Kutoweka uzalendo kwa nchi: CCM haiwezi kuepuka lawama

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Kila Taifa ni lazima liwe na maono yake. Kila Taifa ni lazima lijue linapoelekea. Kila Taifa ni lazima liwe na muongozo na Dira. Matumaini ya Taifa lolote huwa mikononi mwa Viongozi wao ndio wanaamua baadae na historia ya Taifa.

Tatizo tulilonalo ni viongozi walikosa ambition kwa Taifa hili. Hao ndio wanakwamisha juhudi za kuleta maendeleo kwa Taifa hili. Wanachukulia madaraka kama ni sehemu kupata pride ya uongozi na nafasi ya kula lakini sio kuleta mabadiliko kwa watu wa Taifa hili. Hilo ndilo Tatizo tulilonalo.

Viongozi wetu wameridhika na hali iliyopo. Mimi binafsi ningependa tutafakari ni jinsi gani tutalitoa Taifa hili kutoka hapa lilipo.Changamoto hii ya kimawazo ni lazima iwepo kwenye kila kichwa cha mtazania.

Nimeandika mawazo yangu mengi kuongelea jinsi gani tunaweza kuliondoa Taifa hili kutoka hapa lilipo na ninaendelea kutafakari ili kupata majibu sahihi kwa matatizo yetu. Natambua Taifa hili litajengwa na sisi wenyewe kwa nguvu zetu pamoja na akili zetu.

Kitu cha muhimu ni kwamba ni lazima tuunganishe nguvu zetu kukabiliana na changamoto tulizo nazo kama Taifa. Ni lazima tuangalie upya siasa zetu ziwe ni za kujenga nchi na sio siasa maslahi binafsi. Embu turudishe akili zetu pamoja tutafakari kuhusu mustakabali wa nchi hii.

Nchi hii itajengwa na watu wanaotafakari na italindwa na watu wanaotafakari. Kitu gani kinasababisha kuendelea kuwa maskini kama sio tatizo letu la kukataa kuwa wamoja ili tutafakari kwa pamoja matatizo yanayo tukabili? Kuna vitu ambavyo ni muhimu kutafakri ili kuleta nchi yetu katika mstari ulionyooka.

Sitachoka kuwalaumu watawala waliopo kwa kushindwa kuleta utawala wa haki na kusababisha disorder katika jamii yetu. kuruhusu ufisadi na wizi na kusababisha umoja wa Taifa hili kumomonyoka kisha taifa kuwa la watu wabinafsi, la watu wanajifikiria wenyewe na sio baadae yetu.

Ni ukweli usiopingika kwamba CCM wameshindwa kuongoza Taifa hili kuelekea kwenye tija. Nchi inaendelea kuwa tegemezi kwa wahisani na ndoto yetu ya kuwa Taifa lenye kujitegemea haimo miongoni mwa viongozi. Tumetengeneza Taifa la watu wanaoamini katika misaada na sio katika juhudi zetu wenyewe ili kujiletea maendeleo.

Umoja wetu umepotea hili ni lazima tuwalaumu CCM kwa kuondosha umoja na uzalendo wa nchi. Dhambi hii haiwezi kuwatoka. Wameshindwa kuongoza nchi katika utawala wa sheria na maadili kila kitu kimevurugika.

Matumaini ya Taifa hili yamemomonyoka watu wamekata tamaa juu ya maisha na juu ya baadae ya Taifa letu. Viongozi wa CCM , taifa linaharibika wao wanaendelea kustarahe. Taifa limekosa dira sababu ya uongozi wao mbovu.

Hakuna kitu kingine kilichosababisha Taifa hili kuyumba na kukosa mwelekeo zaidi ya uongozi mbovu wa CCM hili halina ubishi. Mtu yeyote mwenye macho anaona. Hili liko dhahiri.

Taifa hili linahitaji mwelekeo na Dira. CCM wameshindwa kuonyesha uongozi katika kila nyanja. Hata kuwapa matumaini watu wa Taifa hili wameshindwa. Hili liko dhahiri hata ukipita barabarani na kuangalia nyuso za watu, hakuna matumaini.

Kuna kutoridhika kwa watu juu ya CCM na uongozi wake, wameshindwa kukidhi matarajio ya wananchi ya Elimu bora, huduma bora za afya na kuleta umoja wa watu wa Taifa hili. Hakuna order makazini watu wamekuwa wezi, wananchi maskini wanateseka.

Watu wowote pale duniani sehemu yeyote ile wana haki ya kuitoa serikali yeyote isiyokidhi matarajio ya watu na kuiweka serikali nyingine itakayoleta tija na matumaini kwa watu.

Na ikiwa serikali yeyoye inawazuia watu wenye kiu ya kuleta maendeleo yao wenyewe kwa ufisadi na wizi watu wao wana haki ya kuiondoa serikali hiyo, serikali ni lazima iwajibike kwa watu wake na si vinginevyo, ni lazima itoe huduma kwa watu wake na si vinginevyo. Kwahiyo watu wakiona serikali imeshindwa kutoa majibu kwa matatizo yao wana haki ya kuitoa serikali hiyo.

Hii ni haki ya kimsingi kabisa kwa raia wowote huru. Watu wa TAIFA hili wasikubali uhuru wao uwekwe rehani na wezi. Taasisi zote zilizoundwa katika Taifa hili ni kwaajili ya kuhudumia wananchi ni taasisi zao, wananchi wana haki nazo. Wana uhuru wa kuhoji uendeshaji wake.

Wana haki ya kupewa majibu sahihi wanapohoji. Wana haki ya kuwaadabisha viongozi wao kama hawako sawasawa. Nguvu hii iko mikononi mwao.

Msipo kemea na kuwaadabisha mapema viongozi mafisadi uhuru wenu utapokonywa na baadae ya Taifa hili itakuwa gizani. Hatua ya kwanza kwa serikali yeyote kuwa ya kiimla ni pale inapokuwa ya kifisadi ni lazima itaanza kuua tu raia wake.

Itawafanya raia watwana. Uhuru wao utapotea. Utawala wowote wa ukandamizaji unaanzia kwenye ufisadi. Kamwe hatutaweza kujenga TAIFA hili kwa siasa za ulaghai hata kidogo. Hatutaweza kujenga Taifa hili katika misingi ya ubinafsi bali katika nguvu ya umoja.

Tunahitaji viongozi wakweli na wazalendo ili kuongoza Taifa hili. Viongozi wenye msimamo watakaoleta dira katika Taifa hili. Tunahitaji viongozi wanaojua wanasimamia nini. Ndipo Taifa hili litakapo pata mwelekeo na matumaini kurudi kwa watanzania. Ni hili tumaini tu litakalo tupa nguvu ya kufanya kazi na kulitumikia Taifa letu.

Wengi wetu matumaini ya Taifa hili kukua yamepotea au kupungua kutokana na viongozi waliopo. Ndoto ya Taifa lazima inyanyuke upya na kutambua kwamba Taifa hili linauwezo wa kukua na kuwa Taifa kubwa kama mengine. Viongozi ambao wamekosa nguvu na courage ya kuliondoa Taifa hili kutoka hapa lilipo ni lazima waondolewa na tuingize nguvu mpya. Ni lazima tujenge elimu bora yenye misingi imara itakayoleta mageuzi katika Taifa hili, ni lazima tujenge uzalendo kwa watu wetu. Hii misingi yote hii CCM wameivunja. Akili zao ziko kwenye kuuibia nchi. Sio umoja wa watu wa Taifa hili wala maendeleo yake.

Kampeni ya kuiondoa CCM madarakani lazima iwe ''reasonable''. Wananchi lazima waelezwe matatizo yaliyosababishwa na CCM na uwezekano wa Taifa hili kubadilika na kuwa bora zaidi bila ya CCM Kuwepo madarakani. Wananchi lazima waambiwe aina ya Taifa tutakalolijenga baada ya kuiondoa CCM lazima wajengewe matumaini ya maisha.

Inaonekana CCM wameshindwa kabisa ku reform chama chao. wangekuwa na hamu ya ku reform chama chao wangemtoa mwenyekiti wa chama chao ambaye nae pia amesemwa sana katika tuhuma mbali mbali lakini pia ameshindwa kukileta chama chake pamoja kuwa chenye nidhamu na maadili. Kwa kukosa mwelekeo kwa CCM na nchi pia imekosa mwelekeo kama Baba wa Taifa alivyosema bila CCM imara nchi yetu itayumba.

Ni lazima tuwe serious katika masuala ya nchi. Ni lazima tuwe serious na ujenzi wa vyama vya kisiasa imara kwakuwa viongozi wetu hutoka humo. Tukiwa na vyama vya siasa ambavyo sio madhubuti nchi yetu itayumba. Ni lazima tujenge vyama vyetu vya siasa katika uzalendo na maadili. Katika masuala ya nchi tusioneane huruma wala kucheka na mtu. Wananchi wana haki ya kuwadhibiti wabunge na serikali yao kwakuwa wao ni watumishi wao na si vinginevyo.

Matatizo yote ya elimu ambayo haijajengwa katika misingi ya kizalendo ambayo itawafanya vijana walitumikie taifa lao, na matatizo mengine ya kiuchumi na kijamii CCM, haiwezi kuepuka lawama kwa nchi yetu kukukosa mwelekeo na kukosa ORDER. Wameshindwa kuonyesha uongozi. Uamuzi ni wa wananchi kuona hali iliyopo na kuchukua hatua.

Kama nilivyosema hatu ya kwanza kwa Taifa lolote kuendelea ni pale raia wanapobadilisha fikra zao kutoka kwenye ubinafsi kuja kwenye Utaifa na uzalendo, na kuijenga nchi yetu kwa pamoja Tofali baada ya tofali.

Katika matumaini haya ya Taifa la watu wamoja na wenye nia moja ni lazima tuishi, tutembee na tukuzwe katika fikra hizi, ya kwamba tunauwezo wa kujenga Taifa hili na kuwa kubwa, na ya kwamba funguo za maendeleo ya Taifa hili ziko mikononi mwetu ni wajibu wetu kufungua au kufunga mlango wa maendeleo. Ni lazima tuamini hivi ama sivyo tutakuwa hatuna nguvu ya kulijenga Taifa hili na ni wajibu wetu kuwekeza nguvu zetu na akili zetu katika kujenga Taifa hili.

Naliona Taifa hili katika macho ya uwezekano, naona tija, Taifa hili linauwezo wa kuwa kama Taifa lolote kubwa ikiwa viongozi na wananchi wakiwa wamoja katika kuleta maendeleo yao wenyewe. Ikiwa tutajenga vyama vyetu vya kisiasa katika maadili na uzalendo. Katika matumaini haya ni lazima tuishi.
 
UZALENDO NA MAADILI YA TAIFA

UTANGULIZI.


UZALENDO ni ile hali ya mtu kuipenda na kuithamini nchi yake na kuweka maslahi ya taifa lake mbele. Uzalendo ni neno dogo lakini maana inayobebwa na neno uzalendo ni kubwa.

Elimu ya uzalendo ni elimu ambayo imekosekana kwenye jamii yetu. Hili linatokana na watu kutofundishwa kuipenda nchi yao.

Upungufu huo ndio ambao hupelekea watu mbalimbali katika jamii kutenda mambo ambayo hushangaza watu na kuacha wengi katika mfadhaiko wa kujiuliza kama huyu mtu anaipenda nchi yake ama la.


Kuna vitendo kama vya utoaji rushwa, upokeaji rushwa, upoteaji wa tamaduni (kutothamini kabila lako na chanzo chake), kutojiamini kama Mtanzania kwamba wewe ni bora kama wengine, wivu wa maendeleo uliyojikita kwa Mtanzania mwenzako na sio kwa mtu wa taifa lingine, kutothamini cha kwako na kutukuza cha mwenzako na kutojua ya kwamba utunzaji wa maslahi ya taifa lako ni jukumu langu na lako.

Uzalendo hujengwa na sisi wenyewe
Ujenzi wa uzalendo huanza tangu elimu ya msingi, mfano; enzi za siku za nyuma wanafunzi wa shule kuanzia za msingi na sekondari kabla ya kuingia darasani walisimama mstalini na kuimba mwimbo wa Taifa wakati kilanja akipandisha bendera ya Taifa. Baada ya hapo ulifuatia ukaguzi wa usafi ambapo bendi ya shule ilipiga wimbo wa "Tanzania nakupenda kwa moyo wote".

Aidha, jioni kabla ya kuondoka shule wanafunzi walipanga mstari tena kuteremsha bendera. Wakati huo bendi ilipiga wimbo wa "Tazama ramani utaona nchi nzuri..." kila mwanafunzi aliimba wimbo huo kwa furaha na matumaini makubwa ya maisha bora yaliyoko mbele yake. Matumaini ya kuondokana na umaskini na kufanikiwa kimaisha. Kwa ufupi vijana walifundishwa kuipenda nchi yao, kujivunia, kuilinda na kuitetea.

Mambo yamebadilika sana kwani siku za nyuma salamu za kuiponda rushwa zilikuwa ni hadharani kama vile; "Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa...Shikamoo mwalimu" leo hii wimbo unaoimbwa katika mashule ni ule wa "Kutesa kwa zamu..." yaani ukipata nafasi ya kazi sehemu unayoweza kula rushwa, basi kula rushwa na iba sana kabla hujaondolewa..."

Muda sasa umefika kuanza kuwafundisha watoto wetu uzalendo. Kuwafundisha kwa moyo wa dhati ili watakapokuwa watu wazima waendelee kulipenda, kulilinda na kulitetea Taifa letu. Binafsi naamini sana maneno yaliyonenwa katika kitabu kitakatifu (Biblia) kwamba "Mlee mwanao katika njia ipasayo, naye hataiacha hata atakapokuwa mzee." (Methali 22:6).

Ni dhahiri kuwa tusipowafundisha watoto wetu kuishi kwa maadili yafaayo, kamwe hatutapaswa kuwalaumu kwa lolote.


Mabadiliko huanza na mtu mmoja au kundi dogo la watu na wengine kujiunga, na baadaye tutakuwa na taifa tulilokusudia. Mambo ya msingi tusikasirike tunapokosolewa ni kitu kizuri sana kwa maendeleo ya nchi ndiyo maana blogs na vyombo vingine vya habari vina kazi ya ziada kuwaelimisha na kuwataarifu watanzania (inform public) nini kinaendelea ndani ya nchi yao.


MSINGI WA MAADILI MEMA YA TAIFA

Suala la maadili limekuwa likivisumbua vichwa vya watu wengi tangu karne nyingi zilizopita kabla hata ya kuzaliwa kwa Masiha.

Kwa mfano msomi mmoja wa Kigiriki aliwahi kusema katika mwaka 560 B.C. kuwa mfanyabiashara anafanya vizuri kwa kukubali kupata hasara kuliko kupata faida haramu.

Sababu yake ni kwamba, hasara inaweza kuuma kwa muda mfupi,lakini faida haramu inauma milele. Hata wafanyabiashara wa leo nao bado wanakabiliwa na ukweli huu.
Kutokana na umuhimu wa uzalendo na maadili, kila taifa linapaswa kujitengenezea maadili yake, kisha kila mwanainchi wa nchi hiyo anapaswa kuyafuata maadili hayo.

Nchini Tanzania, karibu kila kabila lina maadili yake, lakini maadili ya taifa hili yaliwekwa rasmi na waasisi wa taifa hili wakiongozwa na Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Nyerere na kutolewa kwa wanainchi kwa mara ya kwanza kama ahadi za TANU, na baadaye ahadi hizi zilirithiwa na Chama Cha Mapinduzi.

Ahadi hizo ni nane nazo ni:


1.
Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.

2. Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote.

3. Nitajitolea nafsi yangu kuondoa ujinga, umaskini na maradhi.

4. Rushwa ni adui wa haki,sitapokea wala kutoa rushwa.

5. Cheo ni dhamana sitakitumikia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.

6. Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote.

7. Nitashirikiana na wenzangu wote kuijenga nchi yangu.

8. Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.

Kama anavyoainisha Kaduma,katika kitabu chake, Maadili ya Taifa na Hatima ya Tanzania, kwa ujumla wake ahadi hizi zinalenga kumuandaa Mtanzania ili awe mtu mwenye upendo, mwaminifu na mtiifu, awe mtumishi bora wa umma, ajielimishe kwa bidii na kisha atumie elimu hiyo ili alete maendeleo kwa taifa zima.

Awe mkweli na muwazi, akatae kutoa wala kupokea rushwa, apambane kwa bidii zake zote na maadui watatu wa taifa hili yaani, Ujinga, Umaskini na Maradhi.
Ingawa uzalendo na maadili kama haya ni muhimu kwa taifa lolote lile,lakini ni dhahiri kwamba maadili haya ni muhimu zaidi kwa taifa changa kama letu.

Hata hivyo, ingawa muda mchache sana umepita tangu Baba wa Taifa afariki dunia, tayari tumeanza kushuhudia mmomonyoko wa baadhi ya maadili haya. Nchi yetu imepata matatizo kwa sababu Watanzania hatujawa waaminifu katika kutekeleza ahadi ya nane, yaani nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.

Watanzania wengi na hata baadhi ya viongozi hawako hivyo. Mtu huwezi kuukemea uovu kama wewe wenyewe si mkweli maana unachelea usije ukanyooshewa kidole.


NDUGU ZANGU WATANZANIA HEBU KILAMTU AJITATHIMINI YEYE MWENYEWE NA AKILI KAMAKWELI ANAFANYA KAMA ILIVYOHAINISHWA HAPO JUU.
 
Kwanza namshukuru Mungu kwa kunijalia uzima mimi na wanajamvi wenzangu hapa JF.

Tunaelekea kumaliza mwaka sasa (2012) ambapo Mhe. Rais Kikwete aliunda upya baraza la mawaziri (hatimaye ameunda mabaraza manne ndani ya miaka 7) kutokana na utendajl mbovu.

>>Hoja yangu ni juu ya viongozi kuwalaumu wananchi haswa wapinzani wakitaka wawe wazalendo kwa kukubali yanayotendwa na serikali.Mimi sikubaliani kwa sababu kuu mbili:

1.Serikali ya ccm siyo shirikishi kwa wananchi, mikataba mingi kuhusu madini,gas na uwindaji inafanyika kwa siri.Wawekezaji kwenye URANIUM wamepewa leseni,wangapi wanajua?

2.Serikali ya ccm haijifunzi kwa makosa yake yenyewe,kiukweli ukienda Geita,Shinyanga au Mererani kwenye TANZANITE huwezi kuona ubora wa huduma za kijamii na rasilimali zilizopo,je mtawaambia nini Mtwara?

Kumbukeni..."Patriotism is supporting your country all the time,and your government when it deserves it (Mark Twain)" Does our government deserves?
 
Mungu wangu! Wamekubaliwa kuchimba URANIUM ktk nchi ya Wajinga kama hii! Tujiandae na madhara Makubwa, nchi za wenyeakili na pesa madhara yake wanashindwa kuyadhibiti, itakuwaje kwetu? Wamehongwa sh ngapi?
 
Kila kitu chenye manufaa kwa taifa wanakifanya bila kuwashirikisha, commission ya Nuclear Tanzania ilimwambia Naibu Waziri J.Makamba juu ya uhaba wa fedha na vifaa vya kufanyia utafiti lakini alisema budget ijayo watawatengea fedha zaidi.

Suala ni kwamba kabla ya Uranium, ni nini hatma yetu kwenye dhahabu, Almasi, Nikel, Tanzanite na makaa ya mawe?
 
Katika umri(51) wa taifa letu la Tanzania ,uzalendo miongoni mwa watanzania umeshuka sana kiasi cha kutia ofu ktk jamii nzima,kwani wale waliopewa wajibu wa kitaifa au nafasi ktk Serikali wanatumia nafasi hizo kwa ajili yao na watoto wao na familia zao.

Wanachuma mali za taifa kwa kujilimbikizia mali kwaajili yao na familia na marafiki wao.

Kama Mtanzania naona wajibu wa kutengeneza uzarendo na maadili ya Taifa ufundishwa aidha mashuleni ,ktk jamii au miongoni mwa makudi ya kijamii.

Je, katika hili la kushuka kwa uzalendo sijui nani wa kulaumiwa kati ya jamii yenyewe, Serikali au mfumo wa siasa?
 
Heri ya mwaka mpya 2013 ndugu watanzania wenzangu. Ombi langu kwenu nyote katika kuupokea mwaka mpya tutafakari namna ya kurejesha uzalendo wetu kwa taifa. Enzi hizo za miaka ya sabini yalifanyika yafuatayo;
  1. VIONGOZI WAKUU WALISHIRIKI KAZI ZA KILIMO VIJIJINI, YAANI WAKUU WA MIKOA, MAWAZIRI NA RAIS
  2. VIONGOZI WALIFANYA ZIARA NYINGI VIJIJINI KUHIMIZA MAENDELEO.
  3. WANAFUNZI WALIJIFUNZA KAZI ZA MIKONO KWA VITENDO, YAANI KILIMO, UFUGAJI, UFUNDI NA MAPISHI
  4. WALIMU WALITEMBELEA WANAFUNZI NYUMBANI KWAO KUJUA MAZINGIRA WANAYOISHI
  5. HOTUBA ZA VIONGOZI ZILIJAA MATUMAINI YA MAISHA BORA NA SIYO KUKATISHA TAMAA
  6. WAKULIMA NA WAFANYAKAZI WALIJITUMA KAZINI BILA MANUNG'UNIKO
  7. MAZAO YA BIASHARA KAMA VILE KOROSHO YALINUNULIWA KWA WAKATI NA KWA BEI NZURI
  8. VIONGOZI HAWAKUJILIMBIKIZIA MALI WALA WATU WAO WA KARIBU.
  9. ARDHI HAIKUUZWA KWA WAGENI NA KUSABABISHA MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI.
  10. CHAGUZI ZA VIONGOZI HAMA AZIKUTUMIA MUDA MWINGI AU GHARAMA KUBWA.
  11. HAWAKUWEPO WATOTO WA MITAANI.
  12. WATOTO WALIWAHESHIMU WAKUBWA NA MAVAZI YAO YA HESHIMA.
  13. UPENDELEO KATIKA UTEUZI NA AJIRA HAUKUWEPO KABISA.
  14. WANANCHI WALIJITOLEA KWA HALI NA MALI KWA AJILI YA NCHI YAO. MFANO VITA VYA KAGERA NA UJENZI WA MAKAO MAKUU DODOMA.
  15. VIONGOZI WALITUMIKIA WANANCHI KWA HALI NA MALI
NAWAOMBA VIJANA WENZANGU WA MIAKA YA SABINI ONGEZENI NILIYOACHA KWA FAIDA YA VIJANA WA SASA.
 
Kwa muda mrefu nimekuwa kimya nikifuatilia threads mbalimbali ndani ya JF. Zipo zinazosisimua na kutoa mafundisho kwa watanzania wana, JF na wengineo duniani.

Wapo ambao ni Watanzania kwa kuwaona kwa macho lakini hatuko pamoja kiuzalendo. Nitatoa mfano wa mmoja tu ambaye alifikia kutamuka kuwa "Ni heri kwenda kuishi nje ya Tanzania kuliko kukaa kwenye nchi yenye rsilimali nyingi iliyojaa ufisadi".

Hapa nashindwa kumwelewa kwani mtanzania mmoja akianza mwenyewe kuchakatua/process maliasili hizo ndiyo mwendelezo wa mtanzania wa pili, wa tatu , wanne na wengine zaidi hadi Watanzania wengi wanafanikiwa.

Nashawishi Watanzania tuwe na uzalendo wa kutaka kuendeleza nchi yetu badala ya kutamani kukimbilia nchi zingine. Kwenye mambo ya msingi tushikamane kama wanamtwara.

Tusiruhusu nyoyo zetu kutawaliwa na mawazo kutoka nje yenye lengo la kuendeleza ukoloni mamboleo, ukoloniutandawazi, ukoloniNGOS, ukoloniSIASA na ukoloni mwingineo.
 
Watanzania ni wazalendo sana. Lakini wakti mwingine wanakatishwa tamaa na walioko madarakani.

Jamani tunaishi kwa uhuru na tunapendana. Kila nchi ina matatizo yake. Sisi tuna tatizo kubwa moja tu la jinsi ya kutumia raslimali zetu vizuri
 
Ninaomba kuhoji wadau wenzangu kwa nini uzalendo nchini kwetu umeshuka sana? Habu tutafute kiini cha tatizo ili tuweze kupendekeza njia za kuikomboa nchi yetu.
 
Kisu kile kinachokata na kutawanya kabisa misingi imara ya uzalendo ni UFISADI ULITUKUKA, U-SISI na ushikaji katika yale yalio ya pamoja kitaifa.
 
Ninaomba kuhoji wadau wenzangu kwa nini uzalendo nchini kwetu umeshuka sana?
Habu tutafute kiini cha tatizo ili tuweze kupendekeza njia za kuikomboa nchi yetu.
kaka yyangu lema tena katibu wacdm mkoa wa Kilimanjaro CDM unafanya nini kama bado tu hujagundua sababu ya uzalendo nchi hii kwisha, kazi ya chadema ni nini?

Tumejiunga CHADEMA ili kurudisha Utu wa Mtanzania. Kitu ambacho ndo kimepotza uzalendo. Kaka hama hujui kukosa uzalendo ni ugonjwa unaoambukiza. na Source ya Ugonjwa huu ni viongozi wa CCM wanatuambukiza sisi watanzania.

kinga ya ugonjwa huu ni kujiunga na CDM pekee sasa unantia mashaka ndugu
 
Basil Lema,

mazingira na maisha ya wananchi wa SAME yanatishiwa na uchimbaji wa bauxite katika msitu wa SHENGENA. tunakuomba ndugu katibu wa chama ulete ujumbe wa chama katika kata ya Chome ili muweze kusikiliza kilio cha wananchi wa Same.

Tunakuomba ndugu katibu uliwasilishe suala hili kwa tume ya wabunge wa Chadema ili waweze kuwasilisha hoja binafsi bungeni uchimbaji wa bauxite usitishe ili kuweza kuhifadhi maisha na uchumi wa wilaya ya Same.

Tunaomba CHADEMA mtuunge mkono katika kuwasilisha kilio cha wananchi kwa mabalozi wa nchi za nje walioko Tanzania, vyombo vya fedha vya kimataifa, Umoja wa mataifa na taasisi zake, pamoja na taasisi za mazingira za ndani na nchi ya nje.

TUNAWAOMBA CHADEMA MUINGALIE WILAYA YA SAME KWA JICHO LA UPENDO. WANANCHI WA SAME TUNAUMIZWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA KATIKA WILAYA YETU.

nakala: Edwin Mtei, Dr.W.Slaa, Zitto, MTENGETI, Molemo, Kitila Mkumbo, John Mnyika, Mwita Maranya
 
Last edited by a moderator:
Hizi nyimbo za uzalendo chini ya maccm ni ndoto za mchana. Ndo maana hata tra wameachana na mambo ya kukusanyia kodi hazina badala yake wanakusanyia kwenye matumbo yao. Walishtuka baada ya kuona kuna watu wakiona hazina imejaa wanachanganyikiwa na kuwa wehu.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom