Kutokutiwa nguvuni Tundu Lissu kesho 27/7/2020 ni kutangaza uasi juu ya Sheria za Nchi yetu

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
1,406
3,967
Yafuatayo yafanyike baada ya kutua uwanja wa ndege JKNIA

Kumnyang'anya passport ya kusafiria mara moja na jina lake liwe blacklisted kwenye mfumo wa waombaji Passport uhamiaji yaani yeye asije tena kupewa passport ya kusafiria maisha yake yote

Uchunguzi wa shambulio lake uanze Mara moja siku hiyo hiyo maafisa wa vyombo vya dola wamuweke kizuizini mpaka dereva wake aje ili utaratibu wa kisheria wa kesi yake uanze

Kwa sababu alikuwa na kesi mahakamani na hajatii masharti ya dhamana na yeye ni mwanasheria na anajua athari za kuruka dhamana basi aende mahabusu mpaka kesi yake itakapoisha

Dola ikiamuru Chama cha CHADEMA kumvua uongozi alionao Mara moja kwa sababu uongozi wa chama cha siasa ni Mali ya umma kwa hiyo yeye ni kiongozi wa umma na amekiuka masharti ya viongozi wa watumishi wa umma
 
Passport ni haki ya kikatiba kwa kila raia (Hata alieua), hakuna sheria ya kukataza mtu asiombe passport (Ila kuna mazingira ambayo mamlaka wanaruhusiwa kuzuia tu kwa muda passport ya raia kwaajili ya upelelezi au kuwekea dhamana)

Pili, kuna wakati jeshi la polisi linapaswa kutumia "BUSARA" katika utendaji wake wa kazi, hata kama mtu ana "ARREST WARRANT/HATI YA KUKAMATWA" ya kukamatwa kwake, ila jeshi la polisi linatakiwa kutumia busara kwenye mazingira ya kumkamata (Sio kumkamata muda wowote tu kwa kutumia nguvu/mamlaka bila kuangalia mazingira kama ni rafiki), kuna mazingira hayaruhusu jeshi la polisi kumkamata mtuhumiwa (Mfano, mazingira yanayoweza kuhatarisha AMANI ya NCHI na MAISHA ya RAIA/ASKARI WENYEWE)

Ombi lako la kukamatwa Tundu Lissu linaashiria unataka kuchochea MACHAFUKO kesho yatokee, raia wapate TAHARUKI, AMANI ivunjike na RAIA wapoteze maisha au waumizane.
 
Yote hayo umeyasema bila kutaja ata kifungu kimoja ya sheria aliyovunja kuhusu passport na uhamiaji. Kweli mme wako anavumilia mengi.
Usiwe na wasi wasi atakamatwa tuu kama raia wengine wanavyokamatwa na bado nchi itaendelea kuwa salama sheria haina huruma kabisaa usipande matikiti utegemee kuvuna maharage.
 
Wewe jaribu uone moto utarudi chattel na singilend, wakati huo sisi wananchi tutakuwa pembeni kuwaangalieni mnavyofanywa na mabeberu
Usiwe na wasi wasi atakamatwa tuu kama raia wengine wanavyokamatwa na bado nchi itaendelea kuwa salama sheria haina huruma kabisaa usipande matikiti utegemee kuvuna maharage
 
Na bado...Lisu akitua lazima uokote makopo kabisa toka Lumumba hadi Chato
Usiwe na wasi wasi atakamatwa tuu kama raia wengine wanavyokamatwa na bado nchi itaendelea kuwa salama sheria haina huruma kabisaa usipande matikiti utegemee kuvuna maharage.
 
Back
Top Bottom