Kutokunywa maji ya kutosha husababisha kuvimbiwa (constipation)

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
20210403_123606_0000.png

Kuvimbiwa ni ile hali ya mtu kupata haja chini ya tatu kwa wiki au haja kuwa ngumu.

Hali hii hutokea wakati utumbo mpana unaponyonya sana maji kutoka kwenye kinyesi na kukifanya kuwa kikavu na kupelekea kuwa ngumu kutoka nje.

Sababu za kuvimbiwa ni pamoja na:-

Kutokula vyakula vya nyuzi nyuzi kama vile matunda na mbogamboga.

Kutokunywa maji ya kutosha.

Kutofanya mazoezi

Msongo wa mawazo

Kubadilisha mizunguko ya kawaida ya maisha kama kusafiri au kubadilisha muda wa kulala.

Dalili za kuvimbiwa(Constipation) ni pamoja na:-

Kupata haja chini ya mara tatu kwa wiki

Kuwa na kinyesi kikavu, kigumu na kinatoka kwa vitonge na huwa ni vigumu kutoka.

Maumivu ya tumbo, uchovu na kichefuchefu.

Kuhisi kuwa hujamaliza haja lakini ukijaribu kutoa haitoki.

Watu wa umri wowote wanaweza kupatwa na kuvimbiwa mara kwa mara. Isipokuwa kuna watu au hali ambazo zina uwezekano mkubwa wa kusababisha kuvimbiwa zaidi. Hii ni pamoja na:-

Wazee huwa hawana nguvu za kutosha, mifumo yao ya umeng'enyaji wa chakula ni dhaifu hali inayopelekea kuvimbiwa mara kwa mara.

Mwanamke, haswa wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua. Mabadiliko katika homoni za mwanamke huwafanya kukabiliwa zaidi na kuvimbiwa. Mtoto ndani ya tumbo hugusa utumbo na kupunguza kasi ya kupita kwa kinyesi.

Ili kuondoa tatizo la kuvimbiwa unashauriwa kunywa maji ya kutosha kila siku, kula matunda kama Papai, mbogamboga na tende au juisi yake na kufanya mazoezi.
 
Ahsante kwa kutukumbusha.
 
Kuna gazeti la Mwananchi lilimnukuu Dr mmoja hivi akisema kunywa maji mengi ni hatari kwa Afya,hii dunia kuna tafiti zinakinzana sana
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom