Kutosimamisha uume sio tatizo la kimwili bali limeegemea kiakili zaidi

LELELU

Senior Member
Jan 29, 2018
167
259
Salamu kwenu wote ndugu zangu leo nimekuja kusema jambo ambalo watu wengi huwa tunachanganya sana.

Ukiwa na mke wako kisha uume ukawa hausimami basi jua kabisa sio kwamba una upungufu wa vitu fulani labda mlo au una ugonjwa flani wa kimwili laaa bali ni tatizo la kiakili zaidi.

Ikiwa macho yako unayaachia kutizama kila mwanamke basi akili nayo itazoea moja kwa moja kuna watu leo wanatabia ya kuwatizama wanawake warembo kama barabarani au kwenye internet lakini wanawatizama kwa kuwatamani na wanawatafuta kwa makusudi waburudishe roho zao kwa kuwaona wanawake hao (kwa kuwatamani).

Lakini ikiwa mtu unawaona warembo na akili yako ikachukulia kawaida yani mfano wanaume wa dar wanavopishana na warembo wanaona kawaida tu baadhi yao na kufanya mengine lakini wengine macho juu juu kutizama kila apitae njia.

Sasa hii ya kutizama kwa kuwatamani ndio mbaya zaidi kwa sababu unapomtizama mrembo mara nyingi kwa kumtamani tayari akili yako inahifadhi picha ile na kila picha ambayo utaitizama kwa kuwa tu hukuchukulia poa.

Mfano leo watu wanaotizama sana movi za mbele hasa za Action basi utaona wakitizama movie za bongo wanaona sio kitu na hawawezi kuigiza..ni kwa sababu akili zao zilishazoea kuona bora ya hivi vya bongo ndiyo mana wanadharau na hyo ni akili yenyewe.

Sasa wewe unaetizama warembo wakali wacheza porno hawana hata kipele na makalio mfano wa duara alafu mwisho wa siku unataka kusimamisha na kusisimka na mkeo ambae hata akitembea kanga haichezi huku nyuma na vipele vya joto kwa mbaalii???

Usitegemee kabisa kwa sababu akili ilishazoea kuona vitu bora zaidi ya hivyo
ikiwa wewe ni mtu wa kutafuta picha kama hizi kwa kukidhi hisia zako na matakwa yako basi tambua unajitafutia matatizo makubwa sana.

Nawasilisha kwa wadau wenzangu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom