Kutumia mtihani mmoja wa Taifa kupima wanafunzi wote sio sahihi, ni upotofu mkubwa

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
29,555
2,000
Itawaletea shida ya kubaguliwa wanafunzi huko mbele. Syllubus ni moja tu. Labda useme pia kuwa na syllabuses nyingi. Kama ilivyo sasa wale wa intentional schools walivyo na syllabus tofauti na mitihani/watahini tofauti. Localy italeta confusion!

Kama unakubali hoja ya kuwa na syllabus moja kwa nchi, then huwezi kuwa na mitihani zaidi ya mmoja.

Maana lengo la mitihani ni kupima kama kile mwanafunzi anachotakiwa kujua kwa level fulani (syllabus) je anakijua kwa kiwango gani!?

Kama kwa syllabus yetu tunataka mtoto anayemaliza drs 7 ajue kuhesabu na kuandika mpaka 10, huwezi kuwa na vipimo tofauti kwa shule tofauti kwa lengo hilo hilo. Huwezi kupima shule moja kuona kama wanahesabu vizuri mpaka 5 tu na nyingine mpaka 10, halafu wakifuzu wote uwape cheti cha kufuzu darasa la 7. Akija huku kwenye ajira, nianze kumfundisha kuhesabu kuanzia 6-10? Kwa nini nisimchukue ambaye tayari anajua kuhesabu mpaka 10?
umepigilia msumari penyewe
 
  • Thanks
Reactions: SMU

ram

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
8,426
2,000
Maana yake hoja yako ni kuwa Shule za Kidumu mfagio zipewe mitihani miepesi

Sent using Jamii Forums mobile app
Halafu wakifaulu huo mtihani wao waende kusoma wapi? Kwa sababu huko mbele lazima tu watakutana wote hakuna advance au chuo cha aliyetoka shule ya kidumu au aliyetoka kwenye basi la njano
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
29,555
2,000
Mleta mada labda tumuulize pia kuna shuke za private zina Huduma na mazingira mazuri mno ila kila mwaka zinakuwa na division zero tupu kibao na kuwa za mwisho mwisho kitaifa hizo nazo ataziweka kundi gani? Kwa hiyo kigezo anataka kiwe mazingira tu ya kusomea au?
 
Diazepam

Senior Member
Dec 3, 2020
145
500
Kuna wengi sana waliofeli pia huko kwenye vidumu na mfagio na wakakosa fursa ya kuendelea mbele kielimu.

Kwa nchi yetu kuboresha miondombinu itachukua hata miaka 40 na pia wanafunzi wanazidi kuongezeka kila siku. Haya mapendekezo yangu na wengine waliounga hoja hii mkono yanaweza kuanza kutumika hata kesho kwa gharama nafuu kabisa na yakaleta tija kubwa.
Kwa hiyo unashauri kuwe na mitihani hata 10? Yaani kuna mathematics watafanya wale waliosoma mada 2, wale wa 3, wale wa 6 na waliomaliza mada zote? Hii sababu ya kimazingira umeiangalia kwa upande mmoja tu mbona hata wengine wanafeli pia na wanamazingira mazuri?

Kingine, ukweli wa mambo kuhusu ufaulu wa watoto hauishii kwenye mazingira yanayotolewa na serikali mashuleni tu. Kuna mengine mfano wazazi hawawahimizi watoto kujisomea, watoto wako busy na mambo ya mtandao, maadili zero etc.

Muamko wa kielimu ni mdogo hasa hayo maeneo unayolenga, mtoto hana bidii ya kujisomea vitabu shule vipo, hana hata motive ya future yake. Nitakupa mfano sio kwa nia mbaya nina ndugu yangu yeye alipokuwa O level alikuwa anasoma sana na motive yake ilikuwa aje tu kusafiri kwa bus aende akasome mbali sababu hajawahi safiri tangu awe na akili za kujielewa. Motive ni kupanda bus tu, na jamaa ameshapanda hayo mabasi na ameendelea mpakaa huko alikotaka.

Back to topic bado watoto wanahitaji motive nyingi ili kuweza kumaliza hizo topics na wafanye mtihani. Hizo mada sio nyingi kuliko kusema mitihani iwe aina 5 et sababu chitoholi hawajamaliza topic then mwisho wa siku aje kushindana na wale waliomaliza kila kitu.
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
29,555
2,000
Hapana kabisa. Unapelekaje watu chuo kikuu kama hawakumaliza syllabus ya sekondari? Kama kuna uhaba wa walimu na watoto hawajafundishwa ipasavyo, solution kamwe haiwezi kuwa kuwapa mitihani tofauti (rahisi?).

Labda sijapata hoja yako. Katika mfano wangu rahisi wa kufuzu drs 7, unataka tuwe na mitihani miwili? Mmoja unapima kuhesabu mpaka 5 na mwingine unapima mpaka 10? Na uwapeleke form one hao ambao waliishia kuhesabu 5 tu? Hebu nifafanulie vizuri hoja yako kwa huo mfano wangu au mwingine wowote rahisi kabisa.
Yaani umeeleza kwa mfano rahisi mno asipoelewa basi
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
12,825
2,000
Itaje moja tu na mahali ilipo.
Mleta mada labda tumuulize pia kuna shuke za private zina Huduma na mazingira mazuri mno ila kila mwaka zinakuwa na division zero tupu kibao na kuwa za mwisho mwisho kitaifa hizo nazo ataziweka kundi gani? Kwa hiyo kigezo anataka kiwe mazingira tu ya kusomea au?
 
EvilSpirit

JF-Expert Member
Jun 15, 2017
6,438
2,000
Nadhani ndugu mwandishi unamaanisha kama tunavyopimana humu kutokana na tunavyochangia kwenye thread mbalimbali kumpima mtu kutokana na uandishi
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
12,825
2,000
Hata sasa hivi wengi wanaovuka kwenda kidato cha kwanza, cha tano na chuo kikuu wanakuwa hawajamaliza syllabus ila wanatumia njia mbalimbali kupata angala ufaulu wa chini utakaowavusha au kuwafanya wafike vyuo.

Nimeandika kwa kirefu hapo juu kwamba lengo la kuziweka shule katika makundi tofauti sio suala la kumaliza syllabus tu bali ni kutokana na hali pamoja na mazingira mengine mengi na ya muhimu zaidi ya kimasomo ambayo yanaleta utofauti mkubwa kati ya makundi tofauti ya wanafunzi. Syllabus ni kipengele kidogo sana katika hii hoja.
Hapana kabisa. Unapelekaje watu chuo kikuu kama hawakumaliza syllabus ya sekondari? Kama kuna uhaba wa walimu na watoto hawajafundishwa ipasavyo, solution kamwe haiwezi kuwa kuwapa mitihani tofauti (rahisi?).

Labda sijapata hoja yako. Katika mfano wangu rahisi wa kufuzu drs 7, unataka tuwe na mitihani miwili? Mmoja unapima kuhesabu mpaka 5 na mwingine unapima mpaka 10? Na uwapeleke form one hao ambao waliishia kuhesabu 5 tu? Hebu nifafanulie vizuri hoja yako kwa huo mfano wangu au mwingine wowote rahisi kabisa.
 
SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,522
2,000
Hata sasa hivi wengi wanaovuka kwenda kidato cha kwanza, cha tano na chuo kikuu wanakuwa hawajamaliza syllabus ila wanatumia njia mbalimbali kupata angala ufaulu wa chini utakaowavusha au kuwafanya wafike vyuo.

Nimeandika kwa kirefu hapo juu kwamba lengo la kuziweka shule katika makundi tofauti sio suala la kumaliza syllabus tu bali ni kutokana na hali pamoja na mazingira mengine mengi na ya muhimu zaidi ya kimasomo ambayo yanaleta utofauti mkubwa kati ya makundi tofauti ya wanafunzi. Syllabus ni kipengele kidogo sana katika hii hoja.
Kwa nini tunafanya mitihani? Anayetunga mitihani nia yake ni nini? Nini kinamuongoza katika kutunga mtihani? Ukitaja mtihani, huwezi kukwepa kuzungumza syllabus. Tunaposema mtu kamaliza kidato cha nne kwa mfano, kuna mambo tunategemea awe anayajua (ambayo kimsingi yanaongozwa na syllabus).Na ndio hayo pia mtahini (NECTA) anayapima kwa kipimo kimoja.

Sasa hiyo mitihani unayosema iwe tofauti, huo utafauti uwe kwenye nini hasa kama syllabus ni moja? Labda uwe na syllabus tofauti kwa shule tofauti ndipo hasa hoja ya kuwa na mtihani tofauti itasimama. Nje ya hapo, hakuna hoja.

Kwamba wengine wapewe mtihani mgumu na wengine rahisi (kwa scope/syllabus ile ile)? Hii ndio hoja yako hasa? This will be disastrous!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom