Kutokana na Muujiza ambao Mungu amemtendea Lissu, Taifa zima tunapaswa kuungana na kwenda kumpokea siku ya Jumatatu

Elice Elly

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
1,268
1,593
Taifa Limependelewa na Mungu katika Mambo mengi sana,lakini hakuna Muujiza Mkubwa Mungu ameutenda ndani ya Taifa letu kwa Kumuokoa na kifo mmoja wa Raia wa nchi yetu ambaye alimiminiwa Risasi nyingi na bado Mungu hakuruhusu Roho ya Mh.Lissu kuacha Mwili.

Ili kama Taifa tuonekane tumerudisha Shukrani kwa Mwenyezi Mungu, tunapaswa kila mmoja kumuombea Mh.Lissu lakini kwa namna ya pekee kwenda kwa uwingi kumpokea uwanja wa Ndege Siku ya Jumatatu.

Mungu ni Mkubwa na ametenda makuu kwetu,Siku Lissu anapigwa Risasi zile watu wote wenye dhamiri Hai walihuzunika na kuumizwa na kitendo kile kibaya sana.Sasa Jumatatu kila mmoja aliye chukizwa na kitendo kile ni nafasi ya kuonyesha furaha Yake na.kumrudishia Mungu Utukufu.
KARIBU TENA NYUMBANI MH.TUNDU LISSU.
IMG-20180623-WA0011.jpeg
 
Back
Top Bottom