Kutokuwa na Ajira, nini sababu Kwa Vijana Wa kitanzania

Jamii imetufundisha kitu kimoja. -soma-faulu-soma-faulu-ajiriwa.

Hili ni tatizo sugu, ikitokea mtu akafeli, anahisi ndio mwisho wa kila kitu. Na ikitokea mhitimu akakosa ajira inakuwa ni kasheshe.
 
Elimu ya kwenye vyeti ni tatizo kubwa sana hili suala hutaliamini ila nakuhakikishia wasomi wengi wa kitanzania wanakosa ajira hapa namaamisha kujiajiri na kuajiriwa pia,,,ni kama wiki mbili zilizopita ofisin kwetu tulikua tunahitaji wanne mabinti watatu mwanaume mmoja ila kubalance gender kwan waliopo wote ni vidume nikaanza kutangaza hyo kazi ilikuwa ni post ya afisa mauzo kwenye bank kubwa tu nilibahatika kupata CV za wasichana wawili walikuja ofisin nikapannga siku ya interview huwezi amin nlpoanza kuwaeleza job description kuwa watakua wanaenda kutafuta wateja kwenye makampuni kwa ajili ya mikopo na accounts then watakuwa wanalipwa kwa commission na mtu una uwezo wa kujilipa hadi million tano it depends na volume ya mikopo yako...wakawa inspired sana walipoanza kazi ndo vituko sasa wanakwambia mm na degree yangu nianzu kuzurura juani kama machinga hawakudumu hata mwez wakakmbia..
Nilinote kitu hizi taalum za kwenye makaratasi ni upuuzi sana znafanya tusiwe committed,tuwe na negative mindset juu ya kaz fulani
Mkuu nipe kazi hiyo mimi aisee hautajutia
 
The struggle is real wazee usiombe utoke familia duni usome weee afu ukose kazi...
Kazi ukose afu utafute mtaji kibishibishi ufanye kujiajiri sawa unajua kasheshe linakuja wapi? Ukipata hasara kurudi tena kwny game majaliwa mana kipato huna cha kukusimamisha upya usione watu wanajaa kwny intavuu changamoto za kujiajiri si mchezo...
Mana kwny biashara pia you can win or lose
 
Vijana wa Leo hii in woga wa kazi mfano alietoka Chuo kikuu kupiga zege au kusukuma toroli hawezi.
 
Vijana wa Leo hii in woga wa kazi mfano alietoka Chuo kikuu kupiga zege au kusukuma toroli hawezi.
Wakati nasubiri matokeo ya form four nilifanya kazi kama gardener nikaja nikafanya kazi ya ufundi seremala.
Wakati wa kusubiri matokeo ya kidato cha sita nilikua saidia fundi ujenzi na tiles.

Hizi kazi haziji mara kwa mara halafu malipo yake siyo makubwa. Na wakati unavyosogea ndiyo majukumu yanaongezeka.

Mnatulaumu bure.
 
Tangu nilipoona uteuzi wa mkuu wa wilaya kisarawe na jinsi mteuliwa alivyoshukuru huko insta ndipo nilipojua vijana wengi ni jobless hii nchi
 
Back
Top Bottom