Kutokujua sheria sio utetezi popote, ukijua umevunja sheria usiseme kuwa hukujua kama ni kosa

Mgeni wa Jiji

JF-Expert Member
Jul 27, 2017
7,905
13,366
Habari wana JF.

Huu mwaka nimedhamiria angalau kwa kila wiki niwe naweka uzi mmoja unaohusu swala la kisheria.

Nimeamua hivyo baada ya kuona changamoto nyingi sana za kisheria zinazoikumba jamii yetu, sio rahisi kufikia kila mtu lakini bora kidogo kuliko kukosa kabisa, basi nitatumia zaidi JF kuweka mchango wangu kwenye huu ulimwengu wa sheria.

Nitakayokuwa naandika huku sio ushauri rasmi na wala sijalenga yatumike hivyo.

Basi, leo ikiwa ni mwanzo wa safari yangu hii kwa mwaka 2023 nitaanza na hili swala la ULAZIMA WA KUZIFAHAMU SHERIA ZA NCHI, ndio sheria za Tanzania zinatambua kuwa wewe mtanzania unazifahamu.

Hapa unaweza ukajiuliza kivipi mimi nazifahamu au nalazimishwa kuzifahamu?, jibu ni rahisi kabisa na jibu ni kuwa KUTOKUJUA SHERIA SIO UTETEZI, hili ndio jibu.

Kwa kufafanua ni kwamba kama utakamatwa au kutuhumiwa kufanya jambo fulani na ukafikishwa Mahakamani na kujitetea kuwa HAUKUJUA KAMA HILO JAMBO NI KOSA KISHERIA basi fahamu kuwa Mahakama haitazingatia kabisa huo utetezi wako na hapo kiufundi (kwa mazingira mengi) utakuwa umekiri kufanya kosa hivyo utahukumiwa endapo Mahakama itajiridhisha.

Kwa hiyo basi kama kutokujua sheria sio utetezi nifanye nini pindi ninapojikuta matatani?, ushauri mzuri ni kuwa endapo utajipata matatani na vyombo vya dola na kufikishwa Mahakamani na kwa bahati mbaya hauna uwakilishi wa wakili, kamwe usiseme kuwa HAUKUJUA/KUFAHAMU KAMA NI KOSA.

Badala yake jitetee kwa namna tofauti na hii ya kuwa mjinga wa sheria.

Kwa leo nina haya machache ya kuwajuza ndugu zangu, kama kutakuwa na swali naomba liwe na uhusiano na uzi huu ili kuweza kupata mtiririko wa pamoja. Ikiwa una swali lisilohusiana moja kwa moja na uzi huu pia usisite kuuliza lakini tambua kuwa majibu yake yatategemea aina ya swali ulilouliza.

Ahsanteni
Na
Jioni njema kwenu.
 
Asante sana,je nijitetee kwa namna ipi naomba mfano
 
Mfano rahisi ni kukataa mashitaka/makosa. Kwasababu mshitaki/jamhuri anatakiwa kuleta ushahidi ili kuthibitisha kuwa ulifanya hilo kosa, atakupanafasi ya kuuliza maswali mashahidi kwa lengo la kuwekamashaka juu ya ushahidi wao.

Mfano, umetuhumiwa kwa kosa la kuuza chenchi/hela. Usije ukasema kuwa ulikuwa hujui kuwa ni kosa kisa unaona watu stendi wakiuza chenchi na hawashikwi badala yake wewe kataa kuwa hujawai fanya iyo biashara ikiwezekana pakatae na eneo linalotajwa kuwa umefanya hiyo biashara haramu ya kuuza chenchi.

Ika unapokana uwe na mahesabu ya kudili na mashahidi vyema.
 
Mkuu ahsante pia ukiweka uzi humu wa sheria nitag
 
Back
Top Bottom