Kutosajili laini ya Simu kutozwa faini ya Tsh milioni 5 au kifungo cha mwaka mmoja jela

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
25,284
38,305
Watanzania tujiandae kisaikolojia, milioni tano sio mchezo hasa kwa usawa huu.

Kwa nini wasiifunge laini ambayo haijasajiliwa kuliko kutunga sheria ya ajabu kama hii.

Wengi tutachezea jela.
*****

Ni nadra kwa Bunge kumaliza mkutano mmoja bila ya kufanya marekebisho ya sheria, na Bunge linaloanza vikao vyake leo, litayafanyia marekebisho sheria kadhaa, ikiwemo itakayompeleka gerezani kwa miezi 12 au kulipa faini ya Sh5 milioni, mtumiaji wa laini ya simu isiyosajiliwa.

Hii itawezekana kama Bunge la Jamhuri ya Muungano litakubaliana na mapendekezo ya Serikali ya kurekebisha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, ikiwa ni moja ya mapendekezo ya mabadiliko kadhaa yatakayowasilishwa katika mkutano huo wa 16.

Katika marekebisho hayo, Serikali pia inapendekeza adhabu kwa mtoa huduma, msambazaji, wakala ama aliyethibitishwa kushughulika na uuzaji ama usambazaji wa kadi za simu za mkononi, atakayesababisha kwa namna yoyote kutumika kwa laini ya simu isiyosajiliwa.

Kwa kundi hilo, mapendekezo yanataka wahusika watozwe faini isiyopungua Sh10 milioni au kifungo kisichopungua miaka miwili jela au vyote kwa pamoja.

Serikali iliamua kuachana na usajili wa zamani wa laini baada ya kuona mfumo uliokuwepo unatumiwa vibaya na wahalifu ambao waliweza kusajili chipu za simu kwa kutumia picha ya mtu yeyote.
 
Kwa Nini na kwenye simu fake awakuweka fine,line nikitu kidogo Sana kuzifunga Sasa hivi nikisafiri nje ya mipaka ya tz nikirudi baada ya miezi mitano Mara nyingi line inakuwa ishafugwa ili limenitokea juzi halotel nilipowauliza wakaniambia miez mitatu kwao inatosha kufunga line Kama aipo kwenye simu.kama nitakuwa sijasajili kwa halama ya kidole Hadi deadline day Bora waniondolee mnara wao tusisumbuane kwakweli
 
Siku ukifikishwa mahakamani we jibu hivi Mheshimiwa hakimu sikuona umuhimu wa kusajili line kwa sababu nilipanga siku nyingi ifikapo mwaka huu moja ya malengo yangu ilikua ni pamoja na kuachana na matumizi ya simu.

Hivyo mheshimiwa hakimu mbele ya mahakama yako tukufu kutosajili line yangu kusichuliwe kuwa ni kosa, bali ni moja ya kutimiza malengo yangu niliyojiwekea.
 
Adhabu za kidikteta ambazo ni kubwa sana ukilinganisha na kosa husika. Wakati huo huo yule mhujumu uchumi mkubwa nchini aliyekwapua 1.5 trillion hazina na uhujumu uchumi mwingine mbali mbali ikiwemo kukwapua nyumba za Serikali bado anapeta Ikulu yeye ni kundi la UNTOUCHABLES pamoja na mafisadi na wezi akina mkapa na kikwete.

Watanzania tujiandae kisaikolojia, milioni tano sio mchezo hasa kwa usawa huu.

Kwa nini wasiifunge laini ambayo haijasajiliwa kuliko kutunga sheria ya ajabu kama hii.

Wengi tutachezea jela.View attachment 1196372
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom