Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,013
- 144,371
Kama ambavyo yule mama aliekuwa Mkurugenzi wa SSRA alivyoendolewa katika nafasi yake kutokana na issue ya kikokotoo, ndivyo hivyo Waziri wa Mambo ya Nje, Prof. Kabudi atavyoweza kuondolewa kwenye hiyo wizara kutokana na matamshi yake juu ya wabunge wa Bunge la Ulaya.
Kama ambavyo sitaki kuamini yule mama aliekuwa boss wa SSRA alifanya maamuzi yale bila baraka za wakubwa, ndivyo ambavyo sitakuwa tayari kuamini Prof. Kabudi kaongea aliyoyaongea bila baraka za wakubwa wake, ila kama alivyopigwa chini yule mama, ndivyo ambavyo hata Prof. Kabudi nae anaweza kupigwa chini.
Kwa sasa ninahakika mzee Baba atakuwa anasoma upepo na akiona unavuma vibaya, basi ni swala la muda tu kabla hatujaona Msigwa akija na Press release ya mtu kutenguliwa ingawa bado anaweza kupewa wizara nyingine baraza kamili litapotangazwa.
Hata hivyo, kwa siku hizi za mwanzo, msishangae Mzee Baba nae akaja na kauli kama za msaidizi wake, ila moto ukiwaka, atageuka na ataanza kwa kumtoa huyo msaidizi wake katika hiyo nafasi.
Kwahiyo hapa tutegemee scenario mbili: moja ni Kabudi kuondolewa kulingana na upepo utavyovuma, na scenario ya pili ni boss wake kuja kupigilia msumari matamshi ya Kabudi na baadae kugeuka na kuchukua hatua iwapo bwana wakubwa hawa watakuja juu. Ni swala la muda tu kabla haya hayajatimia.
Yakitokea kama navyotabiri, hawa MATAGA ambao leo hii wanamshangilia Kabudi, ndio watakuwa wa kwanza kumpongeza Mzee Baba na kuanza kamponda Kabudi.
Kabla sijamaliza, naomba niwape na scenario ya tatu: Kabla jua halijazama, Kabudi anaweza kujitokeza hadharani na kusema amenukuliwa vibaya ingawa hii haitamsaidia litapokuja swala la kutolewa mbuzi wa kafara.
Time will tell.