Kutokuwepo kwa Mabalozi wa US, UK, Sweden, Norway, Denmark, EU, Japan na South Korea leo Dodoma, kuna nini kinaendelea jikoni?

Kuna kitu nahisi kinakuja, na si cha kawaida kwa kweli. Sie tulioibiwa Uchaguzi nafikiri huu ni muda sahihi kuchukua popcorn na kuangalia huu mchezo unavyozidi kuwa mtamu

Kuchukua popcorn na kuangalia tu kama movie?!?! Watu wengine wa mabara mengine ndio wafanye jambo kwenye dhulma uliyofanyiwa wewe (huku wewe ukiwa unaenjoy ‘show’)??!! SMH
 
Wameshindwa kazi waliotumwa na serikali zao ya kuhakikisha janja janja ya wazungu inaota mizizi.
 
Tanzania ni tajiri, biashara ya kuwa watumwa kwenye nchi yetu iliisha tulipopata uhuru na JPM ameamua kuiondoa nchi hii kwenye utumwa mambo leo. Sasa kama kuna makuwadi wa hizo nchi walifikiria sisi ni shamba la bibi imekula kwao. Hapa kazi tu!

 
Kuchukua popcorn na kuangalia tu kama movie?!?! Watu wengine wa mabara mengine ndio wafanye jambo kwenye dhulma uliyofanyiwa wewe (huku wewe ukiwa unaenjoy ‘show’)??!! SMH
Kuna muda inafika lazima tufurahie external support. Kama sie wanatuua na kutubambikia makesi, acha wapambane na wababe wa dunia sie tufurahie
 
Wakati anahutubia na baada ya hotuba,mkulu hakuwa na uso wa bashasha,alionekana hana raha na mwenye feelings nyingi,japo mzee wa mjengoni na gwajboy walichombeza vijembe vingi kwa upande ule ulioshindwa lakini mkulu alikunja viganja vya mikono na kuonekana anaomba Mungu amsaidie kwa magumu yajayo.Kwa kweli politocal strategic iliyotumika kupata ushindi wa kimbunga dhamiri zao zinawahukumu mpaka wanakosa furaha na matokeo ya ushindi mnono

Furaha atakua awe nayo asilani kwa kuwa kapora ushindi

Angekua na furaha sana kama angeshinda kihalali hata kama ni ushindi mwembamba
 
Tutapata shida mimi na wewe, usitegemee viongozi kupata shida, hili jambo la kuchelea hata kidogo, mfano zimbambwe ilipobanwa, unafikiri mgabe alitapata shida kwa mahitaji ya kawaida?, Waliopata shinda ni wazimbambwe wa kawaida waliokua wanapata ration ya petrol
Bora tupate shida ili akili zitukae vizuri
 
Tanzania ni tajiri, biashara ya kuwa watumwa kwenye nchi yetu iliisha tulipopata uhuru na JPM ameamua kuiondoa nchi hii kwenye utumwa mambo leo. Sasa kama kuna makuwadi wa hizo nchi walifikiria sisi ni shamba la bibi imekula kwao. Hapa kazi tu!


Tangu lini tajiri akawa ombaomba??? Nyie ni malofa tu
 
Tanzania ni nchi huru, nchi ulizozitaja zina hiyari ya kuhudhuria au kutokuhudhuria.
 
Ila Saudi Arabia anaenda.
Kwani Saudi arabia wamechafua demokrasia?Wao katiba yao imepiga marufuku mambo ya vyama vya siasa,Tanzania katiba inaruhusu siasa za vyama vingi ila wapinzani wakifanya siasa wanakiona cha mtema kuni.Huo ndiyo tunaita ni uchafuzi wa demokrasia Tanzania.
 
Ha ha ha ha ha, haya bhana. Lakini tatizo wapinzani hawapo serious.
Ni haki ya kikatiba ya mpinzani kufanya siasa hata kama hayupo serious.Kwani katiba ya Tanzania inasema wapinzani walio serious pekee ndiyo wanaruhusiwa tu kufanya siasa na ambao hawapo serious wapigwe,wauawe,wateswe,wafungwe,etc kama tunavyoshuhudia sasa hivi?
 
Ni swali muhimu sana kwa mustakabali wa nchi yetu.

Amani iwe nanyi wadau!

Usiku wa Jana, Wakili Robert Amsterdam ameitaarifu dunia kupitia Twitter yake kuwa amefikia hatua nzuri kupeleka mashtaka katika mahakama ya ICC Uholanzi dhidi ya Magufuli na Serikali yake.

Leo alfajiri, Magufuli akateua mawaziri wawili -- wa Mambo ya Nje, na wa Fedha.

Muda mchache uliopita kwa mara ya kwanza, wawakilishi wa nchi zinazoisadia zaidi Tanzania kifedha na kimisaada yaani Marekani, Uingereza, Sweden, Norway, Japan, Ujerumani, Finland, Korea ya Kusini na Umoja wa Ulaya hawajaudhuria hotuba ya Rais Magufuli Bungeni.

Naomba mnaojua mtuelezee humu, kuna nini kinaendelea jikoni? Au ndo mambo yashakuwa mambo?

Naomba michango yenu!
Ya kwao yamewashinda wanaangaikaje na ya kwetu? Waambie wamarekani wakaondoe ubaguzi wa rangi uliokithiri kwako na makandokando mengi yanayofanywa na wazungu kwa watu weusi ambao ni wamarekani.
 
Yaani pamoja na matamko yote yale ya kutoridhishwa na namna Uchaguzi ulivyofanyika, ulitegemea waende pale kufanya nini?!

Nakuhakikishia, japo jiwe amejitutumua pale Bungeni, lakini "deep inside" anajua ameharibu, na sijui ataanzia wapi kuwatongoza wale Wazungu.
Hakuna kitu Kama hicho hata wakati tunaamua kuanza ujenzi wa bwawa la kufumua umeme la Mwl Nyerere mlisema hivyo hivyo na hakuna lolote.Waambieni hao mabwenyenye Tanzania ni nchi huru inajiamulia Mambo yake yenyewe.Rais Trump analalamika kuibiwa kura na kuhujumiwa kwenye uchaguzi katika mazingira hayo analalamika kwa kusema uchaguzi haukuwa huru na wa haki. Waambie wamarekani ya kwao yamewashinda kamwe hawataweza ya watanzania Mungu tuliyenae ni Mkuu kuliko wanavyofikiri ndiyo maana hata ugonjwa wa Corona kwetu hakuna
 
Balozi mwenye akili timamu hawezi kuja kwenye uchafuzi wa demokrasia
Niambie Ni Chama gani Cha upinzani Kuna demokrasia? Niambie viongozi wa vyama vya upinzani na wagombea Ubunge wa majimbo na vitimaalumu kwenye hivyo vyama vya upinzani wanapatikana kwa namna gani?Kama si kuteuana tu kwa kujuana,Rushwa na uhuni. Sasa Kama umeshindwa kujua demokrasia iliyopo kwenye vyama vya upinzani huwezi kujitambua wewe bilashaka wewe ni GUNZI
 
Back
Top Bottom