Kutumbua majipu na kisa cha Yesu

CK Allan

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
2,781
6,065
Ukisoma kitabu cha luka 16 :1 kwa bahati mbaya nimeshindwa kupest hapa..
Yesu alitoa mfano wa mtu mmoja tajiri aliyekuwa na wakili wake...baadae akapata taarifa kuwa wakili wake huyo haendi sawa sawa ndipo akamuita akamuuliza kuwa " ni habari gani hii ninayosikia juu yako? Toa hesabu ya uwakili wako maana Kuanzia leo hutakuwa wakili wangu tena ! Yule bwana akawaza ( kulima siwezi..kuomba omba siwezi...sina pa kushika..!) Kwahiyo nitafanya kitu....ndipo akatafuta wale wadeni wa bossi wake..akaanza kula nao njama...akawauliza wewe unadaiwa tsh ngap akasema laki 5 akamuambia sasa utadaiwa laki 2.. Mwingine alikuwa akidaiwa billion 1 akasema sasa utadaiwa milion 300.... Huyu bwana alifanya hivi ili akifukuzwa awe na pa kwenda!?


Sasa nirudi kwenye hoja yangu ukiangalia mfano aliotoa Yesu hapo huyo jamaa alifanya makosa matatu:-

1.alisikia...yaani hapa ndio pale unamfukuza mtu halafu baadae anashinda kesi ( maana ulisikia tu..huna ushahidi)

2.Alimpa muda wa kujitetea - kwa siku za leo ni ile nafasi mtu anayopewa ya " kukabidhi ofisi" kumbuka mtu akishafukuzwa halafu akapewa muda wa kukabidhi ofisi lazima ajiwekee mazingira ya kuishi baada ya kazi na ndio hapo utasikia kiongozi mpya akiingia sehemu analalamika ofisi haina hela!

3.hakumsimamia ipasavyo...hapa huyo tajiri hata alikuwa hajui kazi inaendaje na ndio maana hata alipopelekewa hesabu nusu alimsifia!? Wangap walitumbuliwa halafu wakasafishwa kuwa wanaonewa wivu na kikundi fulani.

Naamini kupitia uzi huu Yesu aliona mbali kuhusu suala la kutumbua majipu
 
sijaelewa hoja yako inalenga nini haswa ingawa ni nzuri. labda unadhani liachwe au lisitishwe au litekelezwe kwa kuzingatia vipengele ulivyo ainisha hapa.
 
Ni kweli wawe makini kwenye utumbuaji wa majipu kwani Serikali inaweza kupata hasara kubwa
 
Back
Top Bottom