Kutokana na ushahidi unaoendelea kutolewa mahakamani, kwenye kesi ya ugaidi ya akina Mbowe, Rais Samia huna budi kumstaafisha IGP Sirro

Kiunde chombo huru ,kamisheni au time ku oversee polisi na matumizi ya nguvu

Hao makamanda wa polisi wwnaenda kutestify kama adhabu zitolewe ikwemo kifutwa kazi
 
Unaamini akiondolewa Sirro ndio Polisi watakuwa watenda haki?
 
Ni kweli jeshi la polisi Tanzania linahitaji kufanyiwa overall kubwa mno ili lifanane na majeshi mengine Kama jwtz kiutendaji na Kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa kikatiba katika utekelezaji wa majukumu Yao.
Pia ni muhimu kikaundwa chombo kingine Cha kukagua shughuli zao za Kila siku Kama ilivyo Kwa kada nyingine Kama za ualimu na uhasibu. Mfano, mwalimu anasimamiwa na mwl mkuu, afisaelimu kata, maafisa elimu wilaya na mkoa, TSC na wathibiti ubora wa elimu. Watu wote Hawa wanamkagua mwalimu mmoja TU na kuwa na taarifa zake za kazi za Kila siku na pia wanashauri, kuonya na kuathibu pale mwalimu anapokiuka miongozo ya utendaji kazi. Inakuwaje jeshi la polisi halina idara za kuwathibiti, kuwaonya na hata kuwaadhibu wasitekekeleza kazi Kwa mujibu wa pgo zao?
Nashauri, pamoja na kufumuliwa na kujengwa upya kuanzishwe chombo kingine Cha kuwakagua, kuwaonya na hata kuwaadhibu wanaotenda kazi kinyume Cha taratibu zao yaani wasiozingatia pgo ambayo ndiyo miongozo wao Kama ilivyo muhtasari wa SoMo Kwa walimu.
Tulikuwa tunajiuliza kuhusu watu wasiojulikana,akili za mbayuwayu changanya na zakakwako
 
Back
Top Bottom