Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,581
- 46,176
Mazingira wanayosema wanafunzi wa Tanzania yanatofautiana sana. Wapo wanaosoma shule za huduma zote na wale ambao hata dawati la kukaa bado ni tatizo.
Wapo wanaokwenda shule na kidumu, ufagio, kuni, mbole, maji n.k na wenzao ambao hivyo vitu hawavigusi kabisa.
Wapo ambao shule zao zinahakikisha wanafika shuleni kwa wakati kwa magari ya shule na wengine ambao kufika shule ni juu yao wenye, hata wakitumia ungo ni sawa tu mradi wafike shule.
Kuna wanaokula shuleni na wanaoshinda na njaa, kuna wenye vyoo vya kutosha na wengine ambao vyoo ni vya kugombania.
Wapo ambo kumuona mwalimu wa somo ni sawa na kubeti na wale ambao walimu wa masomo wamejaa tele.
Tofauti ni nyingi sana, zaidi ya milioni moja na kwa namna hiyo hakuna mantiki wala sio sahihi kutumia mtihani mmoja kuwapima wanafunzi wote kwa kipimo kimoja.
Serikali ije na namna tofauti, mbadala ya kuwapima wanafunzi hawa wanaotofautiana mazingira ya kusomea kwa kiwango kikubwa sana ili kupata uhalisia wa uelewa wao na kujua jinsi ya kuwaandaa vyema kwa masomo ya juu zaidi. Tuwatendee haki katika elimu watoto wa maskini wanyonge wa nchi hii.