Kutozingatia vipimo vya utendaji kazi kwa Taasis za umma

1987SANAWA

JF-Expert Member
Nov 29, 2013
387
479
Ofisi za umma/serikali zinatumia OPras kama kipimo cha utendaji kazi ambapo mtumishi anakubaliana na kiongozi wake majukumu atakayotekeleza jambo ambalo ni zuri, mtumishi anaetekeleza majukumu yake anapaswa kupewa motisha mbalimbali kama kupandishwa cheo na motisha zingine, ila cha kusikitisha Vyeo havitolewi kulingana utendaji kazi, na pia hata wenye vyeo wasipotekeleza majukumu yao hawachukuliwi hatua matokeo yake, Ofisi za umma zimekuwa na msaada kidogo sana Kwa wananchi, Huduma ni mbovu na hawajali muda kabisa, mifumo ya kiserikali imetengeneza mabwana na sio watumishi Wa Umma. Uzalishaji kwenye Taasis za umma upo chini sana, Taasisi nyingi zilipaswa kujitegemea na kurejesha mapato serikali kuu mfano; TPDC, TRL,TTCL,TANESCO,NHC,TCRA,mamlaka za maji na nyinginezo.

Mapendekezo yangu;
Kipimo cha utendaji kazi Opras kizingatiwe kwa kuwapandisha watu vyeo wanaostahili na pia wenye vyeo ambao utendaji wao hauridhishi waadabishwe.
Wakuu wa Taasis za umma wapewe malengo yanayopimika kila robo, nusu na mwaka mzima, ambae atashindwa kutekeleza anapigwa chini na mshahara unapunguzwa, changamoto ya sasa hata ukishushwa cheo unaendelea kulipwa mshahara uleule hivyo wakuu wa taasis hawana hofu hata wakitumbuliwa wanakula mshahara wao wa utendaji mkuu
Taasis za umma zijitegemee na kurejesha mapato serikali kuu isipokuwa Taasis chache ambazo haiwezekani kama vile Ofisi ya Rais Utumishi,nk
 
.
JamiiForums1467427807.jpg
 
Back
Top Bottom