Tatizo la kutokwa na damu kwenye fizi: Fahamu chanzo na namna ya kutatua tatizo hili

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,012
1588703113944.png
BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU KUHUSU TATIZO HILI
Kimekuwepo kilio cha muda mrefu toka kwa wadau mbalimbali juu ya Tatizo la Kuvimba fizi. JF imeonelea ni vema iusimamie mjadala huu kwa ukaribu.

(Maoni na ushauri kwa wenye uhitaji yanaanzia post ya 2)
===
Salamu waungwana madaktari.

Nna kabinti ka ndugu yangu naishi nako kana matatizo ya kutoka damu kwenye fizi za meno... kabinti kana miaka 17.

Akipiga mswaki damu inayotoka inatisha. Akimega tunda kama apple lazima damu itoke kwenye fizi.

Yaani kila kinachofanyika mdomoni na kuhusisha matumizi ya meno asilimia kubwa damu lazima itoke kwenye fizi.

Kabla sijampeleka kwa daktari nimeona nipitie hapa kwenu wataalam mnisaidie labda kuna njia mbadala wa tiba bila kwenda hospitali.

Ahsanteni kwa kunielewa na kwa msaada wenu.
---
Jamani wataalamu habarini za kazi?

Jamani mimi nna tatizo la kuvimba fizi za meno kwa mda flani na baadae zinapona, zinakaa mda kama miezi miwili then zinauma na zinapona tena bila kutumia dawa yoyote.
wadau sababu ni nini?

MSAADA
Mbarikiwe wote
---
kwa muda sasa nimekua nikitoka damu kwenye fizi za meno kila ninapokua napiga mswaki, leo asubuhi wakati nakunywa chai ile nang'ata mkate nikaona damu kwenye mkate nadhani tatizo limekua kubwa. naombeni ushauri wenu kama kuna mtu mwenye idea ya hili tatizo na namna ya kulitatua.
---
Habari wana Jf,

mimi ninatatizo la ktokwa na Damu kwenye fizi mdomoni hasa wakati ninapokua napiga mswaka.Hata wakati mwingine nikishika tama afu nikatema mate, yanakua na damu. Fizi huwa haliashi.

Kwa mwenye kufahamu dawa ya kumaliza au kupunguza hali hiyo naomba anifahamishe.

Aksante:

nerd:
===
UFAFANUZI WA JUMLA WA TATIZO HILI
Taarifa Kuhusu Ugonjwa wa Fizi

Ugonjwa wa fizi una hatua mbalimbali. Hatua ya kwanza ni kuvimba fizi (gingivitis). Fizi zinazotoa damu ni dalili ya hatua hiyo. Huenda mtu akatokwa na damu anapopiga mswaki, au anapotoa uchafu kwenye meno kwa kutumia uzi mwembamba au bila sababu yoyote. Vilevile, kutokwa na damu mtu anapochunguzwa meno na daktari ni dalili ya ugonjwa huo.

Ugonjwa wa fizi husonga kwenye hatua inayofuata (periodontitis). Kufikia hatua hiyo, mifupa na fizi zinazotegemeza meno, huanza kuharibika. Ugonjwa huo wa fizi huenda usiwe na dalili zozote hadi unapokuwa mbaya zaidi. Dalili fulani za hatua hiyo ni kutokea kwa nafasi kati ya fizi na meno; kulegea kwa meno; mianya kati ya meno; kunuka mdomo; fizi zinazoachana na meno na kufanya meno yaonekane kuwa marefu zaidi; na kutokwa na damu kwenye fizi.

Mara nyingi kuvimba au kutokwa na damu kwenye fizi huweza kusababishwa na magonjwa mbalimbali ya kinywa na meno ambayo husababishwa na kutofanya vizuri usafi wa meno kwa usahihi au maambukizi ya bakteria ambao usababisha utando mgumu kwenye meno. Utando huu hauwezi kutolewa kwa kupiga mswaki bali kwa kutumia vifaa maalumu na wataalamu wa meno. Pamoja na maambukizi au kutofanya usafi pia kutokwa na damu kwenye fizi usababishwa na magonjwa ya damu, kupiga mswaki kwa nguvu, ukosefu wa vitamini C na K.

UGONJWA huu unawapata watu wengi sana ulimwenguni. Hata hivyo, katika hatua za kwanza dalili zake hazionekani haraka. Ugonjwa wa fizi ni hatari kwa kuwa hautambuliki mapema. Kitabu International Dental Journal kinataja ugonjwa wa fizi kati ya magonjwa ya kinywa yanayosababisha “tatizo kubwa la afya ya umma.” Kinaendelea kusema kwamba ugonjwa wa kinywa “unaweza kusababisha uchungu mwingi na kuteseka na vilevile kupunguza uwezo wa mtu wa kula na kufurahia maisha.” Kuchunguza ugonjwa huo kunaweza kukusaidia kujikinga.

Chanzo na Madhara ya Ugonjwa wa Fizi
Kuna mambo kadhaa yanayochangia kupata ugonjwa wa fizi. Utando wa bakteria ambao kwa kawaida hutokea kwenye meno ndicho chanzo kikuu. Usipotolewa, bakteria husababisha kuvimba kwa fizi. Hatua hiyo inapoendelea, fizi huachana na meno, na hivyo utando huo wa bakteria husambaa na kuingia chini ya fizi. Bakteria zinapofikia hatua hiyo, uvimbe huendelea kuharibu mifupa na fizi.

Utando huo, iwe uko juu au chini ya fizi, unaweza kuwa mgumu na kuwa ukoga. Ukoga pia una bakteria, na kwa kuwa ni mgumu na hushikamana na meno, hauwezi kutolewa kwa urahisi kama utando. Hivyo, bakteria huendelea kuharibu fizi.

Kuna mambo mengine pia yanayochangia ugonjwa wa fizi. Yanatia ndani uchafu mdomoni, madawa yanayopunguza kinga mwilini, magonjwa yanayosababishwa na virusi, mkazo, kisukari, kunywa pombe kupita kiasi, kutumia tumbaku, na mabadiliko ya homoni kwa sababu ya mimba.

Ugonjwa wa fizi unaweza kukuathiri kwa njia nyingine pia. Maumivu mdomoni na kung’oka meno kunaweza kupunguza uwezo wako wa kutafuna chakula na kukifurahia. Pia, unaweza kuathiri matamshi na sura yako. Vilevile utafiti umeonyesha kwamba usafi mdomoni unahusiana na afya ya mtu kwa ujumla.

Kutambua na Kutibu Ugonjwa wa Fizi
Unawezaje kujua kama una ugonjwa wa fizi? Huenda ukaona baadhi ya dalili zilizotajwa kwenye makala hii. Ukiziona ni vizuri kumwona daktari maalumu wa meno ili achunguze fizi zako.

Je, ugonjwa wa fizi unaweza kutibiwa? Inawezekana kuutibu katika hatua za kwanza. Ugonjwa wa fizi unapoenea sana, basi lengo ni kuuthibiti ili usiendelee kuharibu mifupa na fizi zinazotegemeza meno. Madaktari wa meno hutumia vifaa vya pekee vinavyoweza kuondoa utando na ukoga kwenye meno, iwe ni chini au juu ya fizi.

Hata ikiwa si rahisi kwako kupata matibabu ya meno, unaweza kuzuia ugonjwa huo hatari usikupate. Kusafisha mdomo vizuri na kwa ukawaida ndiyo njia bora zaidi ya kuzuia ugonjwa wa fizi.

FANYA YAFUATAYO KUJITIBU MWENYEWE
  • Tumia mswaki laini kusafisha meno kila siku na hakikisha unabadili mswaki kila baada ya miezi mitatu.
  • Usichokonoe meno mara kwa mara, ila tu baada ya kula ili kuondoa mabaki ya chakula.
  • Matatizo ya hormoni asa kwa wajawazito.
  • Epuka uvutaji wa sigara na tumbaku ambao huchangia matatizo mengi ya kinywa na meno.
  • Epuka matumizi ya dawa za Aspirin ispokuwa kwa maelekezo maalumu na wataalamu wa afya
  • Kula mboga za majani, matunda na vyakula vyenye vitamini C na K kwa wingi
  • Tatizo likizidi onana na madaktari wa meno na kinywa walau mara moja kwa miezi 6 kinywa kwa ushauri zaidi kuhusu dawa za kusukutua na kuua maambukizi, kuziba meno yaliyotoboka au kung'oa meno yaliyoharibika.

===
MAONI NA USHAURI ULIOTOLEWA WADAU WA JF

Ugonjwa wa ufizi huathiri ufizi na huweza kusambaa kwenye mifupa inayoshikilia meno. Hii ni mojawapo ya sababu ambazo hufanya watu kupoteza meno. Ugnjwa huwa katika hatua mbili lakini inapokuathiri waweza kutibu kabla ya kusababisha madhara

Ni nini baadhi ya dalili au ishara
Hatua ya kwanza ya ugonjwa huu wa ufizi huitwa gingivitis
Baadhi ya dalili/ishara ni pamoja na:
  • Ufizi nyekundu na iliyofura
  • Ufizi unaotoa damu unaposugua meno
  • Ufizi uliongoka kutoka kwenye meno
  • Harufu mbaya isiyoisha
Wanawake wajawazito kwa kawaida huathiriwa na gingivitis. Ukiwa mjamzito tunza afya yako ni vizuri ikiwemo meno.

Hatua ya pili ya ugonjwa wa ufizi huwa hatari sana.

Waweza kuwa na ishara/dalili zilizotajwa hapo juu
  • Usaha unaotoka kwenye meno na ufizi
  • Meno iliyolegea
  • Nafasi kubwa katikati ya meno mahali ambapo ufizi inapaswa kuwa
  • Kutokuwepo na tofauti katika mpangilio wa meno ukiyauma chini.

Unaitibu vipi?
Ukiwa na dalili zozote za hatua ya kwanza, sugua meno na utumie uzi spesheli kutoa chakula katika meno mara kwa mara na umuone daktari wa meno. Ukiitibu tatizi hili basi utazuia ugonjwa wa ufizi.

Ukiwa na dalili zozote za hatua ya pili, mwone daktari haraka iwezekanavyo. Meno yako yaweza kungoka au kungolewa na daktari wa meno ikiwa hutatibiwa mara moja. Ugonjwa huu ukiwa mbaya sana daktari wako wa meno anaweza kukuelekeza kwa daktari wa meno aliye na ujuzi wa ugonjwa wa ufizi.
---
Asprin,

Pole sana. Utapata maelezo mengi sana, lakini kimsingi unashauriwa umpeleke hospitali yoyote akaonwe na dentist.

Kwetu Afrika hatukimbilii sana kufikiria upungufu wa vitamin C mwilini, kwa sababu tunapata vitamin hizo kwa namna nyingi sana. Umeshasema akila tunda la apple anaacha damu, ina maana huyo anao uwezo wa kupata hata matunda aghali hivyo. Machungwa na mapera pia ni mfano mzuri wa chanzo cha vitamin C. Kwa hiyo ni bora kuondoa wazo hilo kabisa kwa sasa.

Hakuna kitu "KURTU" kwenye meno, kwani kutu ni zao la chuma (iron) kushambuliana na oxygen. Hakuna chuma cha namna hiyo kwenye meno. Kinachotolewa ni mwamba unaotokana (tartar au calculus) na mtu kutopiga mswaki meno yake ilivyo sawasawa na kuacha wadudu wazaliane juu ya masalia ya chakula katika aina ya utando kufunika meno, ambapo protein aina ya pellicle hufanya kazi kama cement au gundi kushikilia uchafu huo. Wadudu wanapenda kutumia masalia (au tabaka la) ya chakula kama raw material na kuzalisha tindikali ambayo hutelemsha tindikali ya mdomoni (pH) hata kusababisha meno kutoboka, lakini pia toxin ya harakati ya bacteria hao huumiza fizi taratibu.

Ukichelewa utakuta hata mfupa unaoshikilia meno unayeyushwa na meno kuanza kulegea kwa kukosa mahali pa kujishikiza. Palipo na calculus wadudu huwa attracted zaidi kukaa kwa sababu habitat yake huwafaa sana. Miamba hiyo ni ishara tosha kwamba hujapitisha mswaki eneo hilo kwa zaidi ya siku saba hata kama unapiga mswaki kila siku, maana yake hupigi ilivyo sawasawa kila eneo la jino. Daktari analazimika kukusafisha kwa kutumia vyombo maalum kwa sababu miamba hiyo haiondoki kwa kupiga mswaki wa kawaida. Huitwa SCALING.

Fizi zilizoathirika kwa kutopiga mswaki ilivyo sawasawa huwa na dalili nyingi, mojawapo ni kutoka damu hovyo hata kama zimeguswa kidogo tu, na utagundua unapopiga mswaki kikawaida unapotoka damu, ujue kuna eneo ndio kwanza limepata mwaki siku hiyo na fizi zinatoka damu. Hali hiyo huisha yenyewe kwa kuongeza bidii ya kupiga mswaki sawasawa kuzungukia meno yote mdomo mzima.

Dawa ya kusukutua anayokupatia sio badala ya kupiga mswaki, maana dawa hiyo haiondoi uchafu bali inafanya kazi ya kuwatibua bacteria wasitawale kwa kuzaliana baada ya wewe kufanyiwa usafi na daktari, kwani wadudu hupunguzwa kasi ya kuzaliana na hivyo kupunguza madhara kwa fizi.

Niseme kwa ufupi tu kwamba mpeleke mgonjwa kwa daktari aone hali halisi ilivyo na kuamua hatua bora ya kumsaidia mgonjwa wako. Inashauriwa mtu amwone daktari wa meno angalau kila miezi 6 kwa check up ya kawaida ili kushughulikia matatizo yoyote yanayojitokeza mapema kwenye fizi au meno.

Upigaji mzuri wa meno ni kila siku angalau mara mbili - BAADA ya kifungua kinywa asubuhi na kiwe ndio kitu cha mwisho kabla hujalala usiku kitandani ili kuhakikisha unadhibiti mioto ya bacteria. Sasa kupiga mswaki kabla ya kifungua kinywa ni hiari yako na sio vibaya, lakini sio sahihi kitaalam kwa lengo la kudhibiti wadudu kwa kuondoa masalia ya chakula. Ukiweza piga hata mchana. Hakikisha kila jino limepigwa mswaki sehemu zote. Huwezi kufanya hivyo kwa dakika tatu.

Itoshe kwa leo.
---
Mkuu kuvimba kwa fizi ni kutokana na mpaka wako kati ya meno na fizi kujaa vyakula na kufanya fizi zako zishindwe kupumua. Ukiacha mda mrefu bacteria wanazaliana na kuanza kushambulia meno yako. Na mara nyingi ukiwa katika hali hio pia damu inaweza au huwa inatoka wakati wa kupigwa mswaki.

Muhimu kwa sasa nenda kwa daktari wa meno wasafishe meno yako na baada hapo piga mswaki mara mbili au kila baada mlo na pia toa vyakula vilivyonasa kwenye meno kila siku baada kupiga mswaki au kabla. Kuna mashine nzuri sana za kutoa mabaki ya vyakula ambavyo mara nyingi huwezi kutoa kwa kupiga mswaki peke yake zinaitwa water pik unaweza ku-google ukasoma zaidi. Sugua fizi zako taratibu kama unakanda kila siku wakati wa kupiga mswaki kwa kutumia mswaki laini.

Ukiacha hivyo baadae meno yako yanaweza kuanza kulegea na kung'oka. Baada kupiga mswaki pia sukutua maji ya chumvi( husaidia fizi kurudi kwenye hali ya kawaida) ya vugu vugu na kama damu inatoka wakati wakupiga mswaki sukutua kwa kutumia Hydrogen Peroxide hili uweze kuua bacteria.

Kumbuka kuskutua kwa maji ya chumvi peke yake haitasaidia kama huto endelea kupiga mswaki vizuri na ku-floss(kutoa mabaki ya vyakula) kila siku.

Kwa sasa nenda kwa daktari wa meno wasafishe na ukirudi fuatisha hayo maelezo na jenga tabia ya kwenda kusafisha meno yako kwa daktari kila baada miezi sita.
---
Kuna dawa inaitwa Chlorhexamed, ni nzuri sana. Mimi pia nilikuwa na tatizo hilo nikaenda kwa dentist akaniandikia dawa hiyo. Nimeitumia mara mbili tu tatizo limeisha. iko kwenye tube ndogo kama zile za dawa za macho, na una massage ufizi kwa kutumia mswaki.

Ila pia kuna masharti: kila ukimaliza kula upige mswaki, na kabla ya kwenda kulala pia upige mswaki. Ukiweza kwenda kusafishwa meno kwa dentist pia itakuwa vizuri.

Ukiweza kupata dawa ya mswaki Parodontomax, ukaitumia pamoja na hiyo chlorhexamed basi utamaliza kabisa tatizo hilo.

Kila la heri.
---
Poleni sana,

Nami nilikuwa na hilo tatizo tena kidogo meno ya dondoke kwani halí hiyo ikiendelea mifupa ya kushikilia fizi hudhoofika hali upelekea meno kulegea, ikifikia hatua hii ma dentist hawatakushauri kusafisha badala yake watakupa dawa za kuimarisha mifupa (calcium) within a week then ndiyo watasafisha meno. Kama upo Dar, nenda pale mtaa wa Jamhuri karibu na kituo cha polisi kuna clinic ya meno ya muhindi mmoja wako vizuri sana.

Kwa wakati huu nakushauri nunua dawa ya meno inaitwa protector inaimarisha fizi, uvimbe na kuzua damu kubleed kwenye fizi ingawa haipatikani kwenye maduka mengi lakini ni nzuri sana ukiikosa nenda pale jamuhuri street. Mimi nipo poa sasa.
---
Kaka. Pole daaa kwanza nimecheka MKEREKETWA kanichekesha!! Kwanza kabisa kutoa damu katika fizi kunaweza tokea kama ! Kuna upungufu wa vitamin c ambazo zitafanya fizi kutokuwa na afya tosherevu

2: inaweza kuwa kwenye meno yako kuna vitu vinavyoitwa calculus , huu ni uchavu ambao hugandamana hasa sehemu ya shingo ya jino , na kuweka vitu vigumu vigumu na hata ukipisha ulimi vitu hvy huleta mikwaruzo,

Uchafu huo unapokuwa sehemu ya jino husababisha ( inflamation ) kuvimba kwa fizi kwani eneo hili huwa na damu nyingi ili kuilinda fizi kutokana na huo uchafu,

Na mara nyingi kunapotokea hali hii, mara upigapo mswaki damu hutoka kwa kiasi fulani , na si mswaki tu hata unapotafuna aina fulani ya vyakula vigumu damu huweza kutoka pia.

TIBA
Kama ni upungufu wa vitamin , utashauliwa kutumia matunda hasa ya vitamin c
2. :Na mara nyingine utapewa vitamic c vidonge ( ASCOBIC ACID)
3:Usafishwe fizi kama unauchafu huo ( calculus ) ugaga , pamoja na kupewa antiseptic mouth wash , eg hydrogen peroxide , linsterin, au medi oral .
4: Mwisho oral hygine instructions namna ya kuswaki , aina ya mswaki !!!!
 
Waweza kuwa ukisumbuliwa na magonjwa ya fizi, yapo ya kama aina mbili (kubwa):
1. Gingivitis
2. Periodontitis

Ni vema ukaonana na daktari wa meno kwa uchunguzi na ushauri wa kina:
Ila matibabu yatakuwa km hv tegemea na daktari wako atakavyoona tatizo.

1. Gingivitis - Oral hygiene instructions (toothbrush, brushing techniques, frequencies of brushing) & No medication prescribed for

2. Periodontitis-Oral hygiene instructions, scaling & rootplaning (SRP), and may be with some antibiotics + anagelsics

Take home message; fizi kutoka damu hakwendani na ukosefu wa vitamin C ktk masingira ya kitanzania....labda mfungwa au baharia anayekaa majini muda mrefu bila kupata matunda
 
naomba msaada wa kitaalamu, nini cha kufanya kuzuia damu kutoka kwenye fizi unapopiga mswaki.

Una Ukosefu wa vitamin C mimi nilikuwa nikiamka asubuhi nikipiga mswaki basi Damu inanitoka Mdomoni nikamueleza Docktor akaniandikia ninunuwe Dawa ya Multi Vitamini unakula kila kidonge kimoja kila siku baada kwisha kula chakula kwa muda wa siku 30.

Lakini kwa ushauri wangu uwe unakula matunda haswa machungwa unakamuwa pia malimau unati akidogo sukari uwe unatumia kila siku hayo matatizo yako yataondoka akipenda Mwenyezi mungu.
 
Ugonjwa wa ufizi huathiri ufizi na huweza kusambaa kwenye mifupa inayoshikilia meno. Hii ni mojawapo ya sababu ambazo hufanya watu kupoteza meno. Ugnjwa huwa katika hatua mbili lakini inapokuathiri waweza kutibu kabla ya kusababisha madhara

Ni nini baadhi ya dalili au ishara
Hatua ya kwanza ya ugonjwa huu wa ufizi huitwa gingivitis
Baadhi ya dalili/ishara ni pamoja na:
  • Ufizi nyekundu na iliyofura
  • Ufizi unaotoa damu unaposugua meno
  • Ufizi uliongoka kutoka kwenye meno
  • Harufu mbaya isiyoisha
Wanawake wajawazito kwa kawaida huathiriwa na gingivitis. Ukiwa mjamzito tunza afya yako ni vizuri ikiwemo meno.

Hatua ya pili ya ugonjwa wa ufizi huwa hatari sana.

Waweza kuwa na ishara/dalili zilizotajwa hapo juu
  • Usaha unaotoka kwenye meno na ufizi
  • Meno iliyolegea
  • Nafasi kubwa katikati ya meno mahali ambapo ufizi inapaswa kuwa
  • Kutokuwepo na tofauti katika mpangilio wa meno ukiyauma chini.

Unaitibu vipi?
Ukiwa na dalili zozote za hatua ya kwanza, sugua meno na utumie uzi spesheli kutoa chakula katika meno mara kwa mara na umuone daktari wa meno. Ukiitibu tatizi hili basi utazuia ugonjwa wa ufizi.

Ukiwa na dalili zozote za hatua ya pili, mwone daktari haraka iwezekanavyo. Meno yako yaweza kungoka au kungolewa na daktari wa meno ikiwa hutatibiwa mara moja. Ugonjwa huu ukiwa mbaya sana daktari wako wa meno anaweza kukuelekeza kwa daktari wa meno aliye na ujuzi wa ugonjwa wa ufizi.
 
Salamu waungwana madaktari.

Nna kabinti ka ndugu yangu naishi nako kana matatizo ya kutoka damu kwenye fizi za meno... kabinti kana miaka 17.

Akipiga mswaki damu inayotoka inatisha
Akimega tunda kama apple lazima damu itoke kwenye fizi
Yaani kila kinachofanyika mdomoni na kuhusisha matumizi ya meno asilimia kubwa damu lazima itoke kwenye fizi.

Kabla sijampeleka kwa daktari nimeona nipitie hapa kwenu wataalam mnisaidie labda kuna njia mbadala wa tiba bila kwenda hospitali.

Ahsanteni kwa kunielewa na kwa msaada wenu.
 
Mimi pia nilikuwa na hilo tatizo....nilienda kumwona dentist akanisafisha....meno yote akanipa dawa ya kusukutua na sasa ni fresh kabisa.

Tatizo ni kutu(yani kwenye meno na fizi zinapokutana kunatengeneza uchafu) kwahiyo wanakwangua kuondoa hiyo uchafu(inaitwa gangetivity-sina uwakika na ''spell''za neno hilo.
After every 6months unaenda wanakusafisha mpaka utakapo pona.

NB:Matatizo ya kinywa yana''side effect sana katika mwili wa mwanadamu,tena wanawake ndio wako''prone'' zaidi kuliko wanaume.Ni vizuri ukawahi Kwa Dentist.
 
Asprin,

Pole sana. Utapata maelezo mengi sana, lakini kimsingi unashauriwa umpeleke hospitali yoyote akaonwe na dentist.

Kwetu Afrika hatukimbilii sana kufikiria upungufu wa vitamin C mwilini, kwa sababu tunapata vitamin hizo kwa namna nyingi sana. Umeshasema akila tunda la apple anaacha damu, ina maana huyo anao uwezo wa kupata hata matunda aghali hivyo. Machungwa na mapera pia ni mfano mzuri wa chanzo cha vitamin C. Kwa hiyo ni bora kuondoa wazo hilo kabisa kwa sasa.

Hakuna kitu "KURTU" kwenye meno, kwani kutu ni zao la chuma (iron) kushambuliana na oxygen. Hakuna chuma cha namna hiyo kwenye meno. Kinachotolewa ni mwamba unaotokana (tartar au calculus) na mtu kutopiga mswaki meno yake ilivyo sawasawa na kuacha wadudu wazaliane juu ya masalia ya chakula katika aina ya utando kufunika meno, ambapo protein aina ya pellicle hufanya kazi kama cement au gundi kushikilia uchafu huo. Wadudu wanapenda kutumia masalia (au tabaka la) ya chakula kama raw material na kuzalisha tindikali ambayo hutelemsha tindikali ya mdomoni (pH) hata kusababisha meno kutoboka, lakini pia toxin ya harakati ya bacteria hao huumiza fizi taratibu.

Ukichelewa utakuta hata mfupa unaoshikilia meno unayeyushwa na meno kuanza kulegea kwa kukosa mahali pa kujishikiza. Palipo na calculus wadudu huwa attracted zaidi kukaa kwa sababu habitat yake huwafaa sana. Miamba hiyo ni ishara tosha kwamba hujapitisha mswaki eneo hilo kwa zaidi ya siku saba hata kama unapiga mswaki kila siku, maana yake hupigi ilivyo sawasawa kila eneo la jino. Daktari analazimika kukusafisha kwa kutumia vyombo maalum kwa sababu miamba hiyo haiondoki kwa kupiga mswaki wa kawaida. Huitwa SCALING.

Fizi zilizoathirika kwa kutopiga mswaki ilivyo sawasawa huwa na dalili nyingi, mojawapo ni kutoka damu hovyo hata kama zimeguswa kidogo tu, na utagundua unapopiga mswaki kikawaida unapotoka damu, ujue kuna eneo ndio kwanza limepata mwaki siku hiyo na fizi zinatoka damu. Hali hiyo huisha yenyewe kwa kuongeza bidii ya kupiga mswaki sawasawa kuzungukia meno yote mdomo mzima.

Dawa ya kusukutua anayokupatia sio badala ya kupiga mswaki, maana dawa hiyo haiondoi uchafu bali inafanya kazi ya kuwatibua bacteria wasitawale kwa kuzaliana baada ya wewe kufanyiwa usafi na daktari, kwani wadudu hupunguzwa kasi ya kuzaliana na hivyo kupunguza madhara kwa fizi.

Niseme kwa ufupi tu kwamba mpeleke mgonjwa kwa daktari aone hali halisi ilivyo na kuamua hatua bora ya kumsaidia mgonjwa wako. Inashauriwa mtu amwone daktari wa meno angalau kila miezi 6 kwa check up ya kawaida ili kushughulikia matatizo yoyote yanayojitokeza mapema kwenye fizi au meno.

Upigaji mzuri wa meno ni kila siku angalau mara mbili - BAADA ya kifungua kinywa asubuhi na kiwe ndio kitu cha mwisho kabla hujalala usiku kitandani ili kuhakikisha unadhibiti mioto ya bacteria. Sasa kupiga mswaki kabla ya kifungua kinywa ni hiari yako na sio vibaya, lakini sio sahihi kitaalam kwa lengo la kudhibiti wadudu kwa kuondoa masalia ya chakula. Ukiweza piga hata mchana. Hakikisha kila jino limepigwa mswaki sehemu zote. Huwezi kufanya hivyo kwa dakika tatu.

Itoshe kwa leo.
 
aspirin,sio matunda yote yana vitamin c kwa wingi.sour fruits kama machungwa na malimao na nanasi ndo yanafaa zaidi.mbogamboga za kijani ambazo hazijapikwa sana (yaani zinatakiwa kuwa kama zimepashwa tu..),otherwise kisamvu na mlenda hazina faida mwilini.

otherwise angalia mswaki anaotumia,inawezekana unamuumiza.meanwhile atumie mouthwash ili kuepuka bakteria wazengea kisusio mdomoni kwake.
 
Poleni sana,

Nami nilikuwa na hilo tatizo tena kidogo meno ya dondoke kwani halí hiyo ikiendelea mifupa ya kushikilia fizi hudhoofika hali upelekea meno kulegea, ikifikia hatua hii ma dentist hawatakushauri kusafisha badala yake watakupa dawa za kuimarisha mifupa (calcium) within a week then ndiyo watasafisha meno. Kama upo Dar, nenda pale mtaa wa Jamhuri karibu na kituo cha polisi kuna clinic ya meno ya muhindi mmoja wako vizuri sana.

Kwa wakati huu nakushauri nunua dawa ya meno inaitwa protector inaimarisha fizi, uvimbe na kuzua damu kubleed kwenye fizi ingawa haipatikani kwenye maduka mengi lakini ni nzuri sana ukiikosa nenda pale jamuhuri street. Mimi nipo poa sasa.
 
nafikiri mod ameshaona hilo tatizo.kidude cha thnx hakionekani kwa darubini wala miwani.
 
Back
Top Bottom