Kutokana na matamshi yake, Prof. Kabudi ataondolewa Wizara ya Mambo ya Nje kama ilivyokuwa kwa Mkurugenzi wa SSRA kutokana na issue ya Kikokotoo

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
40,831
2,000
Kama ambavyo yule mama aliekuwa Mkurugenzi wa SSRA alivyoendolewa katika nafasi yake kutokana na issue ya kikokotoo, ndivyo hivyo Waziri wa Mambo ya Nje, Prof. Kabudi atavyoweza kuondolewa kwenye hiyo wizara kutokana na matamshi yake juu ya wabunge wa Bunge la Ulaya.

Kama ambavyo sitaki kuamini yule mama aliekuwa boss wa SSRA alifanya maamuzi yale bila baraka za wakubwa, ndivyo ambavyo sitakuwa tayari kuamini Prof. Kabudi kaongea aliyoyaongea bila baraka za wakubwa wake, ila kama alivyopigwa chini yule mama, ndivyo ambavyo hata Prof. Kabudi nae anaweza kupigwa chini.

Kwa sasa ninahakika mzee Baba atakuwa anasoma upepo na akiona unavuma vibaya, basi ni swala la muda tu kabla hatujaona Msigwa akija na Press release ya mtu kutenguliwa ingawa bado anaweza kupewa wizara nyingine baraza kamili litapotangazwa.

Hata hivyo, kwa siku hizi za mwanzo, msishangae Mzee Baba nae akaja na kauli kama za msaidizi wake, ila moto ukiwaka, atageuka na ataanza kwa kumtoa huyo msaidizi wake katika hiyo nafasi.

Kwahiyo hapa tutegemee scenario mbili: moja ni Kabudi kuondolewa kulingana na upepo utavyovuma, na scenario ya pili ni boss wake kuja kupigilia msumari matamshi ya Kabudi na baadae kugeuka na kuchukua hatua iwapo bwana wakubwa hawa watakuja juu. Ni swala la muda tu kabla haya hayajatimia.

Yakitokea kama navyotabiri, hawa MATAGA ambao leo hii wanamshangilia Kabudi, ndio watakuwa wa kwanza kumpongeza Mzee Baba na kuanza kamponda Kabudi.

Kabla sijamaliza, naomba niwape na scenario ya tatu: Kabla jua halijazama, Kabudi anaweza kujitokeza hadharani na kusema amenukuliwa vibaya ingawa hii haitamsaidia litapokuja swala la kutolewa mbuzi wa kafara.

Time will tell.
 

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
7,893
2,000
Prof Kabudi ni mtaalamu na bingwa, asiye na mfano katika Taifa hili, kuhusu masuala uliyoyataja. Hivyo basi Mkuu Salary Slip utaomba dua sana na kusubiri zijibiwe bila mafanikio.

Labda umesahau mapema tu, kwamba ulijiaminishi hao viongozi wako, wanasiasa uchwara kwa kuwa hawakusoma nyakati, watashinda katika Uchaguzi Mkuu, matokeo yake wakashindwa vibaya.
 

rommy shabby

JF-Expert Member
Jun 26, 2017
766
1,000
Apige kazi tu hakuna kuangalia nyuma
Prof Kabudi ni mtaalamu na bingwa, asiye na mfano katika Taifa hili, kuhusu masuala uliyoyataja. Hivyo basi Mkuu Salary Slip utaomba dua sana na kusubiri zijibiwe bila mafanikio.

Labda unesahau mapema tu, kwamba ulijiaminishi hao viongozi wako, wanasiasa uchwara kwa kuwa hawakusoma nyakati, watashinda katika Uchaguzi Mkuu, matokeo yake wakashindwa vibaya.
 

Iblis Bin Shetan

JF-Expert Member
Sep 24, 2018
545
500
Kwa yale maneno yake ya jana nimeshangaa yaan kweli kusoma sio kuelimika bali kupata kazi na Kabudu amethibitisha hilo.

Mnaulizwa kuhusu ufisadi wa Kula hela za watu alitakiwa amjib kuhusu euro million 27 zimetumikaje yeye anenda kuparangaparanga maneno kama anatoka kutoa mzigo chooni.

Yaan utapeli hela za watu wenyewe hata wasiulize huo utakuwa ujinga wa kiwango cha juu.
 

Maneno Meier

JF-Expert Member
May 12, 2013
1,940
2,000
Huna jambo jingine zuri la kuzungumzia zaidi ya kutafuta makosa ya viongozi ili usikie wakitumbuliwa? Huo mimi binafsi ninauita umasikini wa akili. Wewe ni kiumbe mfu na mzigo kwa Taifa letu. Ningekushauri jichimbie mwenyewe kaburu ujizike.

Lete Story nzuri kuhusu sayansi ya leo ili vijana wetu wasisimue ubongo wao badala ya kuspeculate mambo ya kike ambayo hayana tija. Kwani ulisikia Professor Kabudi ni robotor ambayo ikiwa programed inafanya kazi tu bila kukosea? Kama binadam kwanini asikosee? Kama kweli kuna kosa kwenye hotuba yake ya jana.

Mbali na hayo huyo mtumbuaji wako yeye ni mungu? Naye hafanyi makosa? Usipende ku m-demonize Rais wetu kana kwamba yeye hana soul.
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
27,473
2,000
Sasa hivi wadau wa maendeleo hawaitwi tena ni mabeberu,wanaitwa ni hooligans neno ambalo wanalijua vyema kwa sababu lipo katika lugha yao.Tanzania ni Taifa ambalo lipo chini ya mfalme juha.Watakao bear cost za ujinga wote huu ni wananchi wanyonge.
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
27,473
2,000
Ila kabudi hyo wizara imemshinda uwezo na akili kulikuwa Kuna haja gani kuwaita hao wabunge wa EU wapuuzi wakati EU michango yake kwa taifa ni muhimu, ni Bora hyo wizara ingempata January Makamba naona anafaa ana exposure flani hivi
Usichokijua ni kwamba mawaziri wa Magufuli hawafanyi kazi kwa utashi wao wala kwa kuwa huru.Huwa wanafanya kazi kwa kuangalia boss wao anataka nini na huwa anafurahishwa na kitu gani.Ile siyo akili ya Kabudi,ile ni akili ya Magufuli ipo kwenye kichwa cha Kabudi.Usipokuwa makini unaweza kufikiri kuwa ni Kabudi anaongea kumbe anaeongea pale ni Magufuli.
 

Maneno Meier

JF-Expert Member
May 12, 2013
1,940
2,000
Sasa hivi wadau wa maendeleo hawaitwi tena ni mabeberu,wanaitwa ni hooligans neno ambalo wanalijua vyema kwa sababu lipo katika lugha yao.Tanzania ni Taifa ambalo lipo chini ya mfalme juha.Watakao bear cost za ujinga wote huu ni wananchi wanyonge.
Kwa lipi?
 

cariha

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
13,846
2,000
Usichokijua ni kwamba mawaziri wa Magufuli hawafanyi kazi kwa utashi wao wala kwa kuwa huru.Huwa wanafanya kazi kwa kuangalia boss wao anataka nini na huwa anafurahishwa na kitu gani.Ile siyo akili ya Kabudi,ile ni akili ya Magufuli ipo kwenye kichwa cha Kabudi.Usipokuwa makini unaweza kufikiri kuwa ni Kabudi anaongea kumbe anaeongea ni Magufuli
Dah sasa ka waziri wa wizara ya nje kaharibu, Tanzania umaskini bado mkubwa then unaenda kutukana wahisani huku baadae unawalilia shida ka si kurogwa huko nini, tabia ya kujifanya maskini jeuri na kibri mwisho kuumiza nchi yako na Raia wako wanaoishi kwa shida.
 

Maneno Meier

JF-Expert Member
May 12, 2013
1,940
2,000
Ila kabudi hyo wizara imemshinda uwezo na akili kulikuwa Kuna haja gani kuwaita hao wabunge wa EU wapuuzi wakati EU michango yake kwa taifa ni muhimu, ni Bora hyo wizara ingempata January Makamba naona anafaa ana exposure flani hivi
Umemwona huyo mbunge wa kutoka hicho chama cha CDU cha Ujerumani jinsi alivyo? Basi kama hujamwona angalia hii pic hapa utajua ni mtu wa aina gani.

Watu wenye mwonekano wa aina hii huko kwao Ujerumani wanaitwa Penner. Penner ni mtu ambaye anapenda dana kulala lala, ni mtu ambaye amesha give up maisha yake.
"unpleasant person or disgusting guy"
Ni mtu ambaye hataki kufanya kazi, mvivu, mlevi, anakula vyakula vya kutoka kwenye mapipa ya taka na analala popote pale. Hana makazi.

Kwako wewe mkamba usiye wajua wazungu unamwona mtu wa maana kwa sababu ya kukosa ufahamu. Unasikitisha. Unajifanya unajua kumbe huna lolote ni mbambaishaji tu.
SmartSelect_20201122-073532_Chrome.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom