Kutokuwa na Civil War kumesababisha wa-Tanzania kuwa watu wenye amani

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
50,323
2,000
Jana nilikuwa ninasafiri nilikaa kiti kimoja na mkaka wa ki-Nigeria katika maongezi aliniambia alikuja Tanzania kwa shughuli za biashara. Ukarimu aliokutana nao Tanzania anasema hata usahau. Kila aliyekutana nae alikuwa mcheshi na mkarimu.

Anasema gharama za hoteli alizojipigia kwa wiki mbili hakulipa kwani wenyeji wake walimkaribisha nyumbani kula na kulala bure kwa wiki mbili.

Mwisho alisema nyinyi mna amani kwakuwa hamjapigana vita ya wenyewe kwa wenyewe. Je kuna ukweli hapa?
 
Mkomavu

JF-Expert Member
Jan 25, 2016
10,816
2,000
Ninadhani hizi taarifa za ubadhirifu na ufisadi zinazifikia watu kwa njia ya mass communication hairatyacha salama ukizingatia watu wameshakata tamaa ya maisha
Ukweli ndio huo mkuu watu washachoka ila wanavuta muda tu
 
Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
8,770
2,000
Kupigana wenyewe kwa wenyewe inaweza kuwa kiashirio cha kuchukiana. Upendo baina yetu, tunauonesha hata kwa wageni.
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
15,642
2,000
Kitu kinachoweza kusababisha watu kupigana ni aidha DINI au KABILA, Kwa kabila Tanzania haiwezekani labda mtu atumie dini ingawa pia siyo rahisi kulingana na misingi iliyowekwa
 
Automata

JF-Expert Member
Mar 3, 2015
2,757
2,000
Jana nilikuwa ninasafiri nilikaa kiti kimoja na mkaka wa ki-Nigeria katika maongezi aliniambia alikuja Tanzania kwa shughuli za biashara. Ukarimu aliokutana nao Tanzania anasema hata usahau. Kila aliyekutana nae alikuwa mcheshi na mkarimu.

Anasema gharama za hoteli alizojipigia kwa wiki mbili hakulipa kwani wenyeji wake walimkaribisha nyumbani kula na kulala bure kwa wiki mbili.

Mwisho alisema nyinyi mna amani kwakuwa hamjapigana vita ya wenyewe kwa wenyewe. Je kuna ukweli hapa?
Naona ulisahau kumwambia kwamba si Tanzania yote yenye amani
Mkuranga na Rufiji ni kama Maiduguri (Northern Nigeria) kuna snipers wa hatari hadi raia kulazimika kulala saa kumi na mbili
Teh! Teh! Teh!
 
SK2016

JF-Expert Member
Apr 6, 2017
7,968
2,000
Tumshukuru Mungu kwa kutopigana wenyewe kwa wenyewe.
Lakini vita tuliyonayo haiwezi kutuacha salama.
 
Erickford4

JF-Expert Member
May 22, 2017
1,139
2,000
Kutokupigana ndio amani yenyewe kwa sababu tuliishi kwa amani na upendo toka zamani na hatukupenda kusuluhisha matatizo yetu kwa vita. Ndio maana tuna amani hadi leo
 
Waberoya

Platinum Member
Aug 3, 2008
15,108
2,000
Jana nilikuwa ninasafiri nilikaa kiti kimoja na mkaka wa ki-Nigeria katika maongezi aliniambia alikuja Tanzania kwa shughuli za biashara. Ukarimu aliokutana nao Tanzania anasema hata usahau. Kila aliyekutana nae alikuwa mcheshi na mkarimu.

Anasema gharama za hoteli alizojipigia kwa wiki mbili hakulipa kwani wenyeji wake walimkaribisha nyumbani kula na kulala bure kwa wiki mbili.

Mwisho alisema nyinyi mna amani kwakuwa hamjapigana vita ya wenyewe kwa wenyewe. Je kuna ukweli hapa?

ni kweli, hata kuto endelea pia ni kwa sababu hatujawahi kupigana!!

huwezi kukuta mahali lichama lina tuhuma zote zote zote za nchi hii, bado wakaendelea kutembea mtaani na nguo za kijani na njano!! nakuambia hata Yanga wangebadili rangi ya jezi yao
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
50,323
2,000
ni kweli, hata kuto endelea pia ni kwa sababu hatujawahi kupigana!!

huwezi kukuta mahali lichama lina tuhuma zote zote zote za nchi hii, bado wakaendelea kutembea mtaani na nguo za kijani na njano!! nakuambia hata Yanga wangebadili rangi ya jezi yao
Na wezi wana guts ya kutuita wapumbavu na malofa
 
Menyainganyi

JF-Expert Member
Mar 12, 2013
1,172
2,000
Kitu kinachoweza kusababisha watu kupigana ni aidha DINI au KABILA, Kwa kabila Tanzania haiwezekani labda mtu atumie dini ingawa pia siyo rahisi kulingana na misingi iliyowekwa
Mkaruka,

Kuna kabila baya sana Tanzania sasa hivi, hili lina uhai wa miaka kama miaka 40 hivi hapa Tanzania . .

Hila kabila ndio linalotawala sasa, na haliamini mtu yeyote nje ya kabila lao kuwa anaweza kuongozaTanzania . . KABILA HILI NDIO LIMEJIFANYA KATIBA YA NCHI . . !

Lakini pia kabila hili ndilo linalochochea utengano, udini, na ukabila.
Hila kabila kwa kufikiri Tanzania ni mali yao, limegawa kwa wageni (wao wanawaita WAWEKEZAJI) bure (dhahabu, gesi, chuma, mafuta etc) rasilimali za watanzania . .

Nakwambieni wana JF, bila kuling'oa hili kabila ktk kutawala, MACHAFUKO HAYAEPUKIKI . . !
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom