Kutosupport chadema ni pigo kwa wananchi wote

Masauni

JF-Expert Member
Aug 15, 2010
386
57
Nimekuwa nafuatilia kwa karibu sana hii ishu ya CHADEMA Kutomtambua Kikwete. Baadhi ya wananchi wakiwemo wasomi(sina uhakika kama ni wengi) wamekuwa wakipinga kitendo hicho, na sababu kubwa wanayoitoa ni kuwa jambo hilo litaicost sana CHADEMA! Lakini mimi namtazamo tofauti kabisa, na nionavyo mimi kutoipa support Chadema haitaighalimu Chadema bali itatughalimu sisi wananchi tena kwa kiwango kikubwa!! SABABU ZENYEWE NI HIZI

  • CCM itakapoona kwamba wananchi wamepinga kitendo cha CHADEMA, itawapa nguvu na itakuwa ni golden chance kwa CCM kuendeleza ubabe wao(hakutakuwa na TUME HURU YA UCHAGUZI, KATIBA HAITABADILISHWA). Katika hotuba ya kikwete hakuongelea kabisa swala la katiba auTume huru(siyo vipaumbele vyake) na hata wapinzani wakipeleka bungeni hoja hiyo itapingwa kwa sababu ya wingi wa CCM bungeni.

  • Kutoisupport CHADEMA, it will be a big blow for tanzanians kwa sababu itawapa CCM kujustify yale wanayoyafanya.Nakumbuka moja ya post zangu niliwahi kusema kuirudisha CCM madarakani ni kuipa CCM go ahead na ufisadi,ni kusema hatutaki katiba mpya, hatutaki NEC huru. Kikwete alipokuwa anaapishwa na katika hotuba yake ya jana bado alisema kwamba ushindi wetu ni kuwa wananchi wanatukubali, na utawala wetu ni mzuri na tunayoyafanya ni mazuri, hii maana yake ni kwamba hakuna mabadiliko makubwa ktk serikali yake sababu yaliyofanywa nyuma yamewaridhisha wananchi yataendelezwa hayo.
  • Nimalizie kwa kusema kwamba the only way ya kuleta mabadiliko ya kweli Tanzania ni WATANZANIA kuwasupport wanamageuzi wakweli (CHADEMA).bila hivyo maisha yataendelea kuwa magumu,demokrasia ya kweli ni ndoto,ufisadi kumalizwa ni ndoto.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom