Kutokana na mishahara kuchelewa TUCTA wanaandaa mgomo mkubwa kwa wafanyakazi wote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutokana na mishahara kuchelewa TUCTA wanaandaa mgomo mkubwa kwa wafanyakazi wote

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MsakaGamba, Nov 29, 2011.

 1. MsakaGamba

  MsakaGamba JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2011
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 392
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nimekutana na mdau mmoja mzito wa Tucta wakiongelea kupanga kuaandaa mgomo mkubwa kutokana na kucheleweshwa mishahara ya wafanyakazi.

  Mpaka sasa wafanya kazi wengi kwenye halmashauri hawajapata mishahara, ki utaratibu wafanya walitakiwa kupata mishahara tarehe 23 na leo ni 29 na hakuna hata dalili ya mishahara hiyo kutoka.

  Kazi kwenu wafanya kazi.
   
 2. mkada

  mkada JF-Expert Member

  #2
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,001
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mbona kama ni wewe ndie unae andaa mgomo!!!!
   
 3. Kisiya Jr.

  Kisiya Jr. Senior Member

  #3
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Toa taarifa kisomi,huyo kiongozi amekaririwa na chombo gani cha habari?
  mgomoni wa wengi kwanini uandaliwe chumbani?
  Mi nadhani we hujajipanga na hiyo taarifa,acha uvivu wa kufikiri,jitume unapoamua kufanaya kazi hasa taarifa kwenye jukwaa la watu makini ka JF.
   
 4. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Mgomo wa kipindi kile waliouandaa ivi ulifanyika??
   
 5. Tundapori

  Tundapori JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2011
  Joined: Aug 12, 2007
  Messages: 521
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  TUCTA hawaruhusiwe kugoma kwa sababu ya Alshababu.
   
 6. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #6
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Kwani hao Al-Shabaab pia wanachukia migomo? Hivi migomo ya TUCTA nayo italeta mikusanyiko
  ya watu? Au hao Al-Shabaab watawafuata wafanyakazi majumbani mwao?
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,593
  Likes Received: 5,775
  Trophy Points: 280
  Mgeni mgeni mgeni mgeni ameingia mgeni hana hiana
  mgeni ameongia mgeni kanyima mishahara mgeni ameingia anwawasha na jf mgeni meingia
  sasa tufanye nini mgeni huyu balaa hata aoni aibu
   
 8. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,675
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mimi natumia NMB Mobile, mpaka jana saa 2 usiku mshahara wangu ulikuwa umeishaingia. Mimi ni mfanyakazi ktk halmashauri iliyoko pembezoni kabisa mwa nchi. So, nahisi ukakasi kama nitakubaliana na wewe moja kwa moja.

  Mimi sio msemaji wa hazina ila kwa kumbukumbu zangu ni kwamba, sio leo wala juzi wafanya kazi wamekuwa wakipata mishahara yao hadi tarehe 5 bila mgomo wa TUCTA wala maandamano. Sasa unapokuja hapa na kusema mgomo hata kabla ya tarehe 30, mimi nitahitaji unidhibitishie kama TUCTA wamepata taarifa rasmi kuwa kuna wafanyaki kiasi kadhaa watacheleweshewa malipo yao.

  Siungi mkono wafanyakazi kucheleweshewa ujira wao, ila mbona imekuwa mapema sana ndugu yangu.

  Ushauri: Humu ni jukwaa la Great Thinkers, mara nyingi great sinkers wanapwaya hapa. Mimi naona FB panakutosha kabisa, tena nibora ukarudi huko mapema kabla wenzio hawajakusahau.
   
 9. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #9
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mrimi umekosea kidogo, ni kweli watumishi wengi wa serikali bado hawajapata mishahara.

  Tatizo ni kubwa hasa kwa wale ambao mishahara yao inaanzia hazina kuu. Wafanyakazi wa halmashauri wanalipwa na halmashauri, hivyo halmashauri yako ikipeleka bank cheki na paylist basi banki inafanya vitu vyake on the spot.

  Sijui kama umeona utofauti lakini?
   
 10. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #10
  Nov 29, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  NATO-no action talking only
   
 11. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #11
  Nov 29, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,675
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kuna thread nyingine ina mada kama hii, na watu wamejaribu kufafanua ukubwa wa tatizo hili, wanaeleweka vizuri na hata mimi sina tatizo katika hilo. Ila jaribu kurejea alichoandika mtoa mada. Amesema TUCTA wanaandaa mgomo kwa kuwa wafanya kazi wengi wa halmashauri hawajalipwa, ndipo nikasema kama ni hili mimi mshahara wangu umeingia tangu jana (bila pungufu). Ni kweli huenda ikawa halmashauri nyingine bado, lakini kwa kurejea kauli yako, basi lawama zitaenda kwnye halmashauri husika.

  Lakini pia issue ya mgomo mbona mapema sana. Mimi na wewe ni mashahidi kwamba swala la watu kulipwa hadi tarehe 5 sio geni.Sioni kama leo tarehe 29 kama inaweza kuwa hoja kuu kwa TUCTA kusimamia. Ndio maana nikahoji kwamba kama mtoa mada
  anaweza kudhibitisha hapa iwapo officially TUCTA wamepewa taarifa ya kucheleweshwa kwa mishahara. Kama utakumbuka, TUCTA ni chama ambacho kinaendesha mambo kwa kufuata sheria hasa linapokuja swala nyeti kama hili la mgomo.

  Nasisitiza siungi mkono wafanyakazi kucheleweshewa ujira wao. Ila napingana na hizi taarifa dhaifu zisizokuwa na mashiko.

  Sijui kama nimeeleweka?
   
 12. s

  semako Senior Member

  #12
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TUCTA?Hivi hujui kazi moja wapo ya TUCTA ni kuzuia migomo ya wafanyakazi?
   
Loading...