Kutumia mtihani mmoja wa Taifa kupima wanafunzi wote sio sahihi, ni upotofu mkubwa

Una hoja ya maingi ila tatizo ni necta, wenzetu Kenya kabla ya kutunga mitihani wanafatilia shule zote kujua wamefundishwa mpaka wapi na wale walio nyuma wanahimizwa kuongeza juhudi halafu wanarudi mara ya pili kukagua, wakishakagua wanatunga mitihani pale wanafunzi walipoishiwa kufundiashwa lakinimpaka necta wamekazania kutunga kwa ajili ya syllabus.
Wakaguzi wa elimu wamekaa maofisini badala ya kufatilia wanafunzi wamefundishwa mpaka wapi
Hii itapelekea uzembe kwa walimu na wanafunzi..!
 
Inategemea aina ya kazi

Kazi routine watu wenye low grade ndio hufaa sana

Zile za kufanya kwa mazoea isizo hitaji matumizi makubwa ya akili.Mfano mtu ana digrii ya chini ukimuweka mfano kuwa cashier ana spidi kubwa sana na anachangamka kuona wateja wanafurahi anapowahudumia kwa spidi na kicheko kichwa linavimba kuwa ona nilipata digrii ya chini lakini ona huku wateja wanavyonithamini!!!! kupata GPA kubwa ndio nini hamna lolote!!!

Kazi hiyo ukimpa mwenye akili zake mwenye GPA kubwa anaona hii kazi ya kijinga sana aweza toa hata barua ya kuacha kazi anataka sehemu ya kutumia akili .Akikaa hapo aweza poromoshea matusi hata wateja kwa kuichoka kazi

Kazi routine zinawafaa wenye vidigrii vya class ya chini nakubaliana na wewe.Lakini kazi inayotaka matumizi makubwa ya ubongo usije chukua mwenye ki GPA cha chini ataanza kelele ohh hii kazi ngumu kazi ya mabosi wananisukumia mimi nifanye!! kichwa kinaanza kupata moto!!! Lakini mwenye GPA kubwa hapo hadi anasikia raha akikutana na challenging job hilo ndio eneo lake la kujidai
No siyo hivyo. Ukifanya personality profiling utawaelewa hawa watu. Unaweza kumkuta mtu amesomea LLB lakini anapenda routine tu...na nimewaona watu wanasema wana MBA - ndugu yangu their thought process iko narrow had utashangaa.

Kumbuka elimu yetu ni academic not competency based - sio watoto wote wanakipaji cha kukariri, na mental condition huwezi kujua ya huyo mwanafunzi wakati wa kufanya mtihani....kwa hiyo waajiri wenye upeo mpana hawaangali sana GPA.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Kutoa kipimo kimoja kwa wanafunzi waliofundishwa vizuri na wale ambao hawajafundishwa kabisa au wamefundishwa katika hali ya uduni sana ni zaidi ya ubaguzi.
Ni uonevu, kujidanganya na ujuha.
Halafu baadaye ashindane na aliyesoma kila kitu. Si mnamtengenezea mazingira magumu ya ushindani. Maana atakuwa na content ndogo.
Ni bora kipimo kiwe kimoja. Kusitokee ubaguzi..!
 
Hii itapelekea uzembe kwa walimu na wanafunzi..!
Hakuna uzembe walioko nyuma inatafutwa sababu baraza linatunga mtihani kwa kile walichofundishwa wanafunzi haiwezekani kutunga mtihani kwa kufata syllabus wakati ahule nyingi hazijamaliza syllabus.
Ndio maana wanafanya kaguzi mara mbili ya kwanza ninkuangalia nq kuhimiza wale walioko nyuma wakati ya pili ni kuangalia wanafunzi wamefundishwa hadi wapi na kutunga mtihani pale walipoishia.
 
Hawa watu wanaopinga hizi system ukiwaambia tutumie system gani ku-grade hawa watoto hawana alternative wanaongea upumbavu mtupu

Yaani yeye anataka watoto wasome,wapite madarasa yote bila mtihani wa aina yeyote

Sasa,dunia hii tuna fani mbali mbali,hawa watoto tutafanya nini kuwa-grade ili tupate hizi competencies?

Jibu lake hawana

Mfumo wa elimu sio perfect

So far ndio alipofika mwanadamu,nyie wenye maono zaidi hebu tupeni njia za kuweza ku-grade hawa wanadamu tujue nani tumpe nini na nani tumpe nini

Sio mnaongea kama ma-gorilla tu

Eti daktari apite kuanzia kindergarten bila mtihani wowote mpaka anakua daktari halafu anakufanyia operation,how on this goddamn hell can you trust this fool to do that on you?

How to we measure competence za hawa watoto kama wameelewa walichofundishwa?

Kwanini you motherfvckers are so scared to be measured kwa kile ulichofundishwa?

Hatusemi hujui vitu vingine,unajua sana,ila hujafundishwa hivyo tunataka upimwe kwa kile ulichofundishwa,ambacho ukifeli tunajua hukikijua sawasawa ndio maana unaandikiwa pale kua ni F ukafanye vile unavyovifahamu sawasawa uachane na hivi ulivyofeli

Yaani hii dunia bwana

Watataka mitihani ifutwe kote,baada ya hapo hata shule zenyewe zifutwe kabisa....yaani mwanadamu hana mwisho kwenye negative progression,mpaka afe
 
Kutoa kipimo kimoja kwa wanafunzi waliofundishwa vizuri na wale ambao hawajafundishwa kabisa au wamefundishwa katika hali ya uduni sana ni zaidi ya ubaguzi.
Ni uonevu, kujidanganya na ujuha.
Sizungumzii ubaguzi wakati wa kusoma. Nasema baada ya kumaliza je taasisi zitawakubali ilhali walichosoma ni kidogo...! Maana yake hawatakuwa competent licha ya kwamba wamefaulu vizuri. Kwa sababu walichosoma si sawa na wale waliosoma wakamaliza syllabus
 
Kumbuka sasa hivi undergraduate degree ni basic maana kila mwanafunzi anapaswa awe nayo katika ulimwengu wa sasa hivi.
mtoto wa maskini hata chuo kikuu ndie anabebwa na bodi ya mikopo
Kigezo kikuu kimojawapo awe kasoma hizo shule za ukwamani au za kayumba!!

Mikopo yote inaishia kwao kwa wasomeshwa private hawapewi !!! Bodi ya mikopo ya kwao yote bado serikali inaendelea kuwabeba!! Yule aliyewapisha kuwa wasome O LEVEL na A LEVEL wanamwadhibhibu kwa nini ulimpisha mtoto wa maskini asome? hatukupi mkopo wa elimu!! Endelea kujilipia!!
 
Hakuna uzembe walioko nyuma inatafutwa sababu baraza linatunga mtihani kwa kile walichofundishwa wanafunzi haiwezekani kutunga mtihani kwa kufata syllabus wakati ahule nyingi hazijamaliza syllabus.
Ndio maana wanafanya kaguzi mara mbili ya kwanza ninkuangalia nq kuhimiza wale walioko nyuma wakati ya pili ni kuangalia wanafunzi wamefundishwa hadi wapi na kutunga mtihani pale walipoishia.
Si mwalimu anasema wanafunzi hawaelewi, hapo anakuwa hayuko limited.
Then yeye anaendelea kurelax na wanafunzi always hawapendi kusoma..! Wanaweza tengeneza ucheleweshaji wa kusudi ili wasimalize tu syllabus
 
Taasisi zetu zinaangalia matokeo ya chuo kikuu tu au Diploma.
Sizungumzii ubaguzi wakati wa kusoma. Nasema baada ya kumaliza je taasisi zitawakubali ilhali walichosoma ni kidogo...! Maana yake hawatakuwa competent licha ya kwamba wamefaulu vizuri. Kwa sababu walichosoma si sawa na wale waliosoma wakamaliza syllabus
 
Bodi ya mikopo haimbebi yoyote, elewa tofauti ya mkopo na msaada. Hiyo ni mikopo ambayo walioichukua wakati wanakatwa 15% ya mishahara yao kila mwezi.Na mkopo wowote huwa unatolewa kwa vigezo, sio pesa za kutupa tu kwa yeyote anayetaka, lazima uonyeshe uhitaji kwa kukidhi vigezo.
mtoto wa maskini hata chuo kikuu ndie anabebwa na bodi ya mikopo
Kigezo kikuu kimojawapo awe kasoma hizo shule za ukwamani au za kayumba!!

Mikopo yote inaishia kwao kwa wasomeshwa private hawapewi !!! Bodi ya mikopo ya kwao yote bado serikali inaendelea kuwabeba!! Yule aliyewapisha kuwa wasome O LEVEL na A LEVEL wanamwadhibhibu kwa nini ulimpisha mtoto wa maskini asome? hatukupi mkopo wa elimu!! Endelea kujilipia!!
 
mtoto wa maskini hata chuo kikuu ndie anabebwa na bodi ya mikopo
Kigezo kikuu kimojawapo awe kasoma hizo shule za ukwamani au za kayumba!!

Mikopo yote inaishia kwao kwa wasomeshwa private hawapewi !!! Bodi ya mikopo ya kwao yote bado serikali inaendelea kuwabeba!! Yule aliyewapisha kuwa wasome O LEVEL na A LEVEL wanamwadhibhibu kwa nini ulimpisha mtoto wa maskini asome? hatukupi mkopo wa elimu!! Endelea kujilipia!!
Ya Bodi ya mikopo ni jambo lingine. Lakini ukifika kwenye ajira ndo unajuta hiyo mikopo na kwamba ukinyimwa huo mkopo kwa njia nyingine inaweza kuwa ni ' blessing in disguise'.

Lakini niwe muwazi hii mikopo imewezesha kwenye ukoo wetu ndugu zangu kupata elimu hiyo ya chuo kikuu.
 
Mazingira wanayosema wanafunzi wa Tanzania yanatofautiana sana. Wapo wanaosoma shule za huduma zote na wale ambao hata dawati la kukaa bado ni tatizo.

Wapo wanaokwenda shule na kidumu, ufagio, kuni, mbole, maji n.k na wenzao ambao hivyo vitu hawavigusi kabisa.

Wapo ambao shule zao zinahakikisha wanafika shuleni kwa wakati kwa magari ya shule na wengine ambao kufika shule ni juu yao wenye, hata wakitumia ungo ni sawa tu mradi wafike shule.

Kuna wanaokula shuleni na wanaoshinda na njaa, kuna wenye vyoo vya kutosha na wengine ambao vyoo ni vya kugombania.

Wapo ambo kumuona mwalimu wa somo ni sawa na kubeti na wale ambao walimu wa masomo wamejaa tele.

Tofauti ni nyingi sana, zaidi ya milioni moja na kwa namna hiyo hakuna mantiki wala sio sahihi kutumia mtihani mmoja kuwapima wanafunzi wote kwa kipimo kimoja.

Serikali ije na namna tofauti, mbadala ya kuwapima wanafunzi hawa wanaotofautiana mazingira ya kusomea kwa kiwango kikubwa sana ili kupata uhalisia wa uelewa wao na kujua jinsi ya kuwaandaa vyema kwa masomo ya juu zaidi. Tuwatendee haki katika elimu watoto wa maskini wanyonge wa nchi hii.
Hili la tofauti za shule ni vigumu ku manage kwa kuwa na tofauti za mitihani.

Dawa pekee, kwa maoni yangu, ni kupunguza ma V8 na anasa nyingine za waserikali na kuelekeza pesa kwenye kuweka mazingira bora ya kutolea elimu kwa shule zote za umma na pia kuongeza idadi ya walimu na motisha. Hii ni rahisi kufanya kuliko kuanza grading za shule na kubagua kwa mitihani.

Tatizo unalolisema, kwa kiasi linaweza kuzingatiwa, mbeleni katika process ya elimu au ajira. Kwa mfano, binafsi nikiona mtoto wa "st Kayumba" huko vijijini kapata div 3, huwa namzingatia au kulingajisha kwa uwezo wa kiakili na aliyepata div 2 kwenye shule "bora". Lakini hili ni very subjective na linahitaji kuangalia viashiria vingine ili kupima uwezo hasa wa mtoto/kijana. Huku kwenye ajira huwa tunawapima kwa aptitude tests na interviews.
 
No siyo hivyo. Ukifanya personality profiling utawaelewa hawa watu. Unaweza kumkuta mtu amesomea LLB lakini anapenda routine tu...na nimewaona watu wanasema wana MBA - ndugu yangu their thought process iko narrow had utashangaa.

Kumbuka elimu yetu ni academic not competency based - sio watoto wote wanakipaji cha kukariri, na mental condition huwezi kujua ya huyo mwanafunzi wakati wa kufanya mtihani....kwa hiyo waajiri wenye upeo mpana hawaangali sana GPA.
Kuna matatizo mengine ni ya mtu binafsi anataka full time awe under tight supervision ili a perform

Vyuoni kunakuwa na tight supervion na deadline nyingi hivyo mtu kama huyo mtaka tight supervision ata perform vizuri chuoni akitoka akaenda eneo relaxed unamkuta unampa kazi muda wote yuko kwenye simu ana chat !! Anatakiwa mazingira anayoenda akutane na ubabe ule ule aliokuwa akikimbizwa chuo kikuu ndio ata perform na kutumia akili yake to the maximum

Ndio maana muhimu sana ukipata mtu mwenye GPA kubwa ukiajiri kile kipindi cha majaribio mtizame na kumsoma vizuri kuwa uchukue approach ipi kama manager ku mu manage ili arudi kwenye performance yake ya GPA kubwa!! Unatakiwa umpelekeshe haraka ukigundua udhaifu ajue kuwa hapo pia hakuna kulala kama ilivyokuwa chuo!! Atarudi kwenye line ila muwahi ajue hiyo ndio culture ya utendaji kazi kati ya wewe na yeye ukikaa sana kama wewe mwanaume yeye mwanamke ukianza kufoka na kutoa deadline aweza kukuzushia kuwa muda wote amekuwa akifanya kazi vizuri ila wewe unamtaka KIMAPENZI akukataa ndio maana unageuka mbogo kwake SASA!! Anataka aendelee ku relax !!!
 
Hili la kuweka tofauti ya shule na kuwa na tofauti za mitihani ndio rahisi zaidi kuliko hayo unayosema ya kupunguza mavietee.

Hayo unayosema ya kupunguza maV8 na kupunguza anasa yamekuwa yakiimbwa tangu karne na karne. Wakitaka kupanga shule katika makundi tofauti mwaka huu wanafunzi nchi nzima watafanya mitihani chini ya huu mfumo.
Hili la tofauti za shule ni vugumu ku manage kwa kuwa na tofauti za mitihani.

Dawa pekee, kwa maoni yangu, ni kupunguza ma V8 na anasa nyingine za waserikali na kuelekeza pesa kwenye kuweka mazingira bora ya kutolea elimu kwa shule zote za umma na pia kuongeza idadi ya walimu na motisha. Hii ni rahisi kufanya kuliko kuanza grading za shule na kubagua kwa mitihani.

Tatizo unalolisema, kwa kiasi linaweza kuzingatiwa, mbeleni katika process ya elimu au ajira. Kwa mfano, binafsi nikiona mtoto wa "st Kayumba" huko vijijini kapata div 3, huwa namzingatia au kulingajisha kwa uwezo wa kiakili na aliyepata div 2 kwenye shule "bora". Lakini hili ni very subjective na linahitaji kuangalia viashiria vingine ili kupima uwezo hasa wa mtoto/kijana. Huku kwenye ajira huwa tunawapima kwa aptitude tests na interviews.
 
Hili la kuweka tofauti ya shule na kuwa na tofauti za mitihani ndio rahisi zaidi kuliko hayo unayosema ya kupunguza mavietee.

Hayo unayosema ya kupunguza maV8 na kupunguza anasa yamekuwa yakiimbwa tangu karne na karne. Wakitaka kupanga shule katika makundi tofauti mwaka huu wanafunzi nchi nzima watafanya mitihani chini ya huu mfumo.
Itawaletea shida ya kubaguliwa wanafunzi huko mbele. Syllabus ni moja tu. Labda useme pia kuwa na syllabuses nyingi. Kama ilivyo sasa wale wa intentional schools walivyo na syllabus tofauti na mitihani/watahini tofauti. Locally italeta confusion!

Kama unakubali hoja ya kuwa na syllabus moja kwa nchi, then huwezi kuwa na mitihani zaidi ya mmoja.

Maana lengo la mitihani ni kupima kama kile mwanafunzi anachotakiwa kujua kwa level fulani (syllabus) je anakijua kwa kiwango gani!?

Kama kwa syllabus yetu tunataka mtoto anayemaliza drs 7 ajue kuhesabu na kuandika mpaka 10, huwezi kuwa na vipimo tofauti kwa shule tofauti kwa lengo hilo hilo. Huwezi kupima shule moja kuona kama wanahesabu vizuri mpaka 5 tu na nyingine mpaka 10, halafu wakifuzu wote uwape cheti cha kufuzu darasa la 7. Akija huku kwenye ajira, nianze kumfundisha kuhesabu kuanzia 6-10? Kwa nini nisimchukue ambaye tayari anajua kuhesabu mpaka 10?
 
Huu mfumo hautaleta shida ya kubaguliwa mbeleni wakimaliza vyuo, jambo la muhimu wafike chuo kikuu.Taasisi nyingi huwa zinaangalia matoke ya chuo kikuu tu katika ajira, ni chache sana huwa zinafuatilia matokeo ya shule za msingi na sekondari.

Hata kwa syllbus moja bado mfumo huu utafaa. Ukichukulia kipengele kimoja tu cha uwiano wa mwalimu kwa idadi ya wanafunzi darasani kuna utofauti mkubwa wa uelewa utatokea katika uwasilishaji na upokeaji kwa wanafunzi walio 90 darasani dhidi ya wenzao walio 30 hata kama wote watafundishwa kwa muda sawa na walimu hawatakosa vipindi. Kwa hiyo pamoja na kuwa wote wamefundishwa syllabus ikaisha wale walio wachache darasani watakuwa na advantage kubwa zaidi ya wale waliorundikana(asilimia kubwa wataweza kuuliza maswali, mwalimu anaweza kujua changamoto zao wote na jinsi ya kuzifanyia kazi kwa mbinu mbalimbali n.k)

vivyo hivyo kwa wenye njaa vs walioshiba, waliopambana na konda asubuhi kufika shule vs wanaolala shuleni na kuamkia darasani, wenye kitabu kila mmoja vs wanaozimana na kipoteza muda wakiandika notes n.k. Hata syllabus ikiwa moja kuna vitu vingine vingi nje ya syllabus vinavyoleta utofauti kati ya shule.
Itawaletea shida ya kubaguliwa wanafunzi huko mbele. Syllubus ni moja tu. Labda useme pia kuwa na syllabuses nyingi. Kama ilivyo sasa wale wa intentional schools walivyo na syllabus tofauti na mitihani/watahini tofauti. Localy italeta confusion!

Kama unakubali hoja ya kuwa na syllabus moja kwa nchi, then huwezi kuwa na mitihani zaidi ya mmoja.

Maana lengo la mitihani ni kupima kama kile mwanafunzi anachotakiwa kujua kwa level fulani (syllabus) je anakijua kwa kiwango gani!?

Kama kwa syllabus yetu tunataka mtoto anayemaliza drs 7 ajue kuhesabu na kuandika mpaka 10, huwezi kuwa na vipimo tofauti kwa shule tofauti kwa lengo hilo hilo.
 
Huu mfumo hautaleta shida ya kubaguliwa mbeleni wakimaliza vyuo, jambo la muhimu wafike chuo kikuu.Taasisi nyingi huwa zinaangalia matoke ya chuo kikuu tu katika ajira, ni chache sana huwa zinafuatilia matokeo ya shule za msingi na sekondari.

Hata kwa syllbus moja bado mfumo huu utafaa. Ukichukulia kipengele kimoja tu cha uwiano wa mwalimu kwa idadi ya wanafunzi darasani kuna utofauti mkubwa wa uelewa utatokea katika uwasilishaji na upokeaji kwa wanafunzi walio 90 darasani dhidi ya wenzao walio 30 hata kama wote watafundishwa kwa muda sawa na walimu hawatakosa vipindi. Kwa hiyo pamoja na kuwa wote wamefundishwa syllabus ikaisha wale walio wachache darasani watakuwa na advantage kubwa zaidi ya wale waliorundikana(asilimia kubwa wataweza kuuliza maswali, mwalimu anaweza kujua changamoto zao wote na jinsi ya kuzifanyia kazi kwa mbinu mbalimbali n.k)

vivyo hivyo kwa wenye njaa vs walioshiba, waliopambana na konda asubuhi kufika shule vs wanaolala shuleni na kuamkia darasani, wenye kitabu kila mmoja vs wanaozimana na kipoteza muda wakiandika notes n.k. Hata syllabus ikiwa moja kuna vitu vingine vingi nje ya syllabus vinavyoleta utofauti kati ya shule.
Hapana kabisa. Unapelekaje watu chuo kikuu kama hawakumaliza syllabus ya sekondari? Kama kuna uhaba wa walimu na watoto hawajafundishwa ipasavyo, solution kamwe haiwezi kuwa kuwapa mitihani tofauti (rahisi?).

Labda sijapata hoja yako. Katika mfano wangu rahisi wa kufuzu drs 7, unataka tuwe na mitihani miwili? Mmoja unapima kuhesabu mpaka 5 na mwingine unapima mpaka 10? Na uwapeleke form one hao ambao waliishia kuhesabu 5 tu? Hebu nifafanulie vizuri hoja yako kwa huo mfano wangu au mwingine wowote rahisi kabisa.
 
Back
Top Bottom