Kutokomezwa kwa corona virus itategemeana sana na ukomavu wa viongozi wetu

goldcall

JF-Expert Member
Oct 20, 2017
394
535
unajua kama viongozi wetu walizalau covid-19 ilipo kuwa inaingia nchini,mipaka na airport ziliendelea kufanya kazi, viongozi wachache wakatumia covid kama siasa na kushindana na kukashifiana, na hawa ndio viongozi wetu, wenye uelewa na ufahamu wa aina hiyo! ninapata ukakasi kuamini suruhisho la hili jambo naona kabisa hili janga linasambaha kirahisi, lakini halitaondoka kirahisi ifahamike hivyo.

kwa baadhi ya viongozi wetu wenye dhamana kwa namna hili janga linavyo chukuliwa na aina ya mikakati inavyo pelekwa,naona corona itapiga kambi bongo na kuondoka itatusumbua sana, viongozi wenye dhamana, badilisheni mtazamo,hili ni janga tena janga kubwa, ukizingatia janga halina tiba wala kinga, mbaya zaidi hili janga linapiga yeyote, mtoto, kiongozi, waziri, na wengine wengi.

imeisha...
 
Ukiwa kama kiongozi kabla ya kutoa tamko litafakari kwanza. Unaposema kila mwananchi lazima avae barakoa kabla ya kutoka nje ya nyumba yake

1. Fahamu kuwa watu unao waongoza ni wa aina tofauti. Wengine hawafahamu barakoa ni kitu gani.

2. Fahamisha matumizi sahihi ya barakoa na uvaaji sahihi. Barakoa inatakiwa izibe kuanzia chini ya macho mpaka chini ya kidevu. Uvaaji usio sahihi bado unakuacha kwenye hatari ya maambukizi.

3.Fahamisha watu watakapoweza kupata barakoa na bei yake.
 
Nina wasiwasi Korona itatuua sana Tanzania kuliko kipindupindu, HIV-Aids na hata town. Naona kama kumekuwa na ubabaishaji sana katika kusimamia janga hili.

Viongozi wa serikali msifanye mchezo wa kufurahisha watu kuwa maisha ni kama kawaida. Trump alifanya hivyo akaiingiza Marekani katika Janga. Viongozi kuweni seriousi na gonjwa hili ambalo ni tofauti kabisa na HIV ambayo mtu alikuwa anaweza kujitunza asiipate kabisa, lakini gonjwa hili halina cha kujitunza; ukiingia mitaani tu linakuzoa.

Fundisheni watu seriously, siyo hii ya lele mama. Tanzania tumewahi kuumizwa na milipuko ya kipindupindu, HIV-AIDS lakini yote hayo yalikuwa yanategemea matendo yako mwenywe; hili jipya halitegemei matendo yako kabisa bali ni exposure tu. Kqwenye daladala, sokoni, mitaani, madukani na sehemu zote za watu wengi utalizoa.

Tusidananyike kuwa barakoa ndiyo dawa, hapana, hiyo inasaidia kwa kiwango kidogo sana. Kwetu nchi ya jasho, unaweza kuwa na barakoa ukazoa hiyo virus kwenye jasho lako na kubeba wakati unafuta jasho.
 
Unataka wafanye nini?

Sent from my SM-A720F using Tapatalk

.....wachukue hatua zozote za kuzuia usambaaji wa gonjwa hilo; kwa mfano kwa vile sasa hivi imeonekana wazi kuwa kuna maambukizi ya ndani kwa ndani, siyo yale ya watu waliotoka nje tena, basi wazuie mizunguko ya watu mitaani. Jinsi gani watafanya hivyo, mimi sijui kwani wao ndio wanaolipwa na wana nyenzo za kufanya kazi hiyo.
 
Watanzania mna penda sanaa kulalamika vitu ambavyo hamvielewi..
Jamaa hapo kakuuliza serikali ifanye nini.
"UNAJIBU HATA WEWE HAUJUI ".
hivi unadhani magufuli anapenda ugonjwa uendelee?.
.....wachukue hatua zozote za kuzuia usambaaji wa gonjwa hilo; kwa mfano kwa vile sasa hivi imeonekana wazi kuwa kuna maambukizi ya ndani kwa ndani, siyo yale ya watu waliotoka nje tena, basi wazuie mizunguko ya watu mitaani. Jinsi gani watafanya hivyo, mimi sijui kwani wao ndio wanaolipwa na wana nyenzo za kufanya kazi hiyo.

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
 
Watanzania mna penda sanaa kulalamika vitu ambavyo hamvielewi..
Jamaa hapo kakuuliza serikali ifanye nini.
"UNAJIBU HATA WEWE HAUJUI ".
hivi unadhani magufuli anapenda ugonjwa uendelee?.


"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
Kwani serikali haioni nchi nyingine ambazo zinafanya kupunguza maambukizi na zimefanikiwa?
 
Wewe uliyeona SI U TUAMBIE WAMEFANYA NINI?
Na nchi zipi hizo?
Kwani serikali haioni nchi nyingine ambazo zinafanya kupunguza maambukizi na zimefanikiwa?

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
 
Kichuguu mkuu wangu, tatizo letu wa TZ ni kuogopa kusema ukweli na kujawa na unafiki.
Bila kumuambia bwana mkubwa kaa pembeni kwa hiari uachie ofisi umeshindwa hakika tutateketea tunajiona au shurti itumike alazimishwe kwa kukosa imani.

Huyu bwana anaendesha mambo mengi kwa mizaha na ukali upo pale tuu pasipo na sifa binafsi.

Watu wanadhani katia woga katika utendaji kumbe katia woga katika uteuzi, watu wanaogopa kupoteza nafasi sio kupoteza weledi.

Corona imechukuliwa kizembe sana hapa kwetu tena kuliko Italy au US na hata matokeo yanafichwa utadhani kwa kufanya hivyo ndio wanakinga wengine.

Hatua ya mwisho eti tuombe kama taifa! Hivi hill huwa in agizo LA Rais au viongozi wa kiroho ndio wajibu wao? Na walikuwa wanatuhimiza na tunafanya kila siku.
Lakini kasema yeye kumbe hizo siku tatu zimekuwa sio za kumtukuza na kumuomba Mungu bali kumsifu yeye na kumtukuza kwamba ndiye kiongozi wa kipekee duniani mwenye majibu ya corona.

Nini hii?? Tuambiane ukweli, Magufuli ashukuriwe kwa yote aliyofanya kama mtumishi wa umma lakini aambiwe apumzike. Tena hakuna haja ya kusubiri October, aache Mama Samia awe acting hadi uchaguzi vinginevyo tunaweza kuyapata ya Italy na kusaga meno. Kwani lazima awe yeye hata kama kafeli?
 
Wewe uliyeona SI U TUAMBIE WAMEFANYA NINI?
Na nchi zipi hizo?

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
Nacho kiona unataka kuleta ujuaji? We unadhani serikali na jopo zima la wataalamu iliyonao hawafuatilii takwimu toka mataifa mbali mbali zinavyokwenda?
 
Watanzania mna penda sanaa kulalamika vitu ambavyo hamvielewi..
Jamaa hapo kakuuliza serikali ifanye nini.
"UNAJIBU HATA WEWE HAUJUI ".
hivi unadhani magufuli anapenda ugonjwa uendelee?.


"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"

Usinitumbulia macho mzee wangu, mimi sina raslimali walizo nazo viongozi kuweza kuwapa maagizo ya kutekeleza; watu wa aina yako ndio huwa mnataka kuwafundisha viongozi hatua za kuchukua bila kujua kama raslimali walizonazo zinatosha kufanya hivyo.

Mimi nimeongelea tatizo kubwa la kutokudanganya umma na kuwataka waache kuwapa wananchi matumaini potofu bali wajenge mazingira ya kuzuia usambazaji miongoni mwa wananchi hasa kuzuia misongamano; sasa wao watajenganje mazingira hayo, hiyo inatokana na madaraka yao ambayo sijui mipaka yake.

Kuwaaminisha wananchi kuwa kila kitu kiko sawa bali vaeni barakoa tu mkiendelea na maisha yenu ya mtaani kila siku ni kudanya umma kabisa.
 
Back
Top Bottom