KUTOKUPATA MISHAHARA KWA WAKATI..Je, kuna anayebisha kuwa Serikali ya JK haijafilisika KIUCHUMI?

Mr. Clean

Senior Member
Aug 7, 2006
194
44
LEO JIONI JAMAA YANGU YUPO WIZARA YA MAGUFULI KANIAMBIA WAMEKUA OMBAOMBA,

HAWAJAPATA MISHAHARA YA MWEZI NOVEMBER KITU AMBACHO HAKIJAWAHI TOKEA!

nimemwambia pamoja na kutokupata mishahara lakini nawapongeza kwani wanaadhimisha miaka 50 ya uhuru kwa kuwa ombaomba lakini pia
hongera zaidi kwani tarehe 9 dec, 2011 watakuwa uwanjani wakiwa wamevaa nguo za kijani na njano wakitembea gwaride na kubeba mabango ya kuisifia serikali ya jk!

wakumbuke kuwa hela zao za mishahara zimekwenda kukimbiza mwenge wa uhuru, kuandaa malazi, kuandaa chakula cha wageni pia kutoa viburudisho kwa wageni siku ya 9 disemba. si wajua babalegelege hukopa hela ili kufanya sherehe watu wale, wanywe, waserebuke?
 
Nyingine zimeongeza posho za waheshimwa waabudiwa!Miungu watu kwa jina la wabunge.
 
si wizara ya magufuli tu ila hata wizara ya afya nao hawajapata mishahara ila wanasheherekea maazimisho kwa mbwembwe ile mbaya, kuna jamaa tumekutana ATM NBC asubuhi akidhani wamewekewa mshahara na alikuwa na madeni ya ajabu, baada ya kukuta mshahara haujaingia akaondoka na maneno kibao. kweli tunakoelekea si kuzuli
 
CCM OyEEEEEEEEEE!
Tumejaribu, tumeweza na tunasonga mbele katika kuyafanya maisha ya mwananchi wa kawaida yawe magumu zaidi
 
Kweli kabisa mimi mpk saiv nimepita mlimani city ATM,shimo bado halijatema! Kikwete pay us! Mzuixxxxxxxxxx
 
Si hao tu ni tatizo la wizara zote, wengi hawajapata bado mshahara.
 
wengi wetu HATUJAPATA hadi sasa ninapopost mie nasikilizia maumivu tu! Kibaya zaidi hakuna taarifa yoyote
 
Na hata unapotoka mbona unakuwa umekatwa? Hii inasikitisha sana kijimshahara chenyewe hata posho anayolipwa mbunge kwa siku1 hakifiki, na bado mnakipiga panga! Lo..shem on u.
 
Back
Top Bottom