Kutokutoa 'siri za serikali'; Je, watanzania waendelee kuona nchi ikiangamia?

Patriote

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
1,718
1,047
Hapa nchini kwetu imekuwa ni jambo la kawaida kwa watawala wetu/serikali yetu kutaka kuwaziba midomo watumishi kutotoa "siri" za serikali kulingana na sheria zilizopo. kwa bahati mbaya, mara nyingi "siri" zinazoongelewa huwa ni zile zilizogubikwa na utata na harufu ya ufisadi.

Kwa mfano, Jana (tar 23/08/2011) Katibu mkuu kiongozi, Bw. Philemon Luhanjo aliwaonya watumishi wa Serikali wanaotoa siri huku akisema kufanya hivyo ni kuvunja kiapo cha kutunza siri za Serikali. Luhanjo alisema, “Nawaonya watumishi wa umma wanaotoa siri za Serikali…, tutafuatilia tujue nani alitoa barua iliyoandikwa na Jairo kuzitaka idara zilizo chini ya wizara husika kuchangia tsh mil. 50 kila moja ili kuwezesha bajeti ipite, akipatikana atapewa adhabu.

Hoja yangu ni kwamba, anachatoka Luhanjo na Serikali ni kuwafanya watumishi kutotoa taarifa ya namna nchi yetu inavyohujumiwa au ni taarifa gani za siri anazozizungumzia??Na je kwa kufanya hivyo, lengo ni kuisaidia nchi au kuiangamiza?? Mi nadhani Tanzania ni yetu, itabaki kuwa Tanzania hata kama utawala/uongozi wa nchi utabadilika, binafsi sioni kosa mana Nchi kwanza, then serikali na mambo mengine yafuate.....
 
Hapa ishu ni kutengua hicho kipengele kwenye katiba mpya. Huo usiri wa nyaraka ndo wizi wenyewe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom