Kutomwambia Mtu kuwa Muathirika ni Sahihi kwa Jamii? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutomwambia Mtu kuwa Muathirika ni Sahihi kwa Jamii?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Chapakazi, Apr 29, 2011.

 1. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Vipi wadau?
  Nime-download kwenye mtandao kipindi cha Njia Panda kinachorushwa na Clouds FM cha tarehe 10/4. Mada ilikuwa inaongelea swala la Loliondo! Kweli nilikuwa impressed na jopo la wachangiaji walioletwa kuongelea hii mada!

  Tatizo langu na lililonitia shaka, ni mmoja wa wachangiaji ni kijana wa Form 2. Yeye ana virusi vya ukimwi na sickle-cell anaemia. Lakini daktari wake ambaye naye alikuwa mchangiaji kwenye kipindi anakiri kuwa huyu kijana hajui kuwa ana VVU. Na iliwabidi wamtoe huyu kijana chumbani ili kuweza kuzungumzia condition yake kama muathirika. Kwa kifupi ni kuwa hawajamwambia yeye ni muathirika!!

  Swali langu...je huyu kijana asiyejua kuwa ni muathirika, kweli sio hatari kwa jamii? Hapa naongelea hasa kwa wadogo zetu waliopo shuleni naye. Yani ikitokea akakutana kimwili na binti, na kwa vile yeye hajui kuwa ni muathirika, si kuna probability kubwa kuwa ataweza kufanya ngono bila kinga? Na hii si itachangia kusambaza kwa wengi?

  Mimi namshangaa sana huyu daktari. Imagine kuna cases za namna hii ngapi huko mitaani. Kweli sio kutafuta majanga huku? Kweli nitashindwa kumshtaki huyu daktari kwa negligence misconduct?
   
 2. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  kwa mtazamo wangu inawezekana kutokana na hali ya huyo kijana kisaikolojia daktari akaona hatahimili kujua hali yake wakati mwingine nimeona dr anawaambia wauguzaji juu ya fate ya mgonjwa wao.ukweli uko pale pale,kila mmoja wetu anawajibika kujilnda dhidi ya ukimwi,hata hao wanafunzi wenzie nao,either wapime kabla ya kuvunja amri ya 6,ama watumie kinga.
   
 3. Big One

  Big One JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 759
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  kweli inasikitisha hata mm nlikuwa msikilizaji kpndi kile kwel dr alimficha yule mtoto na ana ngoma kwahyo yule mtoto shuleni kuna uwezekano mkubwa wa kuambukiza wenzake yaan yule dr cjui anafikilia nn au ma amo
   
 4. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kwani hakuna services za kumsaidia huyo mtoto kisaikolojia? Hapa tatizo sio mtoto, bali jamii! Unahatarisha jamii kwa ujumla kwa kumficha mtoto ukweli! Ni rahisi kusema kuwa ni wajibu wa wengine kujilinda. Lakini itakapotokea kukugusa wewe binafsi, lazima utauliza maswali mengi.
  Pia ni wajibu wa yule mtoto kujikinga! Na kwa kujua ukweli ni mwanzo wa kinga!!
   
 5. NAHUJA

  NAHUJA JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2011
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 15,084
  Likes Received: 15,722
  Trophy Points: 280
  Kwanza huyo kijana sio mwathirika waathirika ni ndugu zake na taifa kwa ujumla. yeye anaitwa "mtu anayeishi na virus vya ukimwi"

  Waathirika ni wengine
   
 6. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  mhh???
   
 7. Mahai

  Mahai JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hizo kesi zitakuwa nyingi sana, na kusema kweli inaogopesha. Kwa nini kijana asiambiwe hali yake? Yuko form II tayari, ni kijana mtu mzima kabisa ambaye anaweza kupambanua mambo mbalimbali. Vijana wanatakiwa kujua hali zao tangu wakiwa wadogo maana wataweza kujilinda na hata kuzoea kutumia dawa wenyewe. Sasa kama huyo mtoto kashaanza hizi dawa za ARVs wanamwambia ni kwa nini anakunywa kila siku? Au wanamdanganya ni za sickle cell? Au wanasema ana ugonjwa wa moyo? Maana at some point itabidi aulize kwa nini nakunywa dawa kila siku. Watoto wanapoambiwa hali zao mapema it will help them to know how they can grow up with HIV, how they can be adults with HIV. Because that is the big part of their life.
   
 8. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ndio hapo sasa! Yani hii ni hatari kubwa kwa jamii! Huwezi kuacha vijana wazurure mitaani huku wana ngoma bila kuwataarifu!
   
 9. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2011
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Duh naomba Mungu huyo kijana hajue haraka na abadilishe daktari maana huyo sio daktari ladba pesa tu ndio mbele kwake

  Na akijua ampeleke kotini kwa kuvunja patient confidentiality kati ya huyo doc na mgonjwa wake bila hata ruhusa etc
   
 10. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Yani hii ishu ni kubwa na ina angle nyingi sana! Huyu daktari ameleta maswali kibao!
   
Loading...