Kutowajibika kwa Marekani nchini Afghanistan kwaleta changamoto kubwa ya kibinadamu

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG31N1234976600.jpg
Muda uliowekwa na Rais Joe Biden wa Marekani kuondoa majeshi kutoka Iraq umepita, huu ni muda ambao wamarekani wengi walikuwa wakiusubiria. Kwani kwa muda wa miaka 20, wamarekani wamekuwa wakijiuliza ni kwanini majeshi ya Marekani yanaendelea kuwepo Afghanistan? Wazazi wa wanajeshi waliokuwa wanauawa au kujeruhiwa nchini humo, walikuwa wanajiuliza ni kwanini watoto wao wanaendelea kufa na kujeruhiwa? Kilio hiki kiliendelea kwa muda mrefu hadi rais Joe Biden alipoamua kutangaza tarehe ya kuondoka kwa jeshi la Marekani na majeshi ya NATO nchini Afghanistan.

Kisingizio cha Marekani kutuma jeshi nchini Afghanistan kilikuwa ni kumsaka Osama Bin Laden, waliyemtaja kuwa kinara wa shambulizi la kigaidi la Septemba 1. Uamuzi huo wa Marekani ulivumiliwa na jumuiya ya kimataifa, kwa kuwa karibu kila mtu aliwaonea huruma wamarekani kutokana na msiba wa shambulizi hilo, na dunia ilijia kuwa ugaidi si jambo la kuchekea.

Lakini baada ya Marekani kutuma jeshi lake nchini Afghanistan, walichofanya kilikuwa ni zaidi ya kumsaka Bin Laden. Mauaji ya raia yalikuwa yakifanyika, ukatili wa kila aina ulikuwa ukifanyika hata wakati mmoja ilizuka kashfa ya gereza la Abu Gharib ambayo iliwafanya hata wamarekani wenyewe kujisikia kichefuchefu. Hata hivyo baadhi waliendelea kuvumilia uwepo wa jeshi la Marekani wakiamini kuwa linafanya kile lilichoenda kukifanya. Lakini polepole ilianza kujulikana kuwa Marekani haikuwa Afghanistan kwa malengo ya kupambana na ugaidi, wala kumsaka Bin Laden.

Kwanza Osama Bin Laden aliuawa mwezi Mei mwaka 2011 nchini Pakistan, kama kweli uwepo wake ulikuwa ni kumsaka Bin Laden basi lingeondoka baada ya kumuua. Lakini jeshi la Marekani liliendelea kuwepo nchini humo kwa miaka 10 zaidi, na katika kipindi chote hicho kisingizio kilibadilika na kuwa kupambana na makundi yenye msimamo mkali, na kulipa uwezo jeshi la Afghanistan liweze kulinda nchi baada ya Marekani kuondoka. Lakini ajabu ni kuwa hata kabla ya Marekani kuondoa jeshi lake, Taliban walitwaa udhibiti wa mji mmoja baada ya mwingine karibu bila kiziuizi chochote. Sijui kama ni kweli Marekani lilikuwa inaliongezea uwezo jeshi la Afghanistan.

Pili, tukikumbuka kipindi kabla ya Afghanistan kuvamiwa na Marekani, nchi hiyo ilikuwa na changamoto zake, lakini baada ya Marekani kuondoa jeshi lake inaonekana kuwa changamoto hizo zimeongezeka. Makundi yanayotajwa kuwa na msimamo mkali yameongezeka, na uwezo wake wa kufanya mashambulizi unaonekana kuwa mkubwa zaidi. Mfano mzuri ni shambulizi lililosababisha vifo vya wanajeshi 13 wa Marekani na raia zaidi ya 90 wa Afghanistan. Kama kweli Marekani ilikuwa inafanya kazi ya kuyatokomea makundi hayo katika kipindi cha baada ya Bin Laden kuuawa, inakuwaje makundi hayo yanaibuka ghafla na kuwa na nguvu kubwa ya kufanya mashambulizi, hata kuwalenga wanajeshi hodari wa Marekani?

Tatu, wengi watakumbuka kuwa kabla ya Afghanistan kuvamiwa na Marekani ilikuwa chini ya utawala wa Taliban. Ingawa baadhi ya watu walilalamikia utawala wa Taliban kwa kufuata msimamo mkali na kutawala nchi kwa sheria za kiislamu, kimsingi jamii ya nchi hiyo ilikuwa na utulivu. Mambo ambayo ni kinyume na maadili yalikuwa nadra. Baada ya jeshi la Marekani kuondoka, na baada ya Taliban kuingia mijini, baadhi ya watu walisikika kufurahia kurudi kwa Taliban wakisema matukio ya uhalifu yaliyoshamiri wakati wa ukaliaji wa Marekani na majeshi mengine ya kigeni sasa yatakomeshwa.

Inawezekana ni kweli kuwa Rais Joe Biden ametumia busara kufikia uamuzi wa kuondoa jeshi la Marekani. Sababu kubwa aliyosema ni kuwa Marekani imetumia dola za kimarekani Trilioni 1 kwenye vita ambayo mwisho wake hauonekani. Na angependa fedha zitumike zaidi kwenye kuboresha hali nchini Marekani. Lakini ni haki tukisema kuwa kuharibu jambo ni suala moja, na kukimbia bila kurekebisha jambo hilo ni kosa kubwa.

Marekani sasa inaondoka Afghanistan ikiharakisha kuondoka askari na raia wake, ikiwaacha watu wa Afghanistan kwenye taabu kubwa kuliko ulivyokuwa kabla ya uvamizi wa Marekani. Kwa sasa sio tu Afghanistan inakumbwa na msukosuko mkubwa wa kibinadamu, hali mbaya ya usalama, bali pia kutokana na uzembe wa Marekani, nchi nyingine nyingi duniani zimelazimika kupokea wakimbizi kutoka Afghanistan ambao maisha yao yamekuwa hatarini kutokana na kushirikiana na majeshi ya Marekani na yale ya NATO.
 
Back
Top Bottom