MTV MBONGO
JF-Expert Member
- Feb 18, 2016
- 1,261
- 1,222
Kesi mbili zimenivutia na ninawasilisha kuwafanya muwe makini katika uwajibikaji na kufuata sheria za nchi:
1. ilinishangaza sana kusikia maamuzi ya mahakama ya kisutu majuma machache yaliyopita pale kampuni ya Tigo ilipoamriwa kuwalipa wasanii AY na MWANA FA sh. Bilioni 2 kwa kutumia miito ya nyimbo za 'usije mjini' na 'dakika moja' bila ridhaa ya wahusika. najiuliza mahakama imekubali pesa nyingi namna hiyo kwa nyimbo 2 kwa vigezo gani? je, wakiuza albam nzima wanapata hata nusu ya hela hiyo? kama ingekuwa hivyo nchi nzima tungekuwa wasanii. naona sio haki japo nao TIGO wawe wanaheshimu kazi za usanii. wangepewa kiasi fulani kinachokadiria mapato ya nyimbo 2 walau.
2. juzijuzi FASTJET wameamriwa na mahakama kumlipa wakili wa mahakama kuu sh. mil. 30 kwa usumbufu wa kuahirisha safari bila ya kumtaarifu. wakili aliomba mahakamani sh. mil. 50 ila mahakama ikasema ni nyingi mno. busara hii nimeimpenda, inamwadabisha FASTJET bila kumkomoa ila ile ya TIGO nasema sio busara sio HAKI nahisi harufu ya RUSHWA!