Selous
JF-Expert Member
- Jan 13, 2008
- 1,325
- 144
na Amana Nyembo - Tanzania Daima
SHIRIKA la Utangazaji Tanzania (TBC), limeomba radhi kwa kushindwa kurusha matangazo ya moja kwa moja ya kikao cha Bunge la Bajeti, Juni 23, wakati Waziri Kivuli, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Dk. Willibrod Slaa, akisoma hotuba yake.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa TBC, Tido Mhando, alisema, hali hiyo ilisababishwa na matatizo ya kiufundi.
Mhando alisema baada ya tatizo hilo kutokea mafundi walijitahidi kufanya marekebisho kwa muda mrefu lakini hawakufanikiwa, hivyo mitambo ya TBC ilishindwa kufanya kazi kama inavyotakiwa na kuwakosesha watazamaji wa televisheni hiyo kuangali kikao cha Bunge cha jioni ya siku hiyo wakati kinaanza.
Juhudi za mafundi zilifanikiwa muda mrefu baadaye, ingawa bado kikao cha Bunge kilikuwa kikiendelea, tuliona si busara kurejesha matangazo hayo kikao kikiwa katikati, alisema Mhando.
Alisema baada ya tatizo hilo kutatuliwa na mafundi, TBC ilimualika Dk. Slaa katika kipindi cha asubuhi cha Jambo Afrika Jambo Tanzania, ambako aliyazungumzia masuala ya hotuba yake kwa kirefu, pamoja na hotuba yake kutumiwa katika taarifa ya habari ya usiku.
Alisema siku moja kabla ya tukio hilo, matangazo yalikuwa yakikatika lakini hali hiyo ilidhibitiwa mapema na mafundi wa shirika hilo.
Mhando aliwaomba radhi watazamaji wa TBC kwa usumbufu uliojitokeza siku hiyo na siku iliyofuata baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi, wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipokuwa akitoa hotuba yake ya bajeti.
Matatizo ya kiufundi kwenye mitambo yetu ya kurushia matangazo ya moja kwa moja yameendelea kwa muda mrefu sasa, tuliwajibika kupeleka kifaa kingine cha akiba Dodoma ili kuinusuru hali hiyo na wakati huo huo tumelazimika kumtuma haraka fundi wetu, Kabisi nchini Uingereza ili kukifanyia marekebisho kifaa hicho, hata hivyo kilionekana hakifai na hivyo tukalazimika kununua kipya, alisema Mhando.
Alisema hawakuwataarifu mapema watazamaji wa TBC kuhusu tatizo hilo kwa sababu walikuwa na matumaini ya kulimaliza tatizo hilo mapema.
Aliwatoa wasiwasi wananchi na wabunge kwa taswira yoyote mbaya iliyojengeka na kuwahakikishia kuwa chombo hicho kiko kwa ajili ya umma wote wa Watanzania na mipango inazidi kufanywa ili kufikisha matangazo yake sehemu zote nchini.