Tatizo la kutokwa na damu kwenye fizi: Fahamu chanzo na namna ya kutatua tatizo hili

Kuna nadharia kwamba time unabrush meno kama hujatoa damu basi meno hayajatakata, Kuna ukweli wowote hapa?
 
Habari wadau...
Aisee naomba msaada wa kitabibu...fizi zangu zinatoa damu...sana sana kwenye jino moja la mbele...naona linalegea...nimebadili dawa za meno...ila wapi...nini tiba?
Natanguliza shukrani!
 
Tatizo hilo limenitesa sana tangu 1990. Ni mwaka huu nimepona kwa Tiash Tooth Paste. Jaribuni muone. Dawa nyingi mno nilishatumia bila mafanikio. Vitamini C nilimeza hadi kuchanganyikiwa... Usafi wa meno nilifanya hadi nikahisi watayatoboa. Sasa sijambo!
inauzwa sh. ngap
 
Anaejua tiba anisaidie,nilienda muhimbili kitengo cha afya na kinywa hawajaona tatizo.Pia Nina kisukari je vina uhusiano?
 
Wamarekani na mataifa makubwa yote duniani wameshindwa kupata tiba ya kutibu kisukari...Ewe mtanzania epuka matapeli, kisukari hakina tiba
 
Wandugu mimi nina tatizo la kutokwa damu kinywani kila ninapopiga mswaki,yaani nikipiga tu mswaki ile kutema basi natema damu tupu,na wala sisikii maumivu kusema kuwa labda nina vidonda mdomoni.

Nina kawaida ya kupiga mswaki mara mbili kwa siku,yaani asubuhi na usiku kabla ya kulala,tatizo hili limekuwa nalo kwa muda sasa, Je ninaweza kusaidiwaje ili nijue tiba na matatizo haya?

Asante.
 
Wandugu mimi nina tatizo la kutokwa damu kinywani kila ninapopiga mswaki,yaani nikipiga tu mswaki ile kutema basi natema damu tupu,na wala sisikii maumivu kusema kuwa labda nina vidonda mdomoni.

Nina kawaida ya kupiga mswaki mara mbili kwa siku,yaani asubuhi na usiku kabla ya kulala,tatizo hili limekuwa nalo kwa muda sasa, Je ninaweza kusaidiwaje ili nijue tiba na matatizo haya?

Asante.
Unahitaji kufahamu damu inatoka sehemu gani, kwenye fizi, meno yenyewe au sehemu gani ya mdomo?
 
wakuu heri ya pasaka, ni zaidi ya miaka 20 tatizo la kutokwa na damu kwenye fizi limekua likinikabili ila sikuwahi fuatilia chanzo na treatment. Hili tatzo hua linatokea hasahasa muda wa kuswaki. na damu inayotoka ni kidogo sana.

Kilichonifanya nisifuatilie ni kutowahi pata maumivu yeyote kutokana na hali hyo.
Leo(mchana wa leo) ghafla nimeshangaa damu imeganda mdomoni imezunguka jino moja na inaoka kwa wingi ikanishtua sana. Ila namshukuru Mungu maana baada ya kusukutua na maji haikutoka tena.

Je, chanzo ni nini?
Je, nifanyeje isitoke tena?
Natanguliza shukrani.
 
Makaura,
Kuna sababu nyingi. Lakini moja kubwa ni formation ya kitu kinaitwa tartar kati ya fizi zako na meno. Kidiri mtu unaovyoishi (japo unakuwa unaswaki kila siku) lakini kuna ''ukoko'' wa aina fulani (kama simenti) unajijenga kidogo kidogo kati ya fizi na meno.

Huu ukoko unakuwa ni kama nyumba ya kuishi bakteria ambao hushambulia fizi na kusababisha meno kutoka damu. Unatakiwa uwe unakwenda kwa dentist mara kwa mara anaukwangua kwa kutumia vifaa maalum.

Kumbuka hata ukiswaki kwa usahihi namna gani huwezi kuuondoa. Inabidi dentist mwenye vifaa vya ncha kali na atakwangua jino kwa jino pia kati ya fisi na meno.
 
Back
Top Bottom