Kutozingatia sheria za ulaji wa vyakula na pombe kali sababu ya ugonjwa wa Figo

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
figooooooooooo.jpg


Imeelezwa kuwa kutozingatia sheria za ulaji wa vyakula na matumizi ya pombe kali vimechangia ongezeko kubwa la wagonjwa wa Figo nchini jambo ambalo ni hatari kwa taifa kutokana ugonjwa huo kuwa tatizo kubwa nchini.

Hayo yamesemwa na Dkt. Gabriel Mpunda ambaye ni mganga mkuu mstaafu wa serikali alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kitabu alichokitafsiri kinachoitwa okoa figo yako ambacho kimetafsiriwa kutoka lugha ya kihindi.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa hospitali ya TMJ Tayab Jafferji amesema kitabu hicho ambacho kimetafsiriwa kwa kiswahili kitasaidia wananchi kujifunza kwa urahisi na kujua jinsi ya kujilinda na ugonjwa huu hatari.

Aidha wagonjwa mbalimbali ambao wamehudhuria uzinduzi wa kitabu hicho wamesema itasaidia kurahisisha uelewa miongoni mwa watu kutokana na matumizi ya lugha ya kiswahili ambapo pia wameiomba serikali kuhakikisha nchi nzima wanapata elimu ya kujikinga na ugonjwa huo.


Chanzo: ITV
 
Back
Top Bottom