Kutokomeza ujangili; Tujuzane hapa soko la bidhaa zitokanazo na wanyama pori na njia ya kuzitokomeza

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Kuna watu hamjui thamani iliyomo kwenye hifadhi ya taifa, wanyama na misitu!! Kwa mfano ikiwa;
  • Kipande cha jino la tembo thamani yake unapata vitz au subaru kutoka japani
  • Kilo moja ya nyama ya simba inafikia hadi 200000 (laki mbili)( wazungu wanakula)
  • Kilo moja ya nyama ya mamba inakaribia dola $300-400
Kwa mifano hii michache, mtaelewa thamani iliyopo msituni ni kubwa sana kiasi kwamba ikisimamiwa vizuri wizara ya maliasili pekee inauwezo Wa kulipa nusu ya bajeti ya serikali!
Kupambana na ujangili si suala dogo inatakiwa uwe mzalendo kwelikweli,
TANAPA hawana uwezo Wa kutokomeza ujangili ukiachilia mbali vifaa duni walivyo navyo pia mazingila ya rushwa kwao ni vishawishi vikubwa!
Pamoja na kwamba walinzi Wa TANAPA wanalipwa mishahara mikubwa pengine hadi 2mil Kwa mwezi lakini hiyo haiondoi hali yao ya kutaka zaidi Kwa kupokea chochote na sababu kubwa wanakaa mda mrefu kiasi kwamba wanafahamiana na majangili.

USHAURI WANGU

  • Serikali itengeneze sheria ngumu, Vifungo vya maisha au miaka thelathini viletwe huku.
  • Zifungwe wireless camera maeneo yote ya hifadhi ili kuboresha ulinzi Wa TANAPA Kwa ndani halafi nje ya hifadhi walinde wanajeshi
  • Chopa za TANAPA ziletwe za kisasa n.k
=====================
Kupambana na ujangili siyo kazi ndogo!
Hakuna waziri aliyewahi kutoka maskini kwenye wizara hii labda kigwangala awe Wa kwanza!
Mtakumbuka waziri aliyewahi kaa mda mfupi sana kwenye wizara hii bwana. ANTONY DIALO lakini hakutoka mtupu!
Wizara hii unaweza usipewe Rushwa lakini zawadi pekee tu zinatosha kukutajilisha!
wizara ambayo mtu pekee ambaye halipii huduma getini ni mmasai tu wengine wote wanalipia!
Wawekezaji kwenye biashara hii ni watu wazito akiwemo tajili Wa Dunia BILL GATe.
 
Hiyo ya kilo moja ya mamba $300-400..kuna mamba ambao wapo mitoni au ziwani wanaofugwa na wachawi si Mali ya serikali kumbe ni dili hivi nilikuwa sijui.
 
Back
Top Bottom