Kutokana na mvua inayonyesha Dar,tutegemee kupata mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika kata ya ndugumbi ,Kinondoni

BVR 2015

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
227
410
Kata ya ndugumbi katika manisipaa ya kinondon inakabiliwa na malundo ya uchafu katika nyumba za wakazi wa kata hiyo baada ya wazabuni wanao zoa uchafu kusitisha hiyo huduma zaidi ya miezi 2 sasa. Ukipita mtaani utakuta kuna uchafu mwingi uliolundikana na mbaya zaidi ,wakazi wanaweka hadi kwenye barabara za vichochoroni. Ukiwauliza serikari za mtaa wanadai tatzo lipo manispaa,kwani walishindwa kukubaliana na mzoa taka baada ya kumpandishia ada ya uzoaji na yeye kuona itampa hasara.
Sisi wananchi tunamuomba mkurugenzi aondoe hii kero itatuletea magonjwa ya mlipuko ambayo yatagharimu maisha yetu.
 
Back
Top Bottom