Kutolewa kafara kwa Mwandishi Daud Mwangosi, mpango ulikuwa Chadema ifutwe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutolewa kafara kwa Mwandishi Daud Mwangosi, mpango ulikuwa Chadema ifutwe!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Sep 17, 2012.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Adverasenso.jpg

  Tuanze kwa kujikumbusha huyu msemaji wa Polisi, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Mama Advera Senso alivyosema kuhusu kifo cha Mwandishi, Daud Mwangosi;

  1. Mwandishi alikuwa akikimbia kutoka upande wananchi na kuelekea walipokuwa Polisi.
  2. Marehemu inasemekana alipigwa na kitu ambacho mpaka sasa hakijafahamika bado mpaka uchunguzi ufanyike.
  3. Kuna kitu kilirushwa kikitokea upande wa Wananchi na kumfikia ambacho kilimjeruhi pia Askari akiwamo Mkuu wa kituo cha Polisi.
  4. Jeshi la polisi limewakamata 32 waliokuwa wakienda Mbeya kwenda kufanya vurugu, wakitokea Iringa kuhusiana na kifo cha Daudi Mwangosi.

  Mpaka sasa najiuliza...hivi hali ingekuwaje kama picha zinazoonesha jinsi tukio zima lilivyotokea hazingekuwepo, lakini sipati jibu. Lililo wazi kabisa ni kwamba Chadema ingejikuta katika hali ngumu kweli kweli kwa sababu ingehusishwa moja kwa moja na kifo cha mwandishi Daud Mwangosi. DW, BBC, Aljazeera na vyombo vingine vya habari vya nje habari kuu ingekuwa Tanzania, kisiwa cha amani, yakabiliwa na hatari ya machafuko kutokana na kitendo cha chama cha vurugu...Chadema kumuua mwandishi wa habari.

  Mpango ulisukwa ukasukukika na kuna watu wanalaani kwa nini haukufanikiwa kama ulivyopangwa na mbinu bado zinatafutwa za kuwajumuisha viongozi wa Chadema na kifo hiki. Lakini Mungu mkubwa...safari hii akasema imetosha, watu wangu wameteseka vya kutosha mikononi mwa hawa waovu! Watanzania tumepewa ishara na ndio sababu kubwa wasimamizi wakuu wa mpango huu hawawezi kutoa tamko lolote hadi sasa kwani giza nene limetanda mbele ya macho yao, wamepigwa butwaa na midomo imewakauka.

  Sasa wameachiwa mavuvuzela kama Tendwa, Nape, Tambwe Hiza, Yusuf Halimoja, na vikaragosi vingine tunavyovishuhudia humu jamvini wakiongozwa na zomba, Ritz na wengineo. Lakini safari hii wamegonga mwamba na hawana pa kutokea, laana inawaandama kama kivuli na muda si mrefu wataanza kuumbuana kwani damu ya Daud Mwangosi haitowaacha wapate usingizi. Msemaji wa Polisi, ASP Advero Senso kaa chonjo, matamko unayoyatoa ni sawa na ya aliyekuwa msemaji wa Sadam Hussein, Tarik Aziz!

   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mkuu umemaliza kila kitu.Wao wana Ibilisi CDM wana Mungu mtakatifu
   
 3. satellite

  satellite JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mission Impossible teeeeehhhh!teehhhhh!
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Zomba please you above this..Kwa hiyo akiwa mwanaChadema ndio inaswihi auawe?..Polisi wana jukumu la kumlinda nani kama sii mwananchi au Chadema hawa sii wananchi maana tuwe tunajiuliza maswali magumu japokuwa tuna mapenzi yetu badala ya kuwa kama wale waarabu wanaoua hata waandishi wa habari kwa sababu ni Wazungu na ni maadui zao..
   
 5. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Siku ya kufa kwa nyani, miti yote huteleza. Walijaribu kwa tabibu Dr. Ulimboka, wakanasa, wakahamia kwa mwandishi Mwangosi, wakanasa na sasa wanatafuta pa kutokea wamenasa, milango yote imebana. Kikwete kimyaa, Pinda kimyaa wamenasa, sauti hazitoki. Hao hao polisi wanaowatumia ndio hao hao watakaowaumbua...it is just a matter of time, hiyo mikono iliyojaa damu ya Watanzania wasio na hatia haisafishiki kirahisi namna hiyo tik, tak, tik, tak...
   
 6. MLUGURU

  MLUGURU JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2012
  Joined: Mar 30, 2012
  Messages: 819
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 80
  cheo dhamana,matamshi yao yatakuja wafunga,wako wapi makomandoo wa mauaji ya kimbari,
   
 7. k

  kitefure2 Member

  #7
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Time will tell
   
 8. B

  Bubona JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Jeshi la Polisi limegeuzwa kuwa kitengo cha CCM. Nyakati hatari katika taifa; Mungu utuokoe na uovu huu!!
   
 9. nzitunga

  nzitunga Senior Member

  #9
  Sep 18, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kufuta CDM ni kosa kubwa sana, ni kama walivyokosea kufuta MWANAHALISI. Uchafu hauondolewi kwa kuwatimua wanaokwambia wewe mchafu, bali unaondolewa kwa kujitasmini na kujisafisha.
  Watoa habari (ambao wamechoshwa na utumbo aka uzandiki unaoendelea ktk serikali) sasa wanayapeleka kwa viongozi wa Siasa. Ni bora mwanzoni waliyapeleka kwa Mwanahalisi.
  Waswahili walisema siku ya kufa nyani miti yote huteleza. Kinachowasumbua CCM ni kwamba wanadhani mbaya wao ni Mbowe, Dr Slaa, Mnyika, Zitto, nk au kwa ujumla CDM. Kumbe mchawi yumo ndani ya CCM yenyewe! Wananchi wamewachoka Si wote wanoenda mikutano ya CDM ni CDM, hata hapa JF si wote wanaoitwa pro-CDM ni CDM. The simple maths is "Wananchi wamechoka usanii unaondelea" CCM na serikali yake.

  CCM imeamua kutumia turufu yake ya mwisho baada ya kutumia turufu za ukabila, ukanda, udini na sasa vuruga amani ya Nchi, ua wananchi ili waogope kwenda mikutanoni, hii inaitwa "liwalo na liwe" au "punda afe mzigo ufike" lakini uzuri wa hii dunia ni kwamba za mwizi arobaini, "Unaweza kuwadanganya watu fulani kwa muda fulani, Lakini huwezi kuwadanganya watu wote kwa muda wote"

  Kuna habari kwamba siku chache kabla hajaua, Muuaji alikuwa akimtania mwenzie, "ukiingia katika anga zangu takulipua". Ni kweli au si kweli si jambo la muhimu. cha muhimu ukifuatilia matamshi ya viongozi wengi IGP, Nchimbi, Tyson, nk utagundua kwamba wameacha uhalisia [Polisi wamehua mtu akiwa ktk kazi yake halali] na badala yake wameingiza Siasa.

  Nimalize kwa kusema Wanaipa CDM nguvu ni CCM wenyewe!
   
 10. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #10
  Sep 18, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Mpango wao umeingia mkenge!
   
 11. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #11
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Nyinyiemu hawana ujanja wana wasiwasi kama wanaoga nje tena mchana kweupeee.
   
 12. calculator

  calculator JF-Expert Member

  #12
  Sep 18, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Huwa napendaga tu kusoma post zako. Kweli una kazi mahsusi huku. Jitahidi tu kaka.
   
 13. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #13
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Hawajui kuwa ibilisi hawezi kukupa sapoti mpaka mwisho. Kuna wakati moto humchoma na kuwakimbia wafuasi wake.
   
 14. G

  GlorytoGod Senior Member

  #14
  Sep 18, 2012
  Joined: Sep 8, 2012
  Messages: 157
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Amina, Daudi kwenye vitabu vitakatifu alisema kuwa alikuwa kijana na sasa yu mzee lakini hakuona mwenye haki wa Mungu ameachwa wala watoto wake wakiomba chakula.

  Ninaamina mungu aliyewaepusha chadema na hilo hata mengine atakuwa ngao na kigao kwao CHADEMA wasikate tamaa maana aliyeko upande wetu ni mkuu mno kuliko aliyeko upande wa mafisadi.
   
 15. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #15
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,964
  Likes Received: 6,735
  Trophy Points: 280
  Ninaikubali kwa asilimia 100, tathmini yako. Kuongezea uzito kuwa hii ilikuwa missin ambayo iliandaliwa na viongozi wa juu kabisa wa CCM, nakumbuka kabla ya tukio la kuuawa muuza magazeti wa Msamvu-Morogoro, Ally Zona, siku mbili kabla, alijitokeza Nape na kuongea na waandishi wa habari na kuwaambia kuwa kwenye mkutano wa Chadema wa Morogoro, Chadema wameandaa kufanya vurugu kubwa, sasa baada ya polisi kumwua huyo Ally Zona, na taarifa za polisi kuwa aliuawa na kitu chenye ncha kali kilichorushwa toka kwa wafuasi wa Chadema, ndiyo tukapata tafsiri ya utabiri wa Nape. Sasa kwa kuwa hakukuwa na picha tukio la Morogoro, magamba wakaona waendeleze mbinu zao hizo chafu huko Iringa. Kwa bahati nzuri, Mungu akasimama upande wa wanyonge, na tukio zima limo ndani ya mikanda ya video. Na hiyo siyo siri, ndiyo sababu kubwa iliyomfanya JK, ashikwe na kigugumizi. Kiongozi tanayemfahamu kwamba ndiye anayeshiklia rekodi ya kuhudhuria misiba, hata ya waigizaji wa filamu! leo kwa taaluma muhimu kama ya uandishi wa habari, kashindwa hata kutuma salaam za rambirambi! Kweli tunapaswa tumshukuru Mungu, kwa kuwaumbua wauaji wakubwa hawa!!
   
 16. kbosho

  kbosho JF-Expert Member

  #16
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 4, 2012
  Messages: 12,505
  Likes Received: 3,314
  Trophy Points: 280
  hata roma ilianguka sembuse awa wacheza vduku ccm
   
 17. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #17
  Sep 18, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Asante meg3, wao wana silaha na sisi tuna Mungu.
   
 18. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #18
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,964
  Likes Received: 6,735
  Trophy Points: 280
  Na pia nakubaliana na tathmini yako kuwa, mission kubwa ya CCM ilikuwa kukifuta Chadema, baada ya kupewa taarifa na UWT kuwa moto wa M4C, hauna jinsi ya kuuzima, na ndiyo maana tumeshudia matamko kadhaa toka kwa vibaraka wa magamba, akiwemo Tendwa kutamka kuwa Chadema ni chama cha vurugu, yanayosababisha maafa kwenye mikutano yao, kwa hiyo ana mpango wa kukifuta! Kwa kauli ya Tendwa, akijua wazi anaupotosha umma wa watanzania, kwa kuwa vurugu hazisababishwi na viongozi na wafuasi wa Chadema, bali ni polisi waliopewa maelekezo maalum na magamba, baada ya kugundua kuwa hali yao ni taabani. Kwa kauli hiyo ya Tendwa, ambaye kwa taaluma ni mwanasheria mwenye hadhi ya ujaji, naamini ametukanisha sana hadhi ya ujaji, na naamini anastahili kuvuliwa kabisa ujaji!!
   
 19. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #19
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,964
  Likes Received: 6,735
  Trophy Points: 280
  Na sasa hivi umma wa wa-TZ, unasubiria kwa hamu kubwa sana hotuba ya mwisho wa mwezi ya JK, ili tumsikie anaongelea nini kuhusu kifo cha Mwangosi. Na hatuamini kuwa atapuuzia kuongelea suala hilo kubwa, lililovuta siyo hisia za wa-TZ, peke yake, bali dunia nzima kwa ujumla wake, na ndiyo maana hata vyombo vikubwa sana vya habari vya dunia hii, kama vile CNN, Aljazeera, DW, na BBC, vilitoa coverage ya habari hiyo kubwa, tunajua kuwa kimya kikubwa cha JK, kuhusiana na suala la Mwangosi, na kukataa kwake kuwavua madaraka watu kama Mwema, Kamuhanga na Chagonja kunatoa tafsira ya wazi kabisa kuwa, operesheni mauaji ya Nyololo yalikuwa na baraka zote toka kwa mkuu wa nchi!!
   
 20. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #20
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kuuliwa alijitakia mwenyewe, unakwendaje kmvaa mkubwa wa polisi wakati umeambiwa sambaratika.

  Nasema hivi kwanini aandike mwandishi na asiandike mwana chadema, au lina impact na sympathy zaidi na ndiyo maana akachombezwa akafanye alichofanya? maana Slaa alikuwa anajuwa watakaidi, ushahidi ni ujumbe aliomtumia Mwema. Kama alijuwa watakaidi asijuwe na hao wakaidi waliowachombeza huko?

  Ukweli ubaki kuwa ukweli.

  Kwa hili la chaddema kuamrisha watu wavunje amani ili nchii isitawalike, hata wafanye nini, Watanzania walio wengi wanaelewa kinachiendelea na wala huu upuuzi hautoijenga chadema kama chama cha walio wengi.

  Huyo alikuwa huko kwa kazi za chadema na alikuwa mmoja ya wailochombezwa na Slaa kufanya fujo.
   
Loading...