingizio kwamba "Tukiruhusu watu kupinga Tume ya Uchaguzi tutayumbisha nchi na uchaguzi ni gharama sana. Hivyo vyama vizuie kutamkwa kwa mshindi, ila akishatamkwa hakuna kurudia." Ndiyo maana unaona mshindi anatangazwa leo, kesho anaapishwa. Mlolongo wa kumuondoa Rais madarakani najua unaufahamu ulivyo mrefu na mgumu kwa nchi kama zetu.

Ni rahisi kumuondoa Obama kuliko JK kwa kuwa Democrats na Republican ni nearly 50-50 na wazungu hawana njaa. Bongo je?
 
Mkuu Rugemeleza,

Asante sana kwa kipande cha hukumu ya kesi ambayo umeiweka hapo juu. Mimi ni kilaza wa sheria, nilikuwa ninaomba ufafanuzi kidogo.

Tangu mfumo wa Vyama Vingi ulipoanza, kumekuwa na malalamiko kuhusu Tume ya Uchaguzi kwamba haiko huru, hivyo inaweza kusababisha uchaguzi usiwe huru na wa haki. Pia nikisoma hiyo hukumu hapo juu kuna mahali majaji wanasema kwamba, "We are further of the considered opinion that any law which seeks to protect unfree and unfair elections from nullification would be unconstitutional". Je, hakuna uwezekano wa wana sheria kufungua kesi ili kuilazimisha serikali kufanyia marekebisho ya muundo na/au uteuzi wa Tume ya Uchaguzi ili uchaguzi uwe huru na wa haki?

Nikienda mbali zaidi, ninaona wazi kabisa kwamba kuna conflict of interest kwa watendaji wa Tume ya Uchaguzi kwa kuwa wanateuliwa single handed na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Siasa na pia anaweza kuwa mgombea wa urais. Hiyo conflict of interest ndiyo inawafanya wakati mwingine wawe biased au kutoa matamko ya ajabu.

Pia, wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya majimbo nao wana conflict of interest kwa kuwa ni waajiriwa wa Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI). Mfano, kulikuwa na thread hapa ikisema kwamba matokeo ya Jimbo la Sumbawanga Mjini yalitangazwa baada ya Mheshimiwa Pinda (Sitting PM) alipoenda kwenye kituo cha kutangazia matokeo ya jimbo ambako inasemekana mgombea wa CHADEMA alikuwa anaongoza na mara kibao kikageuka.

Ni hayo tu.
 
Ndugu yangu cha maana hapa ni ushahidi wa kuonyesha jinsi mwenendo mzima wa uchaguzi ulivyofanya uchaguzi usiwe huru na wa haki. Kuna ushahidi kuwa kura zilizotajwa vituoni si zile ambazo Tume imezitaja. Huo ni ushahidi wa nguvu sana. Kuna ushahidi kuwa raslimali za serikali zilitumika kufanyia kampeni za CCM kinyume cha sheria maana yake CCM walikiuka sheria. Kuna ushahidi kuwa wasimamizi wa uchaguzi walitoa matamko ya kuwakandamiza wapinzani na kuwapendelea CCM.

Kuna ushahidi kuwa Tume hakuruhusu Vyama kuwa na wakaguzi na wahakiki wake katika zoezi zima la kukokotoa kura. Hivyo Tume hakuwatendea haki wagombea. Kuna ushahidi kuwa Tume hakukemea vitendo viovu vya magazeti na vyombo vya habari vilivyoendesha kampeni chafu dhidi ya Dr. Slaa. Yote hayo ni lazima yawekwe hadharani ili watu wajue kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki. Hivyo haki ya kwenda mahakamani iko pale pale. Ni hoja yangu kuwa twende huko kuanika mambo hayo yote. Suala la gharama ni kwa nani? Tunazungumzia kuweka misingi mizuri ya kufanya uchaguzi na viongozi wa serikali ni lazima wajue watu hawatakubali tena uchaguzi ufanyike katika mazingira yasiyo ya haki.

Kampeni ya kupigania kubadilishwa katiba ni suala muhimu lakini ni lazima iende sambamba na mapambano ya kisheria ili kuwaadhibu wote waliokiuka matakwa ya Watanzania.
 
Mkuu Rugemeleza,

....... Je, hakuna uwezekano wa wana sheria kufungua kesi ili kuilazimisha serikali kufanyia marekebisho ya muundo na/au uteuzi wa Tume ya Uchaguzi ili uchaguzi uwe huru na wa haki?

Hiyo conflict of interest ndiyo inawafanya wakati mwingine wawe biased au kutoa matamko ya ajabu.

Ni hayo tu.

Kuna kesi ilifunguliwa kabla ya uchaguzi kutaka kifungu kinachozuia kuipinga tume kiondolewe. Nachofahamu hukumu hiyo ilikuwa haijatolewa hadi matokeo ya Urais yanatangazwa.

Conflict of interest haina mjadala. Kama Rais ndiye anateua M/kiti wa tume kwanini asiweke anayemfavour yeye au chama chake? Hili mbona liko wazi. Hivi Dr. Slaa ndo angekuwa amepata kashfa kama ya Chenge au Rostam au Mkapa unadhani wangemwacha?
 
Ndugu yangu cha maana hapa ni ushahidi wa kuonyesha jinsi mwenendo mzima wa uchaguzi ulivyofanya uchaguzi usiwe huru na wa haki. Kuna ushahidi kuwa kura zilizotajwa vituoni si zile ambazo Tume imezitaja. Huo ni ushahidi wa nguvu sana. Kuna ushahidi kuwa raslimali za serikali zilitumika kufanyia kampeni za CCM kinyume cha sheria maana yake CCM walikiuka sheria. Kuna ushahidi kuwa wasimamizi wa uchaguzi walitoa matamko ya kuwakandamiza wapinzani na kuwapendelea CCM.

Kuna ushahidi kuwa Tume hakuruhusu Vyama kuwa na wakaguzi na wahakiki wake katika zoezi zima la kukokotoa kura. Hivyo Tume hakuwatendea haki wagombea. Kuna ushahidi kuwa Tume hakukemea vitendo viovu vya magazeti na vyombo vya habari vilivyoendesha kampeni chafu dhidi ya Dr. Slaa. Yote hayo ni lazima yawekwe hadharani ili watu wajue kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki. Hivyo haki ya kwenda mahakamani iko pale pale. Ni hoja yangu kuwa twende huko kuanika mambo hayo yote. Suala la gharama ni kwa nani? Tunazungumzia kuweka misingi mizuri ya kufanya uchaguzi na viongozi wa serikali ni lazima wajue watu hawatakubali tena uchaguzi ufanyike katika mazingira yasiyo ya haki.

Kampeni ya kupigania kubadilishwa katiba ni suala muhimu lakini ni lazima iende sambamba na mapambano ya kisheria ili kuwaadhibu wote waliokiuka matakwa ya Watanzania.

Ushahidi upo. Nakubali. Sasa niambie, huo ushahidi utaupeleka mahakama gani? Mahakama kuu haina uwezo wa kusikiliza hii kesi. Mahakama ya katiba si kazi yake kusikiliza kesi ya wizi wa kura na matumizi mabaya ya madaraka.
 
Mkuu Rugemeleza,

Asante sana kwa kipande cha hukumu ya kesi ambayo umeiweka hapo juu. Mimi ni kilaza wa sheria, nilikuwa ninaomba ufafanuzi kidogo.

Tangu mfumo wa Vyama Vingi ulipoanza, kumekuwa na malalamiko kuhusu Tume ya Uchaguzi kwamba haiko huru, hivyo inaweza kusababisha uchaguzi usiwe huru na wa haki. Pia nikisoma hiyo hukumu hapo juu kuna mahali majaji wanasema kwamba, "We are further of the considered opinion that any law which seeks to protect unfree and unfair elections from nullification would be unconstitutional". Je, hakuna uwezekano wa wana sheria kufungua kesi ili kuilazimisha serikali kufanyia marekebisho ya muundo na/au uteuzi wa Tume ya Uchaguzi ili uchaguzi uwe huru na wa haki?

Nikienda mbali zaidi, ninaona wazi kabisa kwamba kuna conflict of interest kwa watendaji wa Tume ya Uchaguzi kwa kuwa wanateuliwa single handed na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Siasa na pia anaweza kuwa mgombea wa urais. Hiyo conflict of interest ndiyo inawafanya wakati mwingine wawe biased au kutoa matamko ya ajabu.

Pia, wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya majimbo nao wana conflict of interest kwa kuwa ni waajiriwa wa Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI). Mfano, kulikuwa na thread hapa ikisema kwamba matokeo ya Jimbo la Sumbawanga Mjini yalitangazwa baada ya Mheshimiwa Pinda (Sitting PM) alipoenda kwenye kituo cha kutangazia matokeo ya jimbo ambako inasemekana mgombea wa CHADEMA alikuwa anaongoza na mara kibao kikageuka.

Ni hayo tu.
Inawezekana lakini inahitaji kuwa na mtu ambaye ni mgombea kupinga muundo mzima wa Tume. Lakini nina wasiwasi kwani Mahakama inaweza kusema hilo ni jukumu la Bunge la Katiba kubadilisha Katiba na si jukumu la Mahakama kuamua muundo wa tume hiyo. Mahakama ina uwezo wa kusema kuwa Tume lazima iendeshe uchaguzi ambao ni huru na wa haki lakini si jinsi ambavyo tume hiyo inatakiwa kuwa.

Hapo ndipo ukomo wa sheria. Hili sula la muundo lifanikiwe ni lazima kupigania kubadilishwa kwa katiba ili kuunda Tume ambayo ni huru na hilo ni suala ambalo Watanzania wote lazima tulipiganie kwa nguvu zote kama mtu mmoja mmoja au kupitia jumuia na asasi mbalimbali.

Ni lazima tujenge mazingira na msukumo wa suala hilo kukubalika na kuwa katika ajenda ya kila chama na kwa bahati mbaya hata Wafadhali.
 
Back
Top Bottom